BENKI YA NMB KUENDELEA KUTOA MIKOPO KWA WAENDESHA BODABODA NA BAJAJI LENGO KUWAEPUSHA NA MIKATABA YA KINYONYAJI

May 25, 2023



Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa halfa hiyo


Sehemu ya Waendesha pikipiki alimaarufu Bodaboda na Bajaj wakimsikiliza kwa umakini Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga katika kikao ambacho kiliitishwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga


Na Oscar Assenga,TANGA

BENKI ya NMB tawi la Madaraka Jijini Tanga limeadhimia kuendelea kutoa Mikopo kwa waendesha Bodaboda na Bajaji kwa lengo la kuwaepusha kujiingiza kwenye mikataba ya kinyonyaji hatua ambayo imechangia kudoofisha jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.


Meneja wa NMB tawi la Mdaraka Jijini Tanga, Elizabeth Chawinga akieleza mipango ya benki hiyo kuwakwamua kiuchumi waendesha bodaboda na bajaji  kwenye kikao maalum kilichowahusisha Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, viongozi wa bodaboda,bajaji na wamiliki kilichofanyika katika Bwalo la Polisi Mkoani Tanga.

Katika kikao hicho, Meneja huyo wa NMB alisema, benki yake tayari imeshaanza utaratibu wa kutoa mikopo kwa waendesha bodaboda hatua ambayo lengo lake ni kuwakwamua kiuchumi na kuwaondoshea changamoto ya kuingia kwenye mikopo yenye mikataba migumu.

“ NMB tunaendelea kutoa mikopo kwa bodaboda na bajaji, tayari tumetoa bajaji na guta,hivyo karibuni sana, wahusika lazima wafuate taratibu ikiwemo kuwa na leseni ya kutumia chombo cha moto,uthibitisho wa wenyeviti wa mitaa na taratibu nyingine muhimu”alisema Chawinga.

Meneja huyo wa Benki ya NMB tawi la Madaraka aliendelea kusema kwamba, kupitia utaratibu huo wa utoaji mikopo ya vitendea kazi hivyo wataweza kuwakomboa wajasiriamali hao huku akiwasihi kufungua Akaunti kwenye taasisi hiyo ya fedha ili kupata huduma stahiki kirahisi.

Kwa mujibu wa Chawinga, mikopo hiyo inaendelea kutolewa kwa waendesha Bajaji na Bodaboda ni yenye masharti nafuu na mkopaji atakuwa akilazimika kulipa kwa Wiki hadi pale atakapokuwa amefanikiwa kumaliza deni lake kwenye benki hiyo ya NMB tawi la Madaraka.

Aidha Chawinga alisema kwamba,huduma hiyo kwa wajasiriamali hao itakuwa endelevu huku akitoa wito kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo inayopatikana kwenye benki hiyo ambayo imejipambanua katika kuwakomboa Wananchi wenye kipato cha chini.

NMB mbali na kuhusika kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo yenye Masharti nafuu wafanyabiashara wadogo lakni pia imekuja na huduma mbalimbali likiwemo suala la utoaji wa Bima hatua ambayo lengo lake ni kulipa fidia kwa wahanga pindi majanga yanapowakuta,

Mwisho.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »