KUELEKEA KIKAO KAZI CHA 18 CHA TAGCO KESHO, NAIBU KATIBU MKUU SELESTINE KAKELE AKAGUA MAANDALIZI YA MWISHO

March 27, 2023

NA KHALFAN SAID

MAANDALIZI ya mwisho ya Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kinachoanza kesho Jumatatu Machi 27, 2023 jijini Dar es Salaam yamekamilika.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho kitakachofanyika kwa siku tano kuanzia Machi 27-31 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

Ili kuhakikisha kila kitu kiko sawa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele akifuatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa pamoja na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Msika na Katibu Mkuu Bw. Abdul Njaidi wametembeela na kukagua ukumbi wa mkutano JNICC.

 Kikao hicho kinawaleta pamoja Maafisa Habari na Maafisa Uhusiano kiasi cha 500 wote wa Serikali ili kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuboresha utendaji kazi, kupeana mbinu mbalimbali za kufanya mawasiliano na namna ya kulinda taswira ya nchi na serikali, Katibu Mkuu wa TAGCO Bw. Abdul Njaidi amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele (mbele) akiongozana na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Msika na Katibu Mkuu wake Bw. Abdul Njaidi wakitembeela ukumbi wa mkutano

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa (wanne kushoto) Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Msika (wapili kushoto) wakimsikilzia Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi wakati Naibu Katibu Mkuu alipokuwa akikagua maandalizi ya mwisho ya kikao hicho kinachoanza kesho Jumatatu Machi 27.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele (kulia) akimsikilzia Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus wakati kiongozi huyo alipokutana na Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo.











Khalfan Said 0716745281

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »