WAZIRI UMMY MGENI RASMI MATEMBEZI YA KILOMITA 5 JIJINI TANGA

February 28, 2023




Na Mwandishi Wetu,Tanga


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  mazoezi ya viungo na matembezi ya umbali wa kilomita tano (5km) yenye kauli mbiu " Tembea na JKCI - Linda Afya ya Moyo Wako" yatafanyika Machi 11 mwaka huu yatakayoanzia kwenye viwanja vya NIMR Bombo Hospitali.


Matembezi hayo yameandaliwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya JKCI 


Akizungumza kuhusu matembezi hayo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Zakaria alisema maandalizi yamekamilika.


Dkt Naima alisema  matembezi hayo yataanza saa 12:30 asubuhi hadi saa 2:30 asubuhi yatakayokwenda sambamba na ufungaji wa kambi upimaji.


Alisema matembezi hayo yataanzia kwenye viwanja vya NIMR Bombo Hospitali kupitia Mkonge Hotel, Raskazone Polisi hadi Nyinda Classic kuelekea Ukuta wa Mbolea (GBP), Masai Utalii College, Lulu Image,Tanga International School, Splended, Tanesco, Toyota Mataa na kumalizikia Bombo Hospitali Viwanja vya Mapokezi.


Hata hivyo Dkt Naima alivitaka vilabu vya mazoezi viweze kushiriki nao pamoja katika ufanyaji wa mazoezi ili kulinda Afya ya Moyo sambamba na kupunguza athari zinazotokana na  magonjwa yasiyo ambukiza kwa jamii.


Mwisho


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »