AFISA Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin akimuonyesha mmoja wa watumiaji wa vyombo vya majini namna ya kuvaa jaketi okozi
|
Na Mwandishi Wetu,Morogoro
SHIRIKA
la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imetoa elimu ya Usalama, ulinzi na
utunzaji wa mazingira mkoani Morogoro pamoja na kuendesha zoezi la
ukaguzi wa Vyombo vya usafiri majini.
Ukaguzi
huo ni sehemu mikakati ya Shirika hilo kuhakikisha vyombo vya usafiri
majini vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa kuzingatia viwango.
Zoezi
hilo liliendeshwa na Maafisa Ukaguzi na Udhibiti wa Vyombo vya Majini
wa Shirika hilo, Bw. Gabriel Manase na Maulid Nsalamba katika wilaya ya
Ifakara mkoani humo. Maafisa hao walitoa elimu ya usalama na ulinzi
ikiwemo utunzaji wa mazingira wanapokuwa kwenye shughuli zao
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo Manase alisema elimu hiyo ina umuhimu mkubwa sana
hivyo jamii inapaswa kuitambua na kuweza kuzuzungatia wakati wote
wanapotekeleza shughuli zao za kila siku.
Zoezi
hili lilianza tarehe 11 Novemba, 2022 ifakara katika maeneo ya
Ngalimila, Ngapemba, Utengule, Chita na Mngeta na Mchombe na litaendelea
katika mikoa ya iringa na Dodoma lengo ni kuhakikisha jamii inapata
elimu.
Zoezi
hilo liliendeshwa pia kwa ushirkiano na Afisa Masoko Mwandamizi wa
TASAC Martha Kelvin na Afisa Uhusiano Mwandamizi Amina Miruko ambapo
waliitaka jamii kuhakikisha inazingatia usalama kwenye vyombo vya maji
ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinazaweza kuwakuta wawapo
safarini.
EmoticonEmoticon