NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA 9 YA VIWANDA,BIASHARA NA UTALII JIJINI TANGA

May 31, 2022

 

Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akitoa elimu kwa wananchi walofika kwenye Banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini hapa kunakoendelea maonyesho ya biashara kulia aliyekaa ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda

Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule za Msingi walofika kwenye Banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini hapa kunakoendelea maonyesho ya biashara  kulia aliyekaa ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda

Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanaga wakiwahudumia wananchi kama wasikiliza kwa umakini wananchi waliotembelea banda lao katika ni Mkaguzi wa NSSF Mkoa wa Tanga Hadija Mpungu kulia ni Afisa Mwandamizi wa NSSF Muheza Fatma Ally  kushoto ni Afisa Matekelezo wa Pangani Hery Kaluyenda
Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama  katika akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Mkoa wa Tanga (TCCIA) Rashid Mwanyoka kushoto wakati walipotembelea banda lao


Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari.


 

NA OSCAR ASSENGA, TANGA. 

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) Mkoani Tanga umesema kwamba wanatumia  maonyesho ya Biashara ya mwaka 2022 yanayoendelea kwenye viwanja vya mwahako kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye mfuko huo

Hayo yalisemwa leo na Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya Biashara. 

Alisema kwamba uwepo wa maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka umekuwa na tija na kwa na bahati nzuri mwaka huu wao wamekuwa moja ya wadhamini hivyo wameona fursa nyingi zinatokea pamoja na kuwa na mkutano na wafanyabiashara na wao kuelezea changamoto walizokuwa nazo na nini kuboreshwe na nini kiongezwe kwenye huduma wanazotoa kwa mkoa huo.

"Kwa kweli niwaambie kwamba maonyesho ya mwaka huu  yamefana kuliko yalivyokuwa miaka iliyopita kutokana na washiriki wamekuwa wengi kutoka 62 mpaka 95 mwaka huu na hiyo ni faida kwetu kwani tumeweza kuandikisha wanachama 53 na waajiri wapya wawili"Alisema

Aliongeza kwamba hatua hiyo inawaweka vizuri katika malengo yao na inawasaidia kuongeza wanachama na kuongeza michango inayofikia kwenye malengo yao ya wanachama wa Sekta ya viwanda na Utalii ambapo kuna wajasiriamali wadogo kupitia NSSF sekta isiyokuwa rasmi wanaweza kuongea nao na kuweza kuwapa elimu na wawo kuweza kuwapa mapendekezo ya aina gani ya mafao watakayopenda .

Hata hivyo alisema tokea kuanza mwa maonyesho hayo mpaka sasa wamekwisha kuandikisha wanachama 51 na waajiri 3 huku lengo lao la siku 10 za maonyesho hayo waandikishe wanachama wapya 230 na waajiri 14

WAZIRI NDAKI AWATAKA WATANZANIA WANYWE MAZIWA

May 30, 2022


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya Unywaji Maziwa yanayofanyika mkoani Katavi leo (30.05.2022), kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mwanamvua Mrindoko na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani.
Afisa Uendeshaji wa mfuko wa uwekezaji wa UTT AMIS, Abbas Kandila (kulia) akitoa maelezo yanayohusu mfuko huo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) muda mfupi leo (30.05.2022) kabla hajafungua Maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya Unywaji Maziwa yanayofanyika mkoani Katavi. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani akifuatiwa na Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini, Dkt. George Msalya.Afisa Uhusiano wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Bi. Neema Mtemvu (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Shirika hilo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kutoka kushoto) muda mfupi leo (30.05.2022) kabla hajafungua Maadhimisho hayo yanayofanyika mkoani Katavi, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani.Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) akipokea ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wafugaji (hayupo pichani) aliyefika kwenye Maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya Unywaji  Maziwa yanayofanyika Mkoani Katavi, Muda mfupi kabla ya kufungua Maadhimisho hayo leo (30.05.2022), Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ametoa rai kwa Watanzania kuongeza kasi ya kunywa maziwa ili kila mmoja afikie kiwango kinachoshauriwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)  na Shirika la Chakula na Kilimo Ulimwenguni (FAO).

Mhe. Ndaki amesema hayo leo (30.05.2022) wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya Unywaji Maziwa yanayofanyika kwenye Uwanja wa Azimio uliopo Mpanda mkoani Katavi.

“Binafsi sielewi kwa nini Watanzania hatunywi maziwa kwa sababu Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) na Shirika la Chakula na Kilimo duniani (FAO), Kila Mtanzania anapaswa kutumia wastani wa lita 200 za maziwa kwa mwaka lakini mpaka sasa takwimu zinaonesha kila Mtanzania anakunywa wastani wa lita 62 tu za maziwa kwa mwaka ambazo kama tukizigawanya kwa siku 365 za mwaka mzima utaona ni kama anakunywa tone tu la maziwa kwa siku na takwimu hizo ni kwa waliohesabiwa pekee” Amesema Mhe. Ndaki.

Mhe. Ndaki ameweka wazi faida za unywaji maziwa kwa watoto hasa wanafunzi ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa wataalam wa afya bidhaa hiyo humsaidia mtoto kuimarisha ubongo wake, kuimarisha meno, kumuongezea kumbukumbu na nguvu wakati wote, kuongeza kiwango cha madini ya wanga na madini mengine yanayohitajika mwilini na kuimairisha misuli yake.

“Maziwa ni chakula cha msingi na muhimu sana ndugu zangu Watanzania hivyo tunyweni kwa sababu yatatusaidia kwa afya zetu” Amesisitiza Ndaki.

Akielezea mikakati ya kuhakikisha kiwango cha uzalishaji wa maziwa nchini kinaongezeka, Mhe. Ndaki amesema kuwa hivi sasa Wizara yake ipo kwenye kampeni maalum ya kuelimisha na kuhamasisha ufugaji wa kisasa ambayo inalenga kuwabadilisha  wafugaji kutoka kwenye mfumo wa ufugaji wa asili unaojumuisha mifugo mingi isiyo na tija na kuwafanya kuwa na mifugo mingi yenye tija na inayoweza kubadili maisha yao.

“Kwa hivi sasa lita 1 ya maziwa ukiikuta “supermarket” inauzwa shilingi 4,000 na kwingine ni hadi 4,500 lakini kama tukiongeza kiwango cha uzalishaji wa maziwa kupitia kampeni yetu ya kuwahasisha wafugaji kufuga kisasa, bei ya hiyo lita 1 inaweza kufika hadi  shilingi 2,000 au chini ya hapo na hapo tutafanikiwa kuwafanya Watanzania wengi kumudu kununua maziwa na hivyo kuongeza kiwango cha unywaji maziwa hapa nchini” Amesema Ndaki.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko ameishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Bodi ya Maziwa nchini (TDB) kwa kupeleka maadhimisho hayo mkoani humo ambapo amewataka wananchi wote wa mkoa huo kutumia fursa hiyo kujifunza namna  ya kufuga kisasa kupitia elimu mbalimbali zinazotolewa na wataalam wa sekta ya ufugaji waliopo kwenye Maadhimisho hayo.

“Lakini pia tunaamini kabisa kwamba ujio wa maadhimisho haya utaongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi wetu, utawaongezea kipato na tunaongeza “connection” na masoko,wazalishaji na wenye viwanda ili kujifunza namna bora ya uwekezaji hivyo niombe ikiwezekana maadhimisho haya kila Mwaka yafanyike hapa Katavi na tupo tayari kwa hilo wakati wowote ule” Amesema Mhe. Mrindoko.

Mhe. Mrindoko alitumia fursa hiyo pia kuishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusudio lake la kujenga kituo cha kukusanyia maziwa mkoani kwake ikiwa ni moja ya vituo 10 ambavyo Wizara hiyo imepanga kujenga kwa mwaka ujao wa fedha ambapo amesema kuwa kituo hicho kitaokoa kiasi kikubwa cha maziwa yaliyokuwa yakiharibika mkoani humo kutokana na kukosa miundombinu ya kuhifadhia.

“Kwetu hiyo pia ni fursa nyingine ya kuboresha soko la maziwa yanayozalishwa hapa Katavi lakini pia itatuhakikishia zaidi kuboreshwa kwa lishe ya wananchi wetu kupitia maziwa kwa sababu watakuwa na uwezo wa kupata huduma hiyo wakati wowote wakihitaji” Amesema Mhe. Mrindoko.  

 Akizungumzia mchango wa Tasnia ya Maziwa kwenye soko la ajira, Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini (TDB) Dkt. George Msalya amesema kuwa kwa mujibu wa tawimu zilizopo mpaka sasa, Lita bilioni 3.4 za maziwa ambazo huzalishwa hapa nchini zina thamani ya dola za marekani bilioni 1.2 ambazo huingia kwenye mzunguko wa wadau wote wanaojihusisha na mnyororo wa thamani wa bidhaa hiyo.

“Kwa hiyo nitoe rai kwa Watu wote kuongeza nguvu kwenye uwekezaji wa Tasnia hii kwa sababu hata kwa upande wa ajira, takwimu zinaonesha kuwa lita 1 ya maziwa hutoa ajira 4 kwa Watanzania” Amesema Dkt. Msalya.

Maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya Unywaji Maziwa hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha unywaji wa maziwa na kufanya tathmini ya maendeleo ya Tasnia ya Maziwa nchini.

KITUO CHA SAYANSI CHA STEMP PARK CHA JIJINI TANGA KIMELETA MAGEUZI MAKUBWA

May 30, 2022

Meneja wa kituo cha Sayansi Maxi George akizungumza wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kilipoanzishwa
Sehemu ya wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali


Na Oscar Assenga,TANGA

Kituo cha Sayansi cha Stemp Park kilichopo Jijini Tanga kimeleta Mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya elimu ambapo kimeweza kuwa kichocheo kwa Wanafunzi kuhamasika kupenda kusoma Masomo ya Sayansi na kuongeza ubunifu.

Stemp Park ipo katika kata ya Kisosora na imeleta mapinduzi makubwa katika masomo ya Sayansi kwa Wanafunzi pamoja na Walimu.

Wanafunzi wanaotumia kituo hicho katika mambo ya Sayansi ni kianzia Chekechea hadi shule za Sekondari.

Akizungumza juzi katika wiki ya Sayansi Afrika Meneja wa kituo hicho Maxi George wakati wa halfa ya kituo hicho kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa Kwake iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya sayansi katika bara la Afrika

Ambapo alisema idadi kubwa ya ubunifu wa kisayansi katika jiji la Tanga umekuwa mkubwa ambapo wanafunzi wamekuwa wakienda kituo hicho na kufanya shughuli zao za ubunifu ambapo wanafanya wa nadharia zaidi.

"Hapa vijana wanapata nafasi ya kuelezwa umuhimu wa Sayansi katika maisha ya kawaida,na katika maisha ya shule kwa kujifinza mambo mbalimbali ya sayansi kwa vitendo na kwa kuona"alisema George

Katika hatua nyingine kituo hicho pia kinawanufaisha walimu wa mkoa wa Tanga kwa kuwapa ujuzi katika kuwafundisha wanafunzi shuleni

"Walimu wanaprogram maalum ambayo inaitwa TOT hii imekuwa chachu ya kuwapa ujuzi katika kuwafundisha vijana,lengo likiwa ni kuchagiza ufaulu kwa masomo ya sayansi"alisema George

Pia aliwaasa wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wajifunze masomo ya Sayansi kuwa sio ngumu bali watu waliaminiashwa kuwa ni ngumu

"Tunatoa wito kwa Wazazi,kuwaachia watoto wajifunze zaidi,pale mtoto anapofanya jambo la ubunifu mzazi amwache akifanye ili apate njia sahihi ya kutengeneza kitu anachokitaka ambacho badae kinaweza kuwa na manufaa"alisema George

Aidha Wanafunzi wanaoenda kwenda kujifunza katika kituo hicho wameeleza kuwa kituo hicho kimewajenga zaidi kwa kuwa wabinifu.

Mmoja wa wanafunzi wa kike Rukia Omari wa Masechu Sekondari anayenda kupata elimu ya Sayansi katika kituo hicho alisema wao wanakabiliwa na changamoto pindi wanapotaka nafasi ya kwenda kujifunza katika kituo hicho kwa kuwa wazazi wanawabana kupatamuda wa ziada ya kujifunza Sayansi

"Mazingira tunayoishi inatufanya wasichana tusiwesawa na wavulana katika kujifunza,ukiomba ruhusa kwenda kujifunza huwezi kupewa,utaambiwa bora umsaidie Mama kazi hivyo kufanya mua wa kusoma usiwepo lakini kwa wanaume iko tofauti akirudi hana kazi"alisema

WAZIRI MCHENGERWA AWAKABIDHI KOMBE LA EUFA MASHABIKI WA REAL MADRID

May 28, 2022

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  akizungumza kabla ya kukabidhi Kombe hilo

 Na John Mapepele


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewakabidhi kombe la EUFA mashabiki wa timu ya Real Madrid baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa usiku wa kuamkia leo huku akisisitiza kuwa  Wizara yake itaendelea kuwa bunifu kwenye sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuwapa furaha watanzania.

Mhe. Mchengerwa amesema hayo kwa wapenzi soka  katikati ya Daraja  la Tanzanite jijini Dar es Salaam kwenye tukio maalum la kuangalia mubashara fainali za EUFA lililoratibiwa na kampuni ya kinywaji cha  Heineken kwa  kushirikiana na Wizara  ya Utamaduni, Sanaa na Michezo usiku wa kuamkia leo.

Katika fainali hii timu ya Real Madrid imeibuka bingwa wa  kombe la EUFA wa mwaka huu baada ya kuibamiza Liverpool bao moja katika kipindi cha pili cha mchezo.

Ameongeza kuwa  sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo nguvu shawishi za taifa lolote duniani.

Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuitangaza na kuifungua Tanzania duniani kupitia Filamu ya Royal Tour.

Kabla ya mechi hiyo mamia ya watu waliohudhuria waliopata fursa ya kuangalia Filamu hiyo ya Royal Tour.

Ameongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau  wataratibu tukio  maalum la kuionesha  Filamu ya Royal Tour kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijijini ili wananchi wengi waweze kupata fursa ya kuiangalia.

Aidha, amewataka wadau mbalimbali wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea  kushirikiana na Wizara   katika kuleta mapinduzi makubwa  kwenye sekta hizo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kampuni ya kinywaji cha Heineken nchini ambayo ndiyo aliyedhamini kuonyesha mubashara fainali hizo hapa nchini kupitia DSTv amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa faida wananchi wa Tanzania.

Katika tukio hilo Mhe. Waziri aliambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu na Watendaji wengine wa Wizara hiyo.

WAZIRI MCHENGERWA ATEMA CHECHE KWA VIONGOZI WA MICHEZO,ATAKA WABADILIKE

May 27, 2022




Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa akizungumza wakati wa akifunga kikao kazi cha viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini kilichoratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)



Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa amewataka  viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini kutotumia taasisi wanazoziongoza kujinufaisha kwa  vipato tu na badala yake wawe wabunifu na wazalendo ili kuleta  mapinduzi kwenye  michezo  na kuendana  na maono ya Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ya kutumia michezo kuleta uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.


 Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Mei 27, 2022 wakati akifunga  kikao kazi cha viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini  kilichoratibiwa  na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufuatia  maelekezo yake aliyoyatoa wakati akiisimika Bodi  ya BMT hivi karibuni ya kutaka kuwa na utawala bora kwenye vyama na mashirikisho ya michezo ili kuendeleza michezo.


 Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa yapo  mataifa  mbalimbali duniani ambayo  hayana miundombinu ya michezo na  yana idadi ndogo ya watu ukilinganisha  na Tanzania  lakini yamekuwa yakifanya  vizuri kwenye  michezo hivyo amewataka kubadili fikra  potofu ili wanaowaongoza waige  mifano kutoka  kwao hatimaye kuleta mapinduzi makubwa kwenye michezo. 


 “Hatutaweza kupiga hatua kwenye michezo kama   sisi viongozi hatutaweza kubadilika na kuendelea kuwa na fikra potofu ya kudhani vyama na mashirikisho ni mahali pa kujipatia vipato tu. Nawaomba tubadilike mimi katika kipindi changu sitaweza kuruhusu kutokea hayo. Mpango wa matumauni ya kesho lazima tuanze kujenga leo”. ameongeza Mhe. Mchengerwa.


Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeelekeza nguvu kubwa kuendeleza sekta za utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo maana iliunda upya Wizara hii ili iweze kujitegemea, kuongeza bajeti, kutoa punguzo kwenye nyasi bandia ili kuimarisha viwanja vya soka pamoja na kuanzisha mfuko wa maendeleo ya michezo.


Ameongeza kuwa mfuko huo umepewa chanzo madhubuti ambacho  ni fedha za asilimia tano ya mapato yatokanayo na michezo ya kubashiri matokeo ya michezo.


Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimejadili kwa kina vigezo   vya muongozo wa kusaidia timu za taifa  kwa kutumia fedha za mfuko wa maendeleo ya michezo na kuja na mawazo ambayo yatafanyiwa  kazi na serikali ili kuwa na uwazi katika usaidiaji wa  timu hizo katika michezo mbalimbali.  


Aidha, amewasihi viongozi hao kufuata  miongozo na taratibu za nchi  sambamba na kuziheshimu  mamlaka  na taasisi zinazosimamia michezo nchini,  kuimarisha  utawala bora na weledi  katika kazi.


Mambo mengine ni pamoja na kuimarisha eneo la utaalamu na taswira za    taasisi zao kwa kuwa na mikakati yenye dira.


Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kujenga miundombinu mipya na ya kisasa ya michezo ambapo kwa upande wake Naibu Waziri, Mhe, Pauline Gekul amewataka wadau washirikiane na kupendana ili kuongoza kwa mafanikio.


Naye Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi amewataka viongozi hao kuwa wabunifu wa kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato badala ya kutegemea Serikali pekee.

WAZIRI MCHENGERWA ATOA SALAMU AFRIKA

May 25, 2022

 



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa

Na Shamimu Nyaki - WUSM, Dodoma 


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa amewaasa watanzania kulinda na kuhifadhi rasilimali na kumbukumbu ambazo ni ushahidi wa Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika katika maeneo waliyopo ambayo kumbukumbu hizo zinapatikana.

Katika taarifa aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari leo  Mei 25, 2022 jijini Dodoma, Mhe. Mchengerwa amesema  Siku ya Afrika ambayo huazimishwa Mei 25 kila Mwaka,ni siku muhimu kwa waafrika wote ambapo kwa mwaka huu  imebebwa na Kauli Mbiu isemayo "Urithi wa Ukombozi, Fahari ya Afrika na Kazi Iendelee".

"Kuthamini utanzania wetu  ni jambo la msingi na ndiyo kielelezo na sifa iliyosababisha Umoja wa Afrika (AU) zamani (OAU) kuichagua Tanzania kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika na kuipa hadhi ya kuwa Mratibu wa Harakati za Ukombozi hadi nchi zote za Afrika zilipopata Uhuru mwaka 1994" amefafanua Mhe.Mchengerwa.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, ni wajibu wa jamii ya waafrika kuenzi kwa vitendo mashujaa wa Tanzania waliojitoa mhanga Kwa ajili ya Afrika chini ya Uongozi wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Katika kuadhimisha siku hiyo, watanzania wameaswa kutembelea Ofisi ya Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika  ili kujifunza na kuona ushahidi waTanzania katika kuikomboa Afrika.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MADINI AFUNGA JUKWAA LA KWANZA LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI JIJINI MWANZA

May 22, 2022

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru leo tarehe 22 Mei, 2022 amefunga Jukwaa la Kwanza la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania Katika Sekta ya Madini lililoanza tangu tarehe 20 Mei 2022 jijini Mwanza.


Jukwaa hilo lililoambatana na maonesho lilishirikisha wadau wa madini wakiwa ni pamoja na wachimbaji wa madini, watoa huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mabenki, na watendaji kutoka Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini.

Akizungumza kwenye ufungaji wa jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru amesema kuwa Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeandaa jukwaa kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanabaini fursa zilizopo na kushiriki kikamilifu kwenye Sekta ya Madini.

Amesema kuwa Wizara ya Madini itaendelea kuhakikisha watanzania wananufaika na Sekta ya Madini kupitia ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini pamoja na kutatua changamoto mbalimbali.

Aidha, amewataka wadau wa madini kushiriki katika zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu ili kuiwezesha Serikali kuweka mipango mbalimbali ya maendeleo.

_Wakati huohuo,_ Ndunguru ametoa tuzo na vyeti kwa wadhamini wa Jukwaa hilo wakiwa ni pamoja na  Equity Bank (Tanzania) Limited, CMS (Tanzania) Limited, Twiga Minerals Corporation Limited na BR Drilling Limited.

Wengine ni pamoja na Tansec Limited, Boart Longyear (Tanzania) Limited, Geita Gold Mining Limited, Williamson Diamonds Limited, Tembo Nickel Corporation Limited, BG Umoja Services Limited, Epsom Limited,  African Assay Laboratories, Tanga Cement Limited, Shanta Mining Co. Limited na SGA Guards Tanzania Limited.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Reuben Lekashingo sambamba na kushukuru kwa ushirikiano mkubwa unaotolewa na Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini amewataka wananchi kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini.

Naye Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga amesema kuwa jukwaa limewapa mwanga wadau wengi wa madini kuhusu dhana nzima ya ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini.

Aidha amesema kuwa  jukwaa hilo limetumika kama njia mojawapo ya kujadili  namna ya kuzitatua changamoto mbalimbali zinazoikumba Sekta ya Madini hususan kwenye eneo la ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Dennis Mwila akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Tume ya Madini kwa kuandaa jukwaa la kizalendo lenye lengo la kuhakikisha watanzania wanafahamu namna wanavyoweza kushiriki kwenye Sekta ya madini kupitia utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.

Aidha,  amewataka washiriki wa jukwaa hilo kuwa wazalendo kwenye utekelezaji wa shughuli zao na kupata fursa zaidi kwenye migodi ya madini.

SERIKALI IMETOA ZAIDI YA BILIONI 3 UKARABATI VYUO VYA SITA VYA WATOTO WENYE ULEMAVU

May 21, 2022
Naibu Waziri toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi akizungumza jambo Mwenyekiti  wa Watu Wenye ulemavu  toka Korogwe Vijijini Shaban Shekihiyo wakati wa ghafla ya ufunguzi wa chuo cha walemvu
Naibu Waziri toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi akizungumza jambo Mwenyekiti  wa Watu Wenye ulemavu  toka Korogwe Vijijini Shaban Shekihiyo wakati wa ghafla ya ufunguzi wa chuo cha walemvu
Naibu Waziri toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi kulia akicheza mziki na wanafunzi walemavu toka kituo cha YDCP kwenye ghafla ya ufunguzi wa Chuo cha walemavu


NA OSCAR ASSENGA,TANGA
 
SERIKALI ya awamu ya Sita inaoongozwa na Rais Samia Suluhu imetenga zaidi ya Shs bil 3 kwa ajili ya ukarabati wa vyuo Sita vya watoto wenye ulemavu nchini


Kauli hiyo imetolewa Jijini Tanga  na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa Chuo cha Ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu

Katambi alisema Serikali inatambua umuhimu wa kundi hilo na ilitoa maelekezo ya kufanyiwa ukarabati wa vyuo hivyo ili kutoa fursa kwa jamii hiyo kupata elimu itakayowasaidia kujifunza ufundi utakao wanufaisha katika maisha yao.


Aidha aliitaja mikoa ambayo ina vyuo hivyo ni pamoja na Daresalaam,Tanga,Tabora,Mtwara,Singida na Mwanza ambapo alisema kuwa kama vyuo hivyo vitatumika vizuri idadi kubwa ya watoto walemavu inaweza kujitegemea na kuingia katika ajira kwa maslahi ya maisha yao na familia zinazowazunguka.
 
Katambi aliongeza kuwa Mh:Rais Samia Suluhu ameziagiza Wizara zote zihakikishe zinatoa ajira kwa asilimia 3 kwa kundi hilo la walemavu ili kuwaondolea dhana ya kuwa wategemezi na watu wasioweza kujiajiri ama kuajiriwa.


"Lazima haki ya elimu,afya na ajira zitekelezwe kwa mujibu wa sheria za Nchi yetu,unafikiri bila ya kuliwezesha kundi hili kielimu na ufundi,utawaajiri wapi,nazima tuwaandae na tunaweza kupata watumishi bora"Alisema Katambi.


Hata hivyo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha wanapata eneo kubwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho ambapo kitakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi walemavu toka Kanda nzima ya Kaskazini.


Kwa upande wa katibu Tawala Mkoa Tanga Pili Mnyema alisema wapo walemavu elfu tatu ambapo Mkoa inawatambua na Serikali imeweka mazingira rafiki ili kuweza kuwawezesha.


Mnyema alisema kwa mwaka huu wa fedha tayari  Halmashauri imetoa Shs Mil 121 ambayo ni asilimia 2 ya Shs Mil 600 kwa ajili ya kuwawezesha walemavu.
 
Nae Mkuu wa Chuo hicho Joharia Msuya alisema changamoto ya chuo ni pamoja na kuwa na walimu 3 wa kuajiriwa jambo ambalo linazorotesha ufanisi wa majukumu ya kila siku.


Msuya alisema mbali ya walimu na wafanyakazi wasiokuwa walimu pia eneo la chuo hicho ni dogo ungilinganisha na idadi ya wanafunzi inayotakiwq kuhudumiwa ambapo wanatoka mikoa 3.

Mwisho.