Wizara
ya Afya leo imepokea vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi
203,550,000 kutoka Shirika la USAID kwa kushirikiana na JHPIEGO kupitia
mradi wake wa Momentum Challenge Global Leadership (MCGL).
Akiongea
wakati wa hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi
ametaja vifaa hivyo kuwa ni kompyuta za mezani (Desktops) zipatazo 75
ambazo kupitia Idara yake ya Mafunzo zitasambazwa kwenye vyuo vya kada
za Afya vipatavyo sita(6) pamoja na Wizara Makao Makuu.
Prof.
Makubi ameishukuru USAID kwa mchango wao mkubwa ambao utakwenda
kuboresha mafunzo ya TEHAMA vyuoni na itasaidia kuzalisha wataalamu wa
afya wenye ujuzi na umahiri kwenye matumizi hayo nchini.
Ameongeza
kuwa vifaa hivyo pia vitachangia kuboresha huduma za mafunzo na
amevitaka vyuo vyote vitakavyonufaika na vifaa hivyo kuhakikisha
wanatunza na kutumia kwa shughuli zilizokusudiwa.
Hata hivyo
Prof. Makubi alitumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa vyuo vya afya nchini
kuzingatia weledi na maadili ya utumishi wa umma kwa maendeleo ya Taifa
.
“Ni wakati muafaka kwenu ninyi Viongozi kufanya kazi kwa bidii
na kuhakikisha kuwa mnazingatia maadili yote ya kitaaluma ili mzalishe
wataalamu wenye uwezo katika kusaidia utoaji wa huduma za afya zenye
ubora.
Kwa upande wake Mwakilishi wa USAID Dkt. Patrick Swai
amesema kuwa USAID itaendelea kuisaidia Wizara ya Afya katika kuboreaha
utoaji wa huduma za afya nchini.
Dkt. Swai ameongeza kuwa
Tanzania ni nchi mojawapo zilizopewa kipaumbele katika mpango wa
kushughulikia vifo vinavyoweza kuzuilika vya wajawazito na watoto.
Naye
Mkurugenzi wa Jhpiego nchini Bi.Alice Christensen amesema kuwa Shirika
lake litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali na kuahidi kuwa
mshirika hai katika kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »