MHE. KATAMBI : MAPITIO YA SERA YA WATU WENYE ULEMAVU YAMEANZA

MHE. KATAMBI : MAPITIO YA SERA YA WATU WENYE ULEMAVU YAMEANZA

October 31, 2023

 


 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akijibu swali Bungeni leo tarehe 31, Oktoba, 2023, wakati wa Kikao cha Kwanza, Mkutano wa 13 wa Bunge la 12, jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakati akijibu maswali Bungeni leo tarehe 31, 2023, wakati wa Kikao cha Kwanza, Mkutano wa Kumi na Tatu, Bunge la 12, jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Pindi Chana.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali imeanza kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 2004 ili kukidhi mahitaji yaliyopo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi ameyasema hayo Oktoba 31, 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti maalum (CCM), Mhe. Stella Ikupa ambaye amehoji mkakati wa serikali kufanya marekebisho ya Sheria namba 9 ya Mwaka 2010 ya Watu Wenye Ulemavu.

Akijibu swali hilo, Mhe.Katambi amesema mkakati wa serikali kwa sasa ni kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 2004 ambapo utekelezaji wake umeanza.

Aidha, amesema baada ya kukamilika kwa mapitio ya Sera ya Mwaka 2004 hatua za marekebisho ya Sheria hiyo zitaanza kwa kuzingatia mapungufu yatakayobainishwa katika tathmini ya utekelezaji wa Sera hiyo.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti maalum (CCM), Mhe.Mariam Kisangi amehoji serikali imejipangaje kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu ili kutoa maoni kwenye mapitio hayo.

Mhe.Katambi akijibu swali hilo, amesema mapitio ya sera yanatarajiwa kukamilika Mwaka huu na yamekuwa shirikishi kwa makundi yote ya watu wenye ulemavu.

WAZIRI MKENDA AONGOZA TEAM YA TANZANIA MKUTANO WA ACAT

October 31, 2023

Na: Calvin Gwabara – Nairobi.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameongoza timu
ya Serikali ya Tanzania kwenye mkutano mkubwa wa Teknolojia za Kilimo
Afrika (ACAT) ulioanza leo jumatatu nchini Kenya.


Mara baada ya kufika kwenye viwanja vya mkutano huo mkubwa
akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Balozi Dkt. Benard
Yohana Kibesse pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu na watumishi wengine wa
Serikali ametembelea maonesho mbalimbali ya Teknolojia za kilimo
zinazooneshwa nje ya mkutano huo.


“Nimeona maonesho ambayo kimsingi ni kuhusu jinsi Sayansi na
Teknolojia inavyoweza kuleta mabadiliko chanya kwenye kilimo pamoja na
ukweli huu tumeona pia umuhimu wa kuzingatia usalama na afya kwenye
mabadiliko haya na pia kuchukua tahadhari tusipoteze umiliki wa yale
tunayogundua, hasa mbegu bora, ili tusiingie kwenye utegemezi
utakaotudhoofisha” alisema Prof. Mkenda.


Tanzania kupitia wizara yake ya Elimu Sayansi na Teknolojia na taasisi
zilizo chini yake imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi
inawezesha wabunifu kupitia Programu zake mbalimbali ikimwemo.


Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu ( MAKISATU)
ambayo yanafanyika kila mwaka kwa kuhusisha wabunifu mbalimbali
kuanzia kwenye jamii, Shule za Msingi na Sekondari, Vyuo Vya kati, Vikuu
pamoja na Taasisi za Utafiti na kuwapatia washindi fedha na mahitaji
mengine ili kuwezesha kukuza bunifu zao na kuzibiasharisha.


Mkutano huo utazinduliwa siku ya jumanne ya tarehe 31/10/2023 na Rais
wa Jamhuri ya watu wa Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na
kuhudhiriwa na mamia ya wadau wa kilimo kutoka Afrika na Dunia nzima.


Aidha Mkutano huo wa (ACAT) umeandaliwa na Serikali ya Kenya kupitia
Wizara yake ya Kilimo na Maendeleo ya Ufugaji kwa kushirikiana na
Taasisi ya Teknolojia za Kilimo Afrika (AATF)








TANZANIA, UJERUMAN KUZUNGUMZA JINSI YA KUREJESHA MABAKI MIILI YA WATANZANIA ILIYOPO NCHINI HUMO

October 31, 2023

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.


-Rais Samia asema ndugu wanasubiri  mabaki ya miili ya wapendwa wao,  aishukuru Ujeruman

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SERIKALI za nchi za Tanzania na Ujeruman zimesema  zitafanya  mazungumzo yatakayowezesha mabaki ya miili ya watanzania walipoteza maisha wakati wa ukoloni yaliyopo nchini Ujerumani yanarejeshwa nchini.

Kwa muda mrefu mabaki ya miili hiyo ya Watanzania imehifadhiwa katika makumbusho mbalimbali nchini Ujerumani na sasa uamuzi wa kuyarejesha umefikia hatua nzuri na hatimaye mabaki hayo yarejeshwe na kukabidhiwa kwa ndugu.

Ikumbukwe kwamba baadhi ya mabaki hayo ni ya miili ya machifu na viongozi waliokuwa vinara katika vita vya Tanganyika dhidi ya Ujerumani (Maji Maji).

Akizungumza leo Oktoba 31, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Ujerumani  Frank-Walter Steinmeier amesema katika mazungumzo yao wamezungumza masuala mbalimbali likiwemo kurejeshwa kwa mabaki hayo.

"Nakushukuru Rais Frank - Walter Steinmeier kwa kukubali mualiko wangu wa kuja kufanya ziara nchini,  huu ni uthibitisho wa uhusiano mzuri  kwa miaka miaka 60 baina ya nchi hizi.

"Katika mazungumzo yetu tumejadili masuala mbalimbali lakini tumezungumzia kuhusu mabaki ya wapendwa wetu walioko Ujerumani ,  tunaendelea kuzungumza ili mabaki ya miili ya wapendwa wetu irejee nyumbani Tanzania.

Wakati anazungumzia mabaki hayo , Rais Dk.Samia amesema anajua kuna familia ambazo zinasubiri mabaki ya miili ya ndugu zao ambayo yapo kwenye   makumbusho za Ujerumani, lakini sasa wanakwenda   kuyazungumza ili yaweze kurudishwa Tanzania.

Akielezea zaidi kuhusu mazungumzo kati yake na Rais Steinmeier, Rais Samia amesema wamezungumza kuhusu kuendelea kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili sambamba na kushirikiana katika nyanja mbalimbali kama elimu, afya, uhifadhi , kilimo, sekta ya ubunifu na maeneo mengine ambayo wamekuwa wakishirikiana.

Aidha Rais Samia ameishukuru nchi ya Ujeruman kwa misaada mbalimbali waliyoitoa na wanayoendelea kuitoa kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali akitolea mfano kuwa katika eneo la Bima ya Afya kwa Wote nchi hiyo iliahidi kusaidia lakini wanaendelea na ujenzi wa hospitali kubwa Dodoma.

"Ujeruman wamekuwa wakitusaidia katika maeneo mbalimbali,  mbali ya ujenzi wa hospitali pale Dodoma lakini Ujeruman wametusaidia kujenga Hospitali Lugalo.Pia wamekuwa wakitusaidia katika uhifadhi katika hifadhi ya Serengeti na Selous.

Kwa upande wake Rais wa Ujeruman Steinmeier amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kumualika kufanya ziara nchini huku akielezea namna ambavyo wamekuwa na mazungumzo mazuri yanayolenga kuimarisha uhusiano na kushirikiana katika sekta mbalimbali.

Kuhusu mabaki ya miili ya watanzania yaliyoko nchini Ujeruman amesema hilo ni jambo ambalo linazungumzika na watafikia pazuri huku katika hilo litaambatana na kupeleka Ujerumani taarifa za hali za wahanga wa vita vya majimaji ambao natarajia kukutana nao kesho.

" Nitakwenda kukutana na wahanga wa vita , nitawasikiliza na yale ambayo watanieleza nitakwenda nayo Ujeruman ili kufikisha ujumbe wao, "amesema huku akieleza ni vema pia nchi hizo  kutosahau historia ya mambo yaliyopita na kubwa zaidi kudumisha uhusiano .

Pia amesema katika eneo la ubunifu,  amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwasaidia wabunifu wachanga ili kukuza bunifu zao lakini amesisitiza kuendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

MUSWADA BIMA YA AFYA KWA WOTE KUTINGA BUNGENI KESHO

October 31, 2023

Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kurejea Bungeni tena hapo kesho Novemba 1 2023 na Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao ulikwama mnamo Mwezi Februari 2023 kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha kutekeleza Mpango huo.



Muswada huu ni ndoto ya Serikali ya miaka mingi ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha huduma bora za afya kuanzia ngazi ya Taifa hadi ya msingi kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu zaidi na maeneo yao.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya, Wadau wa Sekta na Wataalam wengine tayari wamefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Bunge pamoja na Wadau, hata hivyo semina zimefanyika kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote na tulipokea maoni yao na kuyafanyia kazi wananchi kesho watege macho na masikio yao Bungeni kujua nini ambacho Waziri wa Afya Mheshiwa Ummy Mwalimu atawasilisha Bungeni” Amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya Bw. Englibert Kayombo

Amesema kuwa kupitishwa kwa muswada huu kutawezesha kila mtanzania kuwa ndani ya Mfumo wa Bima ya Afya hatua itakayoboresha zaidi upatikanaji wa huduma za matibabu bila kuwa na kiwazo cha fedha.

Serikali yetu ni sikivu sana na imefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Waheshimiwa Wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi hivyo yaliyomo ndani ya muswada huo yamelenga kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya bila ya kikwazo cha fedha” alisema Bw. Kayombo.

Kuhusu gharama za vifurushi, Kayombo amesema kuwa mara baada ya Muswada huo kupita na kuwa Sheria, kanuni zitatungwa ili kuratibu suala ya gharama za vifurushi na kusema kuwa uchambuzi utafanyika ili vifurushi viwe vya gharama nafuu na kila mwananchi aweze kuwa na bima ya afya.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Serikali imeshakamilisha maandalizi ya kutoa huduma kwa wananchi kupitia mfumo wa bima ya afya kwa wote ambapo imeboresha ubora wa huduma katika vituo vyake vya kutolea huduma ikiwemo upatikanaji wa Dawa, ununuzi na usimikaji wa vifaa na vifaa tiba, ajira za watumishi.

“Kwa sasa nchi yetu iko mbali sana katika utoaji wa huduma, tuna vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa, huduma nyingi za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini lakini pia huduma za afya zimesogezwa sana kwa wananchi hivyo kama nchi tupo tayari kutekeleza hili, nia na uwezo wa kufanya hivyo tunao” amesema Bw. Kayombo.


MRADI WA CSP MIRERANI WAJA NA MATOKEO CHANYA

October 31, 2023

 Na Mwandishi wetu, Mirerani



WANAWAKE wadau wa madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameona matokeo chanya kwenye shughuli zao kwani hivi sasa hawapekuliwi kwa kudhalilishwa na kuvuliwa nguo.


Wanawake hao walikuwa wanapekuliwa kwa kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo, ila baada ya kulalamikia hali hiyo kwenye mdahalo ulioandaliwa na shirika la Civic Social Protection Foundation (CSP) hivi sasa matokeo chanya yameonekana.


Mwanasheria wa CSP Eliakim Paulo akizungumza kwenye mdahalo wa ushiriki imara wa wanawake katika shughuli za madini kwenye eneo la machimbo ya madini Mirerani amesema hali imebadilika.


Paulo amesema hivi sasa wanawake wadau wa madini wanatumia fursa ya madini ya Tanzanite kufanya shughuli zao tofauti na awali walikuwa wanakutana na vikwazo vingi ikiwemo udhalilishwaji.


Amesema wanawake hao walikuwa wanapekuliwa kwa kuvuliwa nguo ila hivi sasa wakiwa kwenye chumba cha upekuzi wanapekuliwa kwa ustaarabu na siyo kudhalilishwa tena.


Amesema mradi huo umepata mafanikio kwani hata kituo cha polisi machimboni na kitengo cha dawati la jinsia linafanya kazi hivyo malalamiko ya wadau wanawake yamefanyiwa kazi.


“Hata barabara ya kwenda kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite, imechongwa na kampuni ya Franone Mining, hivyo magari na pikipiki wanatumia bila vikwazo tofauti na awali,” amesema Paulo.


Hata hivyo, amesema bei ya matumizi ya vyoo nayo imeshushwa kwani awali ilikuwa Sh1,000 na hivi sasa ni Sh500 ila bado mazungumzo yanaendela ili nauli za pikipiki za kubeba abiria (bodaboda) washushe nauli kutoka Sh2,000 hadi Sh1,000.


“Suala la mabasi madogo bado lipo kwenye mazungumza ili magari ya kubebea abiria ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite, yaruhusiwe kufanya kazi,” amesema Paulo.


Mmoja kati ya wanawake wadau wa madini ya Tanzanite, Fatuma Kifunta amesema upekuzi usiokuwa na stara ulikuwa unawakwaza kwani ulikuwa unakiuka haki za binadamu.


"Tunashukuru mno kwani mradi huu wa CSP umekuja na matokeo chanya kwani hivi sasa udhalilishwaji uliokuwa ukifanyika awali umekoma kwani hivi sasa watu wanapekuliwa kistaarabu," amesema.


Mdau mwingine Hawa Kiranga ametoa wito kwa serikali kuhakikisha vyombo vya moto vya usafiri ikiwemo mabasi madogo yanaruhusiwa ili kuwarahisishia usafiri wanawake wajasiriamali.


Kiranga amesema magari ya abiria yakiwa ndani ya ukuta wa madini itakuwa nafuu mno kwa wajasiriamali kwani nauli itakuwa Sh500 na kunufaisha watu wengi hasa wasio na kipato.


RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO RASMI NA RAIS WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI

October 31, 2023

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyeongoza ujumbe wa Tanzania Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.

RAIS DKT.MWINYI AVITAKA VIKOSI VYA SMZ KUENDELEZA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI

October 31, 2023

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amevinasihi vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza uadilifu na uwajibikaji wa majukumu yao ya kila siku.


Dk. Mwinyi ambae ni Kamanda Mkuu wa Idara Maalum ya vikosi vya SMZ, alitoa nasaha hizo viwanja vya JKU – Kama, alipozungmuza na wapiganaji kwa lengo la kuwapongeza kutokana na juhudi zao za kuhakikisha amani na utulivu nchini vinaendelea kuimarishwa.

Alivitaka vikosi hivyo kuweka mbele maslahi ya nchi kwanza, uwajibikaji pamoja na kusimamia uadilifu jeshini.

Rais Dk. Mwinyi alivisisitiza vikosi hivyo juu ya suala zima la kusimamia nidhamu kwenye maeneo yao ya kazi ili kufanya kazi zao kwa uadilifu.

“Jeshi ni nidhamu ikikosekana nidhamu katika jeshi basi hapo hakuna jeshi” alikazia Rais Dk. Mwinyi.

Dk. Mwinyi pia, alivipongeza vikosi hivyo kwa jitihada zao za kutoa huduma bora kwa jamii wakiwemo Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) kupitia hospitali yao iliopo Bububu pamoja na hospitali ya JKU, Saateni kwa huduma za afya wanazozitoa kwa wananchi na nyengine za jamii vikiwemo vyuo vya amali na taaluma.

Alivitaka vikosi hivyo kuwa mfano mzuri wa kutoa huduma bora kwa raia hasa kwenye vituo vyao vya afya na taaluma vinavyohudumia jamii.

Halikadhalika, Rais Dk. Mwinyi aliwaagiza wakuu wa vikosi hivyo kuendelea kusimamia uwajibikaji ili kuwe na tofauti baina ya hospitali za jeshi na za raia ili wananchi wapate huduma bora.

Pia, Dk. Mwinyi alivieleza vikosi hivyo kuwa vinajukumu la kutoa malezi bora kwa vijana na kuhakisha wanatoa vijana wazalendo wenye uchungu wa nchi yao watakaopigania maslahi ya taifa lao.

Akizungumzia suala la kuwajengea uwezo maofisa na wapiganaji wa vikosi hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliwataka wakuu wa vikosi hivyo kuwaongezea uwezo wa kitaaluma maofisa hao kwa kuwapatia fursa za mafuzo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Idara Maalum ya vikosi vya SMZ, Masoud Ali Muhammed alisema, Idara Maalum ya vikosi vya SMZ zote tano zikotayari kuendeleza jukumu mama la kuimarisha na kuendeleza amani, utulivu na mshikamano uliopo nchini vinaendelea kusimama wakati taifa likiendeleza maendeleo ya watu wake.

Alisema, Idara hizo pia zitaendelea kutekeleza maagizo, maono, mipango na fikra za Kamanda Mkuu kwa utii wa hali ya juu.

Akiwasilisha risala ya vikosi vitano vya Idara Maalum ya SMZ, Katibu Mkuu wa Idara hiyo, Issa Mahafoudh Haji alisifu juhudi kubwa ya Kamanda Mkuu wa Idara Maalum ya vikosi vya SMZ, Rais Dk. Mwinyi aliyoifanya kwa vikosi hivyo.

Alimshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa kuvishirikisha vikosi hivyo kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo nchini na kueleza kuwa imewaongezea uwezo na nguvu za kiuchumi kwa kutatua baadhi ya changamoto zao.

Pia, alieleza ushiriki wao kwenye miradi hiyo, umetanua uwezo wao wa ufahamu na ujuzi wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku pamoja na kusifu hatua ya kuwapandishia mishahara makamanda na wapiganaji kufuatia nyongeza ya mishahara aliyoitoa kwa watumishi wa umma wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vinaundwa na Jeshi la kujenga Uchumi (JKU), (KMKM), Vikosi vya Uokozi na Zimamoto, Valantia (KVZ) na Chuo cha Mafunzo.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Kamanda Mkuu Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi alipowasili viwanja vya Kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi Kama, Wilaya ya Magharibi "A" kwa ajili mya kuzungumza na Maafisa na Askari wa Vikosi vya SMZ leo katika shamra shamra za Miaka Mitatu ya Uongozi wake .[Picha na Ikulu] 30/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Kamanda Mkuu Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohamed (wa pili kulia) pamoja na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi wakisaluti wakati Wimbo wa Taifa Ukupigwa leo katika hafla ya Mazungumzo na Maafisa na Askari wa Vikosi vya SMZ katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi Kama, Wilaya ya Magharibi "A" katika shamra shamra za Miaka Mitatu ya Uongozi wake .[Picha na Ikulu] 30/10/2023.

Baadhi ya Maafisa na Askari wa Vikosi vya SMZ wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Kamanda Mkuu Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza nao leo katika viwanja vya Kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi Kama, Wilaya ya Magharibi "A" leo katika shamra shamra za Miaka Mitatu ya Uongozi wake.[Picha na Ikulu] 30/10/2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohamed alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Kamanda Mkuu Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) kuzungumza na Maafisa na Askari wa Vikosi vya SMZ katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi Kama, Wilaya ya Magharibi "A" katika shamra shamra za Miaka Mitatu ya Uongozi wake .[Picha na Ikulu] 30/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Kamanda Mkuu Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na Maafisa na Askari wa Vikosi vya SMZ katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi Kama, Wilaya ya Magharibi "A" leo katika shamra shamra za Miaka Mitatu ya Uongozi wake .[Picha na Ikulu] 30/10/2023.

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA UJERUMANI MHE. FRANK-WALTER STEINMEIER, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

October 31, 2023

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023. Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.

WANNE WAFANYIWA UPASUAJI WA KUPUNGUZA UZITO ULIOKITHIRI MNH-MLOGANZILA

October 31, 2023

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


HOSPITALI ya Taifa Muhimbili Mloganzila imefanikiwa kufanya upasuaji wa kibingwa bobezi wa kupunguza uzito kwa wagonjwa wanne wenye uzito uliokithiri ambapo zoezi hilo ni mara ya kwanza nchini katika Hospitali za Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema utaratibu huo wa matibabu umefanyika kwa njia ya utaalamu wa hali ya juu bila upasuaji ambapo wagonjwa watatu wamefanyiwa kwa njia ya matundu madogo (Laparoscopic Sleeve Gastrectomy) na mmoja amefanyiwa kwa kutumia njia ya Endoskopia (Endoscopic Sleeve Gastroplasty).

Amesema kwa kutumia endoskopia mtu atapoteza uzito kwa asilimia 15-23, na kwa kutumia matundu madogo (Laparoscopic Sleeve Gastrectomy) atapoteza uzito kwa asilimia 50-70 ndani ya miezi kumi na mbili.

“Utaratibu huu wa matibabu kwa watu wenye uzito uliopitiliza umefanywa na Madaktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga&Mloganzila) kwa kushirikiana na mtaalamu bobezi wa upasuaji kutoka nchini India Dkt. Mohit Bhandari pamoja na Taasisi ya Medincredi”. Amesema

Aidha amesema kuwa kila mmoja amefanyiwa huduma hii kwa muda wa takribani dakika 15 mpaka 30 ambapo watatu waliruhusiwa baada ya masaa 24 baada ya kupatiwa huduma na mwingine aliruhusiwa saa nane baada ya huduma.

“Kwa upande waliofanyiwa huduma hii wa juu kabisa alikuwa na uzito Kilogramu 142 na wa chini alikuwa na uzito wa Kilogram 107, ambapo tunategemea baada ya kupata huduma hii watapungua uzito wao kwa kiasi kikubwa”. Ameeleza Prof.Janabi

Prof.Janabi amesema lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinakuwa endelevu ambapo mpango wa hospitali ni kuwezesha huduma hizo kufanyika kila mwezi na kwa siku za usoni zitakuwa zinafanywa na wataalamu wa ndani.

Ameeleza kuwa wanatoa pia huduma mbalimbali za Kibingwa Bobezi ikiwemo kupandikiza figo, kupunguza uzito kwa kutumia puto maalum (intra gastric balloon), kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kwa matundu ya pua, kuvunja mawe kwenye figo kwa kutumia mawimbi mtetemo, kupandikiza nyonga bandia na upasuaji wa kutumia matundu madogo.

Prof.Janabi amempongeza Rais Dkt, Samia Suluhu kwa kuwekeza katika sekta ya afya ambapo amenunua vifaa tiba kuanzia ngazi ya Zahanati hadi kwenye hospitali bobezi ya Taifa na kuweza kumpunguzia gharama mgonjwa kutafuta tiba nje ya mipaka ya nchi.

"Wote mnaelewa changamoto ya fedha za kigeni, hawa tusingewafanyia upasuaji hapa wangetafuta njia moja au nyingine kwenda nje maana yake wangetumia fedha za kigeni"Amesema
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.




Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Madaktari wabobezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi  wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31,2023 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
ZIC,WADAU WAENDESHA MAFUNZO KUHUSU BIMA YA KIISLAM KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

ZIC,WADAU WAENDESHA MAFUNZO KUHUSU BIMA YA KIISLAM KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

October 31, 2023


Facebook




Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo pamoja na wageni waalikwa wakati akizunduza semina ya siku moja kwawawakilishi hao iliyoendeshwa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo ikilenga  kuwajenga uelewa wajumbe hao kuelekea uanzishwaji wa huduma  mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’. Wanaomsikiliza ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango –Zanzibar  Mhe. Dkt Saada Mkuya (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar(ZIC) Bw Arafat Haji (Kushoto) na wadau wengine.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango –Zanzibar  Mhe. Dkt Saada Mkuya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  pamoja na wageni waalikwa wakati wa semina ya siku moja kwa wawakilishi hao iliyoendeshwa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo ikilenga  kuwajenga uelewa wajumbe hao kuelekea uanzishwaji wa huduma  mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar(ZIC) Bw Arafat Haji akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wageni waalikwa wakati wa semina ya siku moja kwa wawakilishi hao iliyoendeshwa na shirika hilo kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo ikilenga  kuwajenga uelewa wajumbe hao kuelekea uanzishwaji wa huduma  mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

 

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau wa Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

……………………………………

Na Mwandishi wetu-Zanzibar

Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kushirikiana na wadau wengine visiwani humo limeendesha mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar ikiwa ni moja ya hatua muhimu kuelekea utoaji wa huduma yake mpya ya Bima ya Kiislamu ‘Takaful’.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika eneo Chukwani nje kidogo ya jiji la zanzibar, yalitanguliwa na mafunzo ya siku moja kwa mawakala wa bima visiwani humo yaliyofanyika visiwani Pemba huku lengo likiwa ni kuwaandaa wadau muhimu kuelekea kuanza matumizi ya bima ya kiislaam nchini.

Akizindua mafunzo hayo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid alisema  kuna umuhimu mkubwa wa kuleta mabadiliko katika kukuza huduma za bima ya kiislamu nchini huku akibainisha kuwa tayari nchi nyingi duniani zimeshafanya mabadiliko ya sheria za kifedha na kodi hivyo hatua hiyo itaweza  kuweka mazingira bora ya kukuza na kustawisha huduma hizo.

“Ni imani yangu kuwa mfumo huu utaenda kuleta mabadiliko makubwa katika sekta za kibima hivyo ni wajibu wa serikali kuweka mikakati imara ili kuhakikisha  wanachi walio wengi wananufaika” alisema, 

Zaidi Mh Zubeir  aliwahamasisha wajumbe wa baraza hilo kuhakikisha wanayatumia vema mafunzo hayo ili kujijengea uelewa wakutosha ili pia na wao waweze kupeleka uelewa huo kwa wananchi.

“Naamini pia kupitia uelewa huo mtaweza kuuliza maswali ya kina pamoja na kutoa maoni yenu muhimu kuhusu huduma hii ili wataalamu waweze kuyazingatia na kuyatekeleza kwa maslahi ya wananchi wetu hapa Zanzibar na taifa kwa ujumla,’’ alisisitiza.

Aidha Mh Zubeir alitoa wito kwa Mamlaka mbalimbali zinazohusika katika kufanikisha mpango huo zikiwemo taasisi za kifedha na mamlaka husika kuhakikisha zinafanya juhudi za makusudi ili kuruhusu utoaji wa huduma hiyo haraka iwezekanavyo lakini pia kwa ufanisi unaotakiwa ili iwe na tija zaidi hususani kwa wananchi wa kipato cha chini.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar(ZIC) Bw Arafat Haji alisema kupitia mkakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo Shirika hilo linaamini kuwa taarifa muhimu kuhusu huduma hiyo mpya zitawafikia walengwa wote kote nchini ili waweze kuichangamkia pindi itakapowafikia.

“Ni matumaini yetu kuwa ujio wa huduma hii ya Bima ya Kiislamu yaani ‘Takaful’ itakuwa ni suluhisho sahihi la kuwavutia wananchi wengi zaidi visiwani Zanzibar na maeneo mengine ya nchi ambao kimsingi wanahitaji huduma ya Bima ila wanashindwa kutokana na imani za kidini.’’ Alisema

Alibainisha kuwa wananchi wengi wa visiwa vya zanzibar wamekua wakisuasua kuingia katika mifumo ya bima kwa kujiepusha na riba ambazo zimekuwa zikienda kinyume na silaka na dini zao.

Akitoa shukrani zake kwa niaba ya serikali na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango –Zanzibar  Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum pamoja na kuwapongeza wadau hao wakiwemo ZIC alisema semina hiyo imeendeshwa kwa kundi muhimu  kwa kuwa wajumbe hao wanawakilisha maelfu wa wananchi hatua itakayorahisisha usambazaji wa elimu hiyo.

 “Baada ya mafunzo haya sisi kama viongozi wa serikali pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi tunabaki na jukumu kubwa la kuhakikisha elimu hii haibaki miongoni mwetu bali inawafikia wananchi tunaowawakilisha huko majimboni na hicho ndio kitu kinachofuata baada ya hapa. Huduma hii ni muhimu sana kwa wananchi wetu na tutahakikisha inawafikia kama ilivyokusudiwa,’’alisisitiza.

Mbali na ZIC wadau wengine waliohusika katika utoaji wa mafunzo hayo kuhusu Bima hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ni pamoja na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),  Kituo cha Usimamizi wa Masuala ya Huduma za Kifedha za Kiislamu na Ushauri Tanzania (CIFCA) na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu(IsDB). 

ZIFF, EU WALETA FILAMU MIKOA MITATU YA TANZANIA BARA

October 31, 2023

 Na Andrew Chale, Dar es Salaam.


TAMASHA la Kimataifa la filamu za Nchi za Majahazi (Zanzibar International Film Festival-ZIFF) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), Nchini wametangaza rasmi uoneshaji wa filamu katika Vyuo Vikuu kwenye mikoa mitatu ya Tanzania Bara linalokwenda kwa jina la “ZIFF Goes Mainland 2023”.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF aliyemaliza muda wake ambaye anaratibu mpango huo, wa "ZIFF Goes Mainland 2023" amesema mpango huo umeendelea kuimarika na kuanzia Novemba 3, 2023, filamu tano zilizoshinda tuzo kutoka msimu wa 26 wa ZIFF na filamu teule za Ulaya zitaonyeshwa.

‘’Filamu hizi zitaoneshwa katika Mikoa ya Dar es Salaam ikiwemo Chuo cha Kampala KIU, Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika Chuo cha TaSUBa, na Morogoro katika chuo kikuu Mzumbe. Wanafunzi watashiriki katika majadiliano baada ya kutazama kuhusu filamu na mbinu zao za kutengeneza filamu.

Tamasha hilo litafungua filamu ya "EONII" ya mwongozaji Mtanzania, na pia kutakuwa na filamu kutoka nchi za Ulaya kuangazia utofauti wa kitamaduni tajiri.’’ Amesema Prof. Martin Mhando.

Aidha, Mwaka huu, ili kuonyesha mshikamano kati ya vita vinavyoendelea na Urusi, filamu kutoka Ukraine, Pia filamu kutoka Afrika Kusini, Kenya, Misri na Tanzania.

‘’#TeamEurope - EU, taasisi zake na nchi wanachama - imekuwa muhimu katika kuimarisha tamasha la ZIFF.
Ushirikiano wetu na shughuli za zamani ikiwa ni pamoja na kusaidia warsha za mafunzo, kufadhili programu za ZIFF, ili kuwasilisha fursa za utayarishaji wa pamoja”. Amesema Prof. Martin Mhando

Kwa upande wake, Mkuu wa Ujumbe wa EU nchini Tanzania, Mhe. Balozi Bi. Christine Grau amesema; "Ulaya imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa tamasha zaidi ya kuonyesha filamu binafsi. Kusaidia wadau wanaohusika na utamaduni, na kuanzisha miundomsingi inayosaidia wasanii kujitahidi na kuhamasisha jamii zao.

Katika mkutano huo, wawakilishi kutoka Balozi tisa zikiwemo nchi za Spain, Belgium, Germany, Ireland, France, Poland, Finland, Italy na Sweden zinazochangia mpango huo wa ZIFF kwenda Bara 2023’’, wameweza zilizohudhuria, wakisisitiza ari ya #TeamEurope na jukumu la Diplomasia ya kitamaduni katika kukuza amani katika Ulaya na Afrika.

Baadhi ya filamu hizo tano ni pamoja na N8, MWANDISHI,NEB TAWY, 9MEMEZA na EONII