RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SOKO LA CRDB KIZIMKAZI DIMBANI,KUSINI UNGUJA ZANZIBAR

August 29, 2023

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati) akipata maeleo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa kuhusu ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
 
======   ======   =======

 Kizimkazi, Zanzibar, 29 Agosti 2023: Katika juhudi za kuendelea kuwezesha jamii inayoizunguka kupitia sera yake ya uwekezaji kwa jamii, Benki ya CRDB kupitia Tasisi yake ya CRDB Bank Foundation inatarajia kujenga soko la kisasa katika Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar. Hafla ya kuweka jiwe la msingi la soko hilo imefanyika katika eneo la Kizimkazi Dimbani kama sehemu ya shamra shamra za tamasha la Kizimkazi na kuhududhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo, Rais Dkt. Samia ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukubali ombi la Mkoa wa Kusini kujenga soko hilo la kisasa ambalo litachochea maendeleo ya watu wa Kizimkazi na Mkoa wa Kusini Unguja kwa ujumla.
“Mwaka jana kama mnakumbuka mlinipa kilio hiki cha soko la jamii ya Kizimkazi. Sasa mimi nikalitupa Mkoa ambapo na wao wakalipeleka CRDB na leo wako hapa kwenye field tayari kuweka jiwe la msingi na ujenzi unaendelea. Kwa hiyo tuwashukuru sana CRDB kwa kutushika mkono katika hilo na haya ndo maendeleo ya Kusini tuliyoyasema na ndo madhumuni ya tamasha letu hili la Kizimkazi” alisema Rais Dkt. Samia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kwa kutambua uchumi wa watu wa kusini unatemegea sana uvuvi, Benki chini ya Taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeamua kuwekeza katika ujenzi wa soko la kisasa ambalo litakwenda kuongeza thamani katika biashara kwa wakazi wa eneo la Kizimkazi. Katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko, Benki imetenga takribani Shilingi Milioni 157.8 na tayari ujenzi wa sehemu ya kwanza tayari umeanza.

“Kwa muda mrefu Benki ya CRDB imekua mdau mkubwa wa maendeleo ya Kizimkazi kupitia tamasha la Kizimkazi ambapo hadi kufikia tamasha la mwaka huu, Benki ya CRDB imeshafanya uwekezaji wa takribani Shilingi Bilioni 1 na soko hili la kisasa la Samaki litaghrarimu zaidi ya Bilioni 2 hadi kukamilika kwake ambapo sehemu ya kwanza ya ujenzi itakamilika mnamo mwezi Oktoba 2023” amesema Nsekela.
Mbali na utoaji wa huduma za fedha kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano, Benk ya CRDB pia imekua ikitekeleza sera yake ya uwekezaji katika jamii katika pande zote mbili. Sera hiyo ya uwekezaji katika jamii inaelekeza 1% ya faida kurejeshwa katika jamii katika maeneo ya elimu, afya, mazingira na uwezeshaji kwa wanawake na vijana.

“Mbali na ujenzi wa soko hili la kisasa, Benki kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeendelea na dhamira yake ya kuleta mageuzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo katika tamasha la Kizimkazi la mwaka 2023, Benki imewekeza zaidi ya Milioni 119.5 katika mashindano ya Resi za Ngalawa ambazo ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi” aliongeza Nsekela.
Mwaka 2021, Benki ya CRDB ilikua mdhamini kuu wa Tamasha la Kizimkazi kwa kugharamia tamasha lote asilimia kuanzia mafunzo kwa wajasiriamali, michezo, maonyesho ya wafanyabiashara hadi kilele cha tamasha. Mbali na hilo Benki ilifadhili ujenzi wa nyumba za madaktari na Ofisi ya Sheha.

Mwaka 2022, Benki ya CRDB ilijenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kizimkazi pamoja na kununua vifaa vyake vya maabara. Sambamba na hilo Benki ilifadhili michezo yote na zaidi kuleta mapinduzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo uliweza kuvutia watu wengi zaidi na kutoa zawadi kubwa zilizoweza kubadili maisha ya wana Kizimkazi ikiwemo zawadi kubwa ya boti ya kisasa yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 kwa mshindi.





MBUNGE MAIMUNA PATHANI UTAJIRI WA LINDI UPO KWENYE MADINI

August 29, 2023

 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan akiongea wakati wa kongamano la madini lililofanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi huku akielezea fursa mbalimbali zinazotokana na upatikanaji wa madini katika mkoa huo.


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Maimuna Pathan amesema Lindi utakuwa mkoa tajili Tanzania kutokana na uwepo wa madini ya Kila aina katika ardhi ya mkoa huo.


Akizungumza wakati wa kongamano la madini lililofanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi,Mbunge Maimuna Pathan alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Lindi wanatakiwa kuzitumia vilivyo fursa za uwepo wa madini katika ardhi ya mkoa huo ambao utakuza uchumi wa taifa zima.


Pathan alisema kuwa baada ya miaka mitano kila mtu anatakuwa anazungumzia utajiri wa madini uliopo katika katika mkoa wa Lindi tofauti na ilivyokuwa awali.


Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa zote zilizopo kwenye sekta ya madini ili kukuza uchumi wao na kupata maendeleo kutokana uwepo wa madini mbalimbali.


Pathan alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na utunzaji wa mazingira kwenye maeneo ambayo madini yanachimbwa 

PROF. MBARAWA: WAKANDARASI ONGEZENI WATAALAM NA MITAMBO KAZI ZIENDE HARAKA

August 29, 2023



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akipata ufafanuzi toka kwa mhandisi mkazi anayesimamia ujenzi wa barabara ya Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo inayounganisha wilaya za Handeni, Bagamoyo na Pangani mkoani Tanga.

Muonekano wa moja ya daraja katika barabara ya Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa mkandarasi M/s Shandong Luqiao Group Ltd anayejenga daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 na barabara za maingilio takriban KM 25 mjini Pangani

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Pangani ambaye pia ni waziri wa maji mhe. Jumaa Aweso alipokagua ujenzi wa daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525.


Muonekano wa baranbara ya Tanga–Pangani KM 50 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.



Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewataka wakandarasi wanaojenga barabara za Tanga-Pangani KM 50, Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 na daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 mkoani Tanga kuongeza wataalam na mitambo ili kuharakisha kazi za ujenzi huo.


Prof. Mbarawa amesema Serikali haitasita kuchukua hatua za kimkataba kwa mkandarasi yeyote anayeshindwa kuajiri wataalam sahihi na wakutosha na hivyo kusababisha miradi kuchelewa kumalizika na kuwanyima wananchi fursa ya kunufaika na miradi hiyo mapema.

“Tunaleta fedha na tutaendelea kuleta kwa awamu hivyo hakikisheni wataalam stahiki wapo site na mitambo ifike kwa wakati ili kulinda dhana ya value for money”, amesema Prof. Mbarawa.

Amewataka wakandarasi M/s China Henan International Cooperation Group Co. Ltd anayejenga barabara ya Tanga-Pangani, KM 50, China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara ya Tungumaa-Mkwaja-Mkange KM 95.4 na M/s Shandong Luqiao Group Ltd anayejenga daraja la Pangani mita 525 na barabara za maingilio takriban KM 25 mjini Pangani kufanya kazi kwa bidii na viwango vya juu ili kukidhi matarajio ya watanzania.

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua ushoroba wa mwambao wa bahari ya hindi na kukuza uchumi wa wakazi wa mikoa ya Tanga,Pwani na Dar es salaam.

Kwa upande wake Mbunge wa Pangani ambae pia ni Waziri wa maji Mhe. Jumaa Aweso ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa inaoufanya mkoani Tanga na kuwataka wananchi wa maeneo inapopita miradi ya ujenzi kuchangamkia fursa za ajira, ujuzi na biashara.

Naye meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Eng. Eliazary Rweikiza amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa wataalam wamejipanga vizuri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa ubora na kuleta tija kwa taifa.

Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya siku mbili mkoani Tanga kukagua miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja ikiwa ni mkakati wa kuwakumbusha wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wakati huu ili kuepuka visingizio vya kuchelewesha miradi pindi mvua za vuli zitakapoanza kunyesha baadae mwezi Oktoba.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI

BENKI YA CRDB YASHIRIKI UFUNGUZI WA TAMASHA LA KIZIMKAZI, ZANZIBAR

August 27, 2023

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Paje, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji CRDB Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, wakati alipotembelea banda letu kwenye ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na wananchi waliofurika kwa wingi katika viwanja vya Paje, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi akiwa pamoja na viongozi wengine wakipiga makofi na kufurahia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kizimkazi, linalofanyika Paje mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar jana.
 Sehemu ya burudani kutoka kwa watoto wa Shule ya Assalam ya Kizimkazi.





 

Mchengerwa awakaribisha wawekezaji Rufiji Benki ya CRDB ikizindua tawi lake Ikwiriri

August 27, 2023

 

 
Rufiji. Tarehe 25 Agosti 2023: Baada ya Benki ya CRDB kufungua tawi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa amewakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza kwenye fursa tele zilizopo wilayani Rufiji.

Mchengerwa amesema Rufiji ambayo ni kati ya wilaya kongwe nchini inazidi kukua kila siku kwa kuimarisha miundombinu ya huduma za jamii kwani tayari serikali imejenga zahanati 24, shule za msingi 45 na sekondari 9 ndani ya vijiji 38 ilivyonavyo zinazotoa nafasi kwa wananchi kutibiwa na watoto kupata elimu itakayowasaidia kujikomboa katika maisha yao hivyo ujio wa Benki ya CRDB inawaongezea fursa za kujiimarisha kiuchumi.
“Uamuzi wa serikali kujenga Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) umeleta neema nyingi zitakazowanufaisha wananchi na halmashauri hii yenye utajiri mkubwa wa ardhi, maliasili na utamaduni. Ukiacha bwawa hili, kuna hekta 300,000 limetengwa kwa ajili ya kilimo kitakachoendeshwa kwa mfumo wa umwagiliaji.  Ni wakati sahihi sasa kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza wilayani Rufiji kwani kuna usalama wa kutosha kuanzia namna ya kuhifadhi fedha zao mpaka kutekeleza miradi watakayoianzisha,” amesema Mchengerwa.

Ili kutoachwa nyuma, Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji tangu mwaka 2015 amewahimiza wananchi wenzake kulitumia tawi hilo la Benki ya CRDB hivyo kunufaika na huduma zinazotolewa na kujihakikishia usalama wa fedha, kukopa kwa ajili ya miradi na mipango binafsi hata kufanya uwekezaji.
“Rufiji ni kati ya wilaya kongwe nchini lakini kwa muda mrefu haikuwa imefunguka ila leo hii Benki ya CRDB imeonyesha njia. Ili kuwa wilaya ya sita wakati wa mkoloni na ya 13 baada ya uhuru. Mimi ni mteja wa siku nyingi wa Benki ya CRDB hivyo nawasihi wananchi wenzangu nanyi mjiunge kutumia huduma za benki hii. 

Benki hii ya CRDB inayo huduma ya imbeju ambayo ni programu maalumu ya kuwawezesha vijana na wanawake. Makundi haya muhimu kwa jamii yetu yapo wilayani Rufiji na kwa kufika kwenye tawi hili ndivyo yataweza kunufaika na programu hii inayotoa mtaji wezeshi kwao. Kwa kuwa Rufiji ina kila kitu kinachohitajika kwa mjasiriamali kujikwamua kiuchumi, mtaji huu unaotolewa na Benki ya CRDB na mikopo ya aina tofauti iliyopo ni msingi mkubwa wa kuwakomboa wananchi kiuchumi,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amezitaja fursa nyingine zilizopo wilayani humo kuwa ni pamoja na kilomita za mraba 6,500 ambazo ni hifadhi na misitu zinazofaa kwa utalii. Nyingine amesema ni uvuvi, huduma za kijamii na ukarimu zikiwamo hoteli. Kwenye kilimo, amesema ufuta, korosho na mazao mengine mengi ya biashara yanastawi vyema wilayani humo na hivi karibuni kiwanda kikubwa cha sukari kitajengwa wilayani humu.
Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema wamejipanga vyema kukidhi mahitaji ya mtaji kwa ajili ya wateja wao wakiwamo wawekezaji wanaohitaji shilingi hata fedha za kigeni.
 
“Jana benki yetu imepata kibali za kuorodhesha hatifungani ya kijani yenye thamani ya dola milioni 300 za Marekani ambazo ni sawa na shilingi bilioni 780. Fedha zitakazokusanywa kutokana na mauzo ya hatifungani hii zitaelekezwa kwenye miradi inayolinda na kujali mazingira. Rufiji ni kati ya maeneo yanayostahili kuzitumia hivyo nawakaribisha mje tuwahudumie,” amesema Raballa.
Afisa huyo amesema kupitia tawi hilo, wananchi wa wilaya nzima ya Rufiji wanafunguliwa milango kunufaika na mtandao mpana wa matawi 260 yanayoifanya Benki ya CRDB kuwa na idadi kubwa zaidi ikilinganishwa na benki nyingine nchini.

Licha ya huduma matawini, kupitia mawakala wa benki, mashine za kutolea fedha na zile zinazopokea malipo ya kadi au kupitia simu ya mkononi, amesema Benki ya CRDB inatoa ushauri na elimu kuhusu masuala ya fedha, uwekezaji na namna bora ya uendeshaji wa biashara.
“Watu wengi hudhani benki ni kuweka, kutoa pesa au kuomba mkopo tu lakini ukweli wasioujua ni kuwa tunatoa elimu na ushauri na tumekuwa tukifanya hivyo kwa wateja wetu ingawa wengi hawaitumii huduma hii. Hivyo niwakaribishe katika Benki yenu ya CRDB kupata ushauri. 

Na kupitia taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation, tunafanya uwezeshaji kwa wanawake na vijana kwa kuwapa mitaji wezeshi kwa masharti nafuu ili kuwapa nafasi ya kuimarisha kipato chao na kushiriki kujenga uchumi wa taifa,” amesema Raballa.

Benki ya CRDB ndio taasisi pekee ya kizalendo yenye matawi nje ya mipaka ya Tanzania ikitoa huduma nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

CMSA yaidhinisha Benki ya CRDB kutoa hatifungani ya kijani

August 26, 2023
Dar es Salaam, 24 Agosti 2023: Katika juhudi za kuongeza uwezo wake wa kufanya uwezeshaji wa miradi rafiki kwa mazingira, Benki ya CRDB imepata idhini kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuuza Hatifungani ya Kijani (Green Bond) yenye thamani ya dola 300 milioni za Marekani (takriban Shilingi bilioni 780). Benki ya CRDB inaweka historia ya kuwa taasisi ya kwanza kutoa hatifungani ya kijani hapa nchini inayoweka mkazo katika masuala ya mazingira na kubwa zaidi kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza wakati wa kupokea idhini ya kuuzwa kwa hatifungani hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema ni furaha kubwa kupata idhini kutoka CMSA kuiuza hatifungani hiyo ambayo lengo lake si tu kupata rasilimali fedha bali kufanikisha utekelezaji wa miradi yenye mrengo wa kuhifadhi mazingira hivyo kushiriki ipasavyo katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
“Pamoja na kuwa Benki ya CRDB inaweka rekodi ya kuwa taasisi kubwa zaidi ya fedha nchini kupata idhini ya kuuza hatifungani ya kijani, lakini Benki yetu sio ngeni katika uwezeshaji wa miradi yenye mrengo wa utunzaji mazingira kwani Novemba 2019 ilitambuliwa na kuingia makubaliano na Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (GCF) kufanikisha miradi ya kulinda mazingira. Hii pia ilikuwa ni mara ya kwanza benki ya biashara kusini mwa Jangwa la Sahara kutunukiwa sifa hiyo na tangu hapo, tumeshiriki kwa kiasi kikubwa kuwezesha miradi inayokusudia kulinda mazingira,” amesema Nsekela.

Kuhusu uwezeshaji wa miradi ya mazingira, Nsekela amesema kwa mwaka jana pekee, Benki ya CRDB ilikopesha jumla ya shilingi trilioni 6.978 ambazo ni sawa na asilimia 26 ya mikopo yote iliyotolewa na taasisi za fedha nchini. Katika fedha hizo, amesema shilingi bilioni 1.44 zilikopeshwa katika sekta ya misitu, kiasi hicho ni sawa na asilimia 55 ya mikopo yote iliyotolewa kwenye sekta ya misitu.  
Kwenye kilimo, sekta muhimu kwenye uhifadhi wa mazingira na inayotoa ajira nyingi zaidi nchini na kulipa Taifa fedha nyingi za kigeni, amesema benki hiyo ilikopesha takriban shilingi trilioni moja ambazo ni sawa na asilimia 43 ya mikopo yote iliyotolewa kwenye eneo hilo na ikapeleka shilingi bilioni 55.88 kwenye sekta ya nishati mbadala.

Licha ya jitihada hizo, mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa bado kuna mahitaji makubwa ya fedha kuliko uwezo walionao hivyo kutafuta namna rafiki ya kufanikisha suala hilo.

“Kwa kutambua mahitaji yaliyopo, Benki ya CRDB imeona ni muhimu kutafuta vyanzo vipya vya fedha kuwezesha miradi hii. Leo nina furaha kuona jitihada zetu zimezaa matunda kwa CMSA kutupa idhini ya kuuza hatifungani yetu ya kijani (green bond) ambayo itauzwa kwa awamu tano ambapo katika awamu hii ya kwanza tunatarajia kupata shilingi bilioni 55,” amesema Nsekela.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama ameipongeza Benki ya CRDB kwa kufanikiwa kuwa Benki ya kwanza nchini kupata idhini ya kutoa hatifungani itakayowezesha kupata fedha za kutekeleza miradi ya kuhifadhi mazingira na matokeo chanya kwa jamii yaani green, social and sustainability bond. 

Idhini imetolewa na CMSA baada ya Benki ya CRDB kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania; Miongozo ya Utoaji wa Hatifungani yaani “Capital Markets and Securities (Guidelines for issuance of Corporate Bonds”; uwepo wa Muundo wa Hatifungani yaani Green, Social and Sustainability Bond Framework; Kanuni za Jumuiya ya Kimataifa ya Masoko ya Mitaji yaani International Capital Markets Association (ICMA); na kupata ithibati kutoka kwa taasisi zenye utaalam kuhusu miradi ya kuhifadhi mazingira na matokeo chanya kwa jamii. 

Amesema Benki ya CRDB imekidhi matakwa haya na kupata ithibati kutoka Taasisi ya Uendelezaji wa Sekta za Fedha Barani Afrika, FSD Africa na Taasisi ya Sustainalytics ya Uingereza. Hatifungani hii inaweka historia ya kuwa hatifungani ya kwanza yenye lrngo la kuhifadhi mazingira na matokeo chanya kwa Jamii kutolewa nchini Tanzania na katika Ukanda kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mkama amefafanua kuwa, utoaji wa hatifungani hii ni hatua muhimu katika ustawi na maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi hapa nchini, kwani utachangia katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha yaani National Financial Sector Development Master Plan 2020/21 – 2029/30 wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya miradi katika sekta ya umma na binasi ili kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu.

Mkama amesema kuwa CMSA imeidhinisha utoaji wa hatifungani hii itakayotoa mikopo kwa shilingi na fedha za kigeni (multicurrencies) kutokana na mazingira wezeshi na shirikishi ya kisera, kisheria na kiutendaji ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi madhubuti wa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mkama amehitimisha kwa kutoa rai kwa wadau wote wa sekta ya fedha kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) katika kutekeleza mikakati ya upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi na shughuli za maendeleo kwa kutoa bidhaa mpya na bunifu zenye lengo la kuhifadhi mazingira, na zenye mguso na matokeo chanya kwa jamii hivyo kuchangia katika kuchochea maendeleo ya jamii na ukuaji wa uchumi nchini. 
Akiishukuru CMSA na wadau wengine walioshiriki mchakato mzima mpaka kupatikana kwa kibali hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt Ally Laay amesema wawekezaji wa ndani na watokao nje wanayo fursa ya kunufaika na hatifungani hii kwani mikopo itapatikana kwa shilingi au dola ya Marekani. 

“Mara nyingi, Benki ya CRDB imekuwa ya kwanza. Leo hii ni fursa nyingine kwa benki hii kuorodhesha hatifungani kubwa zaidi, sio nchini pekee bali kwa nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara. Nawashukuru CMSA na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na wadau wengine waliotusaidia kufanikisha hili. Nawaomba Watanzania wenzangu kujitokeza kununua hatifungani hii pindi itakapoanza kuuzwa muda si mrefu kutoka leo. Tusiiache fursa hii itupite,” amesema Dkt Laay.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama akikabidhi kibali cha kutoa hatifungani ya kijani "green bond" yenye ya thamani ya dola milioni 300 za Marekani sawa na Shilingi bilioni 780 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam. Hatifungani hiyo ni ya kwanza kutolewa Tanzania na ya kwanza kwa ukubwa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Picha zote na Othman Michuzi.
Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru akizungumza katika hafla kukabidhi kibali cha kutoa hatifungani ya kijani "green bond" yenye ya thamani ya dola milioni 300 za Marekani sawa na Shilingi bilioni 780 kwa Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza katika hafla kukabidhi kibali cha kutoa hatifungani ya kijani "green bond" yenye ya thamani ya dola milioni 300 za Marekani sawa na Shilingi bilioni 780 kwa Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam leo.




NSSF YATOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA MANUNUZI YA UMMA

August 24, 2023


Meneja wa Sekta isiyo rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Rehema Chuma (kushoto) akimsikiliza Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga, Theresia Makyao mara baada ya kutembelea banda na NSSF wakati wa kongamano la Wanawake na Manunuzi ya Umma, linalofanyika jijini Tanga
Meneja wa Sekta isiyo rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Rehema Chuma (kushoto) akifuatilia jambo wakati wa Kongamano la Wanawake na Manunuzi ya Umma Jijini Tanga



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeshiriki na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa washiriki wa kongamano la Wanawake na Manunuzi ya Umma, linaloendelea jijini Tanga. 

Akizungumza wakati wa kongamano hilo Meneja wa Sekta isiyo rasmi, Rehema Chuma ambaye  alikuwa miongoni mwa waliotoa mada katika kongamano hilo lililoanza tarehe 23 Agosti, 2023, amesema kupitia kongamano hilo NSSF imetoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ambayo imebeba kundi kubwa.

Kundi hilo kubwa ambalo sekta isiyorasmi ni  kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, bodaboda na wajasiriamali wengine wote ili waweze kujiunga na kuchangia katika Mfuko kwa maisha yao ya sasa na baadaye.

Lengo la kongamano hilo ni kueleza fursa za biashara zinazoambatana na mradi wa bomba la mafuta Afrika Mashariki (EACOP) hivyo mradi huo ni fursa kwa NSSF kupata wanachama wapya ambao watapata ajira za moja kwa moja na wale watakaonufaika na ajira za muda pamoja na wanufaika wengine kama vile mama lishe na bodaboda ambao wataweza kujiunga na kuchangia katika Mfuko.

Katika kongamano hilo, NSSF licha ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii pia itaeleza fursa mbalimbali zinazopatikana zikiwemo za nyumba na viwanja ambazo zinauzwa kwa bei nafuu.

MWISHO