Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda cha mbolea cha ITRACOM Fertilizer Limited kwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba wafanyakazi, Usalama na afya mahali pa kazi na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wakati.
Prof.Ndalichako ameyasema hayo Septemba 18, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Sheria za kazi, ambapo amewataka wawekaji nchini kuiga mfano kwa ITRACOM
Waziri Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya wawekezaji nchini , uwekezaji wa kiwanda hicho cha mbolea umezalisha ajira za awali 1,198 na kitakapokamilika ajira moja za kwa moja 3500 zitazalishwa na ambazo sio za moja kwa moja zitazalishwa ajira 8000.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ameahidi kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili uwekezaji wa kiwanda hicho uweze kukamilika kwa wakati na kuwa na tija kwa wananchi.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kiwanda hicho, Kimaramuziro Nkurikiye ameshukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye ujenzi wa kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo maji, Umeme, na Barabara.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri akieleza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoani Dodoma akiambatana na Viongozi wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na watendaji wengine katika kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisikiliza maelezo kuhusu aina ya mbolea zinazozalishwa kiwandani hapo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Biashara na Masoko wa Kiwanda cha uzalishaji mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Dkt. Keneth Masuke wakati wa ziara hiyo.
Msimamizi Mitambo wa kiwanda cha uzalishaji Mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Eng. Peter Nchuma (wa pili kushoto) akielezea uzalishaji wa Mchanga aina ya Phosphete unaotumika kutoa sumu kwenye ardhi kabla ya kupanda mazao.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea cha Itrocom Fertilizer Limited wakati wa ziara hiyo.
EmoticonEmoticon