JESHI LA POLISI TANGA LAIPONGEZA SHIRIKA LA AMED TANZANIA KWA HATUA WALIZOCHUKUA KUKABILIANA NA AJALI ZA BARABARANI

August 17, 2023

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga William Mwamasika akizungumza  baada ya kumaliza kwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto( Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.
Meneja wa Shirika la  Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza 









Na Oscar Assenga, Tanga

JESHI la Polisi Mkoani Tanga Kitengo cha Usalama Barabarani limepongezwa kwa hatua walizochukua kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupelekea mpango kazi wa Usalama Barabarani kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga uliokuwa unatekelezwa na Shirika la Amend Tanzania kufikia asilimia 90

Pongezi hizo zilitolewa leo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani William Mwamasika baada ya kumaliza kwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto( Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Mahakama ya Watoto ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi huo sambamba na kuweka alama na michoro ya barabarani zinazopita kwenye baadhi ya Shule za msingi katika Jiji la Tanga.

Alisema mpango huo ulikuwa ni Shirika la Amend Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani huku akisema bodaboda katika Jiji la Tanga zinachangia ajali kwa kiwango kikubwa

“Hivyo niwaombe waendesha vyombo vya moto kuheshimu sheria za usalama barabarani kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ajali za barabarani au kuzitokomeza kabisa”Alisema

Mkuu huyu wa Kikosi cha Usalama barabarani pia alitoa rai kwa wazazi na walezi kutokubali wanafunzi kupakiwa mishikaki kwenye bodaboda aidha wakati wa kwenda shule au kurudi nyumbani kwani ikitokea ajali msiba wake utakuwa mkubwa na wenye kuumiza.

Awali akizungumza Meneja wa Amend Tanzania Simon Kalolo baada ya kumaliza kwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto (Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.

Mahakama ya Watoto ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi huo sambamba na kuweka alama na michoro ya barabarani zinazopita kwenye baadhi ya Shule za msingi katika Jiji la Tanga.

Alisema Amend imekuwa ikijishughulisha na usalama barabarani nchini tangu mwaka 2009 na kwa ufadhili wa Shirika la Fondation Botnar jijini Tanga,wanashirikiana na Halmashauri ya Jiji hilo kuboresha miundombinu ya barabara maeneo ya shule.

Aidha alisema wamekuwa wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi, kuanzisha klabu za usalama barabarani na mahakama kifani za watoto, mafunzo kwa madereva pikipiki , kuandaa makongamano ya wadau wa usalama barabarani, kufanya tafiti huhusu ajali za barabarani, na kuandaa Mpango Kazi wa usalama barabarani kwa Jiji hilo.

Alisema mpango kazi huo wa usalama wa usalama barabarani ulikuwa na lengo la kuboresha safari salama na endelevu kwa Jiji la Tanga uliozinduliwa Novemba 11, 2022 na tangu ulipozinduliwa kuna mambo kadha yametekelezwa.

" Baada ya uzinduzi huo tumefanikiwa kuzindua miundumbinu katika shule tatu za msingi za Shaaban Robert, Mabawa na Majengo. Pia kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi 3,501 wa shule za msingi Mabawa, Majengo na Shabaan Robert na wengine 3,247 wa shule za sekondari Toledi, Kihere na Kiomoni.

Hata hivyo alisema kupitia mpango huo wameanzisha klabu mbili za shule za usalama barabarani katika Shule ya Msingi Usagara na klabu ya usalama wa baiskeli katika Shule ya Sekondari Usagara, yenye watoto 20 katika kila klabu.

“Tumetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hawa, baada ya kuhitimu kuwa mabalozi, wakipokea vyeti katika hafla ndogo.Shughuli za vilabu hivi zimejumuisha mafunzo, midahalo ya usalama barabarani," Alisema.

Pia alisema wametoa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki 350 kufanya jumla ya madereva waliopata mafunzo haya kufikia 950.

Kalolo alisema Februari mwaka huu wamesambaza vifaa vya kufundishia usalama barabarani kwa maofisa maendeleo ya jamii katika kata 22 kati ya 27 za Jiji la Tanga.

Aliongeza Juni mwaka huu maofisa maendeleo ya jamii walikuwa wamezungumza kuhusu usalama barabarani katika zaidi ya mikutano au matukio 50 tofauti, na kuelimisha jumla ya takriban wananchi 6,600.

Hata hivyo alisema wamekamilisha uwekaji wa miundombinu ya waenda kwa miguu katika eneo moja lenye shule tatu za msingi na kwamba lengo kuu ilikuwa kupunguza mwendo wa vyombo vya moto hadi chini ya 30km/h na kuwapa watoto mahali salama pa kutembea na kuvuka."

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo Mayasa Said amesema baada ya wanafunzi na walimu kupatiwa elimu ya usalama barabarani sambamba na kuwekwa kwa alama zinazowawezeha wanafunzi kuvuka kwa usalama ajali zimepungua, hivyo wanaishukuru Amend kwa kupeleka mpango huo jijini Tanga.

Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »