NA MWANDISHI
WETU, KIBAHA
MKUU wa Mkoa wa
Pwani Alhaj Aboubakar Kunenge amehimiza ushirikiano baina ya Taasisi za Umma,
Binafsi na watendaji kwenye Halmashauri ili kazi ya kuwatumikia wananchi iwe
rahisi.
Ameyasema hayo
wakati akifungua semina ya kujenga uelewa wa shughuli za taasisi mbalimbali za
umma na binafsi ikiwemo Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) na watendaji
kutoka Halmashauri za Mkoa wa Pwani Machi 30, 2023.
GBT ni taasisi
ya Kiserikali ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikisimamiwa na
Msajili wa Hazina. (TR).
RC Kunenge alisema wataalamu
lazima wajue viongozi wa kisiasa hawawezi kuwa na maamuzi mazuri kama wataalamu
hawatafanya kazi ya kitaalamu inavyotakiwa.
“Lazima tuelewe, serikali ni
moja, mlipaji ni mmoja, fedha inatoka fungu moja na inavyopatikana iwe ni
Halmashauri au Bodi ya Michezo ya kubahatisha yote inaingia sehemu moja kwa
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha au PST.” Alisema na kuongeza ….
Haiwezekani
kwenye Halmashauri kukawa na watendaji kutoka kila taasisi ya serikali na
kushauri ili utendaji wa taasisi hizo kwenye maeneo ambayo ni vigumu kwa
watendaji wao kuwepo ili kuwatumikia wananchi ni vema kukawepo na makubaliano
yatakayowezesha utendaji kazi ukawa rahisi bila ya vikwazo, alifafanua Alhaj
Kunenge ambaye alifuatana na Wakuu wote wa wilaya za Mkoa huo.
“Kama tuna
majukumu ambayo tunaweza kufanya kwa niaba ya wenzetu mnaweza kukasimu shughuli
zenu na zikafanywa na watu wa Halmashauri, lazima tufanye kazi kwa kushirikiana kwani serikali ni
moja.” Alisema.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bw. James Mbalwe
alisema Bodi imefika Mkoani humo kwa lengo la kujitambulisha rasmi kwa
watendaji wa Mkoa ili kuongeza ufahamu wa kamati, uwepo wa taasisi na kuongeza
ufahamu juu ya usimamizi na uendeshaji wa michezo ya kubahatisha hapa nchini.
Pia kuimarisha
ushirikiano katika usimamizi na udhibiti wa sekta na kuomba kamati ya Ulinz na Usalama
ya Mkoa kushirikiana na GBT ili kudhibiti wavunjaji wa sheria ya michezo ya
kubahatisha hapa mkoa wa Pwani, alisema Bw. Mbalwe.
Alisema wanaona
umuhimu wa kutoa elimu mara kwa mara kwa vile GBT ni taasisi change iliyoanzishwa
mwaka 2003
Alisema semina
kama hizo zimekuwa na manufaa makubwa katika kurahisisha utendaji wa GBT na
kutolea mfano Mkoa wa Kigoma ambako baada ya kutolewa elimu kama hiyo utendaji wa Michezo ya Kubahatisha Mkoani humo imekuwa rahisi.
“Kazi yetu ni
udhibiti, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini na ieleweke kuwa GBT haifanyi biashara na iko chini ya Wizara ya Fedha chini ya Msajili wa Hazina.”
Alifafanua
Bw. Mbalwe alihimiza kuimarisha
ushirikiano katika usimamizi wa sekta na kuiomba kamati ya usalama ya
mkoa kuongeza ushirikiano zaidi katika kudhibiti wavunja sheria ya Michezo ya
Kubahatisha.
“Nina sisitiza
Michezo ya Kubahatisha ni Burudani na sio Ajira au njia ya kujitafutia kipato.”
Alifafanua Bw. Mbalwe.
Kuanzishwa kwa
GBT kumewezesha sekta ya michezo ya kubahatisha kuratibiwa vizuri zaidi na
iweze kuchangia ipasavyo katika pato la taifa na wananchi wanaojishughulisha
kwenye michezo hiyo wanalindwa ipasavyo.
“Sekta inakuwa
kwa kasi na kwa sababu hiyo kunahitaji uratibu makini ili iendelee kukua katika
namna ambayo utaratibu unaopasa bila kupoteza malengo ya msingi ya kuanzishwa
kwake.” Alifafanua Bw. Mbalwe.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar Kunenge akifungua semina hiyo kwenye Mji wa Kibaha Machi 30, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Bw. James Mbalwe akizunguzma kwenye semina hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine kutoka Halmashauri za Mkoa huo
Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe (wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Huduma za (DCS) Bw. Daniel Ole Sumayan (katikati) na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Matekelezo Bw. Sadick Elimsu
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar Kunenge (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe (wapili kushoto) Mkurugenzi wa Masuala ya Shirika, Bw. Daniel Ole Sumayan (wakwanza kushoto). Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Mchatta.
Picha ya pamoja
Share this
EmoticonEmoticon