TAASISI ZA FEDHA ZIMEOMBWA KURAHISISHA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WALEMAVU

October 25, 2023

 





Na Pamela Mollel,Arusha 


Taasisi za Fedha zimeombwa  kurahisisha huduma  za kifedha Kwa watu wenye ulemavu hususan wa macho.


Hayo yamesemwa kwenye  Mkutano wa  wiki ya azaki  unaoendelea  jijinibl Arusha  ambapo wameomba kupatiwa mfumo shirikishi utakaowasaidia kwenye utumiaji wa Teknolojia katika  eneo la kifedha.


Mmoja wa walemavu wa macho  Renatusi  Rupoli   kutoka Iringa amesema   watu wasioona huwa wanatumia  mitandao kwa njia ya sauti ambapo alihoji kwanini kusiwepo na Software  kama hizo  ambazo zinajumlishwa  kwenye Mashine za Kutolea pesa (ATM)  Benki    Ili  kupunguza  usumbufu wakutafuta wasaidizi wakati wa kutumia huduma hizo.


Akizungumza katika Mkutano huo Amali Baziadi kutoka Benki ya Stanbic  amesema changamoto hiyo ameichukua na kwamba wataona namna gani yakulifanyia kazi ili kupata ufumbuzi.


"Ninaimani kuwa siyo tu Stanbic pekee ambao hatuna huduma hii lakini naichukua kama changamoto na tuone namna gani tunaifanyia kazi ili kuwawezesha wateja wetu kupata huduma rafiki kwao"amesema Baziadi.


Aidha wadau hao  wameshauri kuwepo kwa huduma rafiki Kwa wazee na wananchi waishio Vijijini namna ambavyo wanaweza kufungua akaunti za Benki kwa kutumia mitandao badala ya kufuata huduma hizo kwa mawakala wa Benki ambao mara nyingi hupatikana mijini.




Mwishooo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »