NA OSCAR ASSENGA,TANGA
SERIKALI ya awamu ya Sita inaoongozwa na Rais Samia Suluhu imetenga zaidi ya Shs bil 3 kwa ajili ya ukarabati wa vyuo Sita vya watoto wenye ulemavu nchini
Kauli
hiyo imetolewa Jijini Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi
wa Chuo cha Ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu
Katambi
alisema Serikali inatambua umuhimu wa kundi hilo na ilitoa maelekezo ya
kufanyiwa ukarabati wa vyuo hivyo ili kutoa fursa kwa jamii hiyo kupata
elimu itakayowasaidia kujifunza ufundi utakao wanufaisha katika maisha
yao.
Aidha aliitaja mikoa ambayo ina vyuo hivyo ni pamoja na Daresalaam,Tanga,Tabora,Mtwara,Singida
na Mwanza ambapo alisema kuwa kama vyuo hivyo vitatumika vizuri idadi
kubwa ya watoto walemavu inaweza kujitegemea na kuingia katika ajira kwa
maslahi ya maisha yao na familia zinazowazunguka.
Katambi aliongeza kuwa
Mh:Rais Samia Suluhu ameziagiza Wizara zote zihakikishe zinatoa ajira kwa asilimia 3
kwa kundi hilo la walemavu ili kuwaondolea dhana ya kuwa wategemezi na
watu wasioweza kujiajiri ama kuajiriwa.
"Lazima
haki ya elimu,afya na ajira zitekelezwe kwa mujibu wa sheria za Nchi
yetu,unafikiri bila ya kuliwezesha kundi hili kielimu na
ufundi,utawaajiri wapi,nazima tuwaandae na tunaweza kupata watumishi
bora"Alisema Katambi.
Hata
hivyo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha wanapata eneo kubwa kwa
ajili ya ujenzi wa chuo hicho ambapo kitakuwa na uwezo wa kupokea
wanafunzi walemavu toka Kanda nzima ya Kaskazini.
Kwa
upande wa katibu Tawala Mkoa Tanga Pili Mnyema alisema wapo walemavu
elfu tatu ambapo Mkoa inawatambua na Serikali imeweka mazingira rafiki
ili kuweza kuwawezesha.
Mnyema
alisema kwa mwaka huu wa fedha tayari Halmashauri imetoa Shs Mil 121
ambayo ni asilimia 2 ya Shs Mil 600 kwa ajili ya kuwawezesha walemavu.
Nae
Mkuu wa Chuo hicho Joharia Msuya alisema changamoto ya chuo ni pamoja
na kuwa na walimu 3 wa kuajiriwa jambo ambalo linazorotesha ufanisi wa
majukumu ya kila siku.
Msuya
alisema mbali ya walimu na wafanyakazi wasiokuwa walimu pia eneo la
chuo hicho ni dogo ungilinganisha na idadi ya wanafunzi inayotakiwq
kuhudumiwa ambapo wanatoka mikoa 3.
Mwisho.
EmoticonEmoticon