MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO AKIMSINDIKIZA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI

March 31, 2023
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris wakati akiwaaga wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kumuaga baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili nchini, leo tarehe 31 Machi 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakimuaga Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na Mumewe Douglas Emhoff katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 31 Machi 2023 mara baada ya kuhitimisha ziara nchini Tanzania. (Picha Ofisi ya Makamu wa Rais)

HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO KUANZISHA KLINIKI ZA KIBINGWA ZA JIONI

March 31, 2023



HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inatarajia kuanzisha huduma za Kliniki za Kibingwa wakati wa muda wa ziada wa jioni itakayoanza Aprili 11 mwaka huu katika hospitali hiyo.

Akizungumza leo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan (Pichani) amesema huduma hizo zitaaza saa tisa na nusu jioni mpaka muda ambao wagonjwa watamalizika ambao watapata fursa ya kuonana na madaktari bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.

Dkt Juma alisema kwamba katika kliniki hiyo huduma mbalimbali za kibingwa ikiwemo magonjwa ya ndani,magonjwa ya ya upasuaji,magonjwa ya wakina mama,magonjwa ya watoto,magonjwa wa koo,pua pamoja na sikio .

Aidha alisema kwamba huduma hizo zitatolewa kwa wagonjwa wote wenye bima bila kujalia aina gani ya bima lakini pia wale wagonjwa wanaofanya malipo ya keshi yatapokelewa.

Hata hivyo alisema huduma hiyo itatolewa siku Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa tisa na nusu mpaka pale watakapomalizika.

Dkt Juma aliwahimiza wananchi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kliniki hizo ili kuweza kukutana na madaktari bingwa wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

Hata alisema uwepo wa kliniki hiyo utasaidia kutoa fursa kwa wagonjwa kuweza kukutana na madaktari bingwa ambao wataweza kuwasaidia hivyo watumie nafasi hiyo kuweza kuonana na madaktari hao bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.



Mwisho.





TASAC YATUMIA MAONESHO YA BIASHARA,UWEKEZAJI NA FURSA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

March 31, 2023


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu kwa wananchi kuhusu namna linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria wakati wa maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Fursa yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mashujaa kuanzia tarehe 19 hadi 31 Machi, 2023 Mkoani Mtwara.

Akizungumza na vyombo ya habari wakati wa maonesho hayo Kaimu Afisa Mfawidhi wa Mkoa wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Mkoa wa Mtwara,Joseph Myaka amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao shirika hilo limejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shirika hilo linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo waliamua kushiriki maonesho hayo ili kuwapa elimu wananchi kuhusu fursa za biashara zilizopo katika Sekta ya Usafiri kwa njia ya Maji sambamba na elimu kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira majini jukumu linalotekelezwa na Shirika hilo.

“TASAC tunashiriki maonesho haya ya Biashara Uwekezaji na Fursa mkoani Mtwara ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yanayotekezwa Kisheria. kama mdhibiti wa shughuli za usafiri kwa njia ya maji tunasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, tunadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba majini”

“Pia tunatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na wadau wa usafiri kwa njia ya maji katika jukumu letu la Udhibiti wa Safari kwa njia ya Maji na udhibiti Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira majini, wanaweza kufanya shughuli zao kwa usalama na kupata maendeleo na kuongeza pato la Taifa.” Ameeleza Joseph.

Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.

Maonesho hayo ya Biashara, Uwekezaji na Fursa ni maonesho ya Kwanza kufanyika Mkoani Mtwara yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza biashara na uwekezaji wa kisasa pamoja na fursa zilizopo katika sekta hiyo na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla.





BENKI YA CRDB YAANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE

March 28, 2023

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally  (katikati) akiwa ameambatana na Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, wakiongozana na Mwenyeji wako, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakati walipowasili kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 1,000. Picha zote na Othman Michuzi.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (watano kulia) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Abdulmajid Nsekela (watatu kulia) wakikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa watoto wawakilishi wa moja ya kituo cha kuwalea watoto yatima, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya  CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Kaimu Sheikh wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja wake, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha CRDB Al-Baraq, Rashid Rashid akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau, pamoja na vituo vya watoto yatima, iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.













 

KUELEKEA KIKAO KAZI CHA 18 CHA TAGCO KESHO, NAIBU KATIBU MKUU SELESTINE KAKELE AKAGUA MAANDALIZI YA MWISHO

March 27, 2023

NA KHALFAN SAID

MAANDALIZI ya mwisho ya Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kinachoanza kesho Jumatatu Machi 27, 2023 jijini Dar es Salaam yamekamilika.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho kitakachofanyika kwa siku tano kuanzia Machi 27-31 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

Ili kuhakikisha kila kitu kiko sawa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele akifuatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa pamoja na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Msika na Katibu Mkuu Bw. Abdul Njaidi wametembeela na kukagua ukumbi wa mkutano JNICC.

 Kikao hicho kinawaleta pamoja Maafisa Habari na Maafisa Uhusiano kiasi cha 500 wote wa Serikali ili kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuboresha utendaji kazi, kupeana mbinu mbalimbali za kufanya mawasiliano na namna ya kulinda taswira ya nchi na serikali, Katibu Mkuu wa TAGCO Bw. Abdul Njaidi amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele (mbele) akiongozana na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Msika na Katibu Mkuu wake Bw. Abdul Njaidi wakitembeela ukumbi wa mkutano

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa (wanne kushoto) Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Msika (wapili kushoto) wakimsikilzia Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi wakati Naibu Katibu Mkuu alipokuwa akikagua maandalizi ya mwisho ya kikao hicho kinachoanza kesho Jumatatu Machi 27.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele (kulia) akimsikilzia Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus wakati kiongozi huyo alipokutana na Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo.











Khalfan Said 0716745281