NDAKI AVUNJA UKIMYA KUHUSU ENEO LA CHIBE

April 14, 2022

 



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) akiwaeleza wawakilishi wa wananchi wa vijiji vinavyozunguka lililokuwa eneo la kupumzishia mifugo la Chibe lililopo mkoani Shinyanga sababu za kuwaondoa kwenye eneo hilo muda mfupi baada ya kuwasili hapo leo (14.04.2022).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki muda mfupi kabla ya Mhe. Ndaki kuanza ziara ya ukaguzi wa shughuli mbalimbali zinazohusu  sekta ya Mifugo mkoani humo leo (14.04.2022).Mkaguzi Mkuu wa Nyama kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bw. Ernest Nigo (wa pili kutoka kushoto) akimuonesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) namna moja ya mitambo ya kusindika nyama iliyopo kwenye Machinjio ya Manispaa hiyo inavyofanya kazi  muda mfupi baada ya Mhe. Ndaki kufika Machinjioni hapo leo (14.04.2022). Kushoto ni Meneja wa Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo mkoani Mwanza, Bi. Lynn Andey.Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kutumia lililokuwa eneo la kupumzishia Mifugo la Chibe lililopo Mkoani Shinyanga  kwa msimamizi wa eneo hilo ambaye pia ni Meneja wa Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo Mwanza Bi. Lynn Andey (kulia)  leo (14.04.2022).

 
Sasa kutumika kuzalishia na kunenepeshea mifugo

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu  kuhusu hatma ya matumizi ya zaidi ya ekari 5000 za eneo  lililokuwa likitumika kupumzishia mifugo “holding ground”  la Chibe lililopo mkoani Shinyanga  , Hatimaye Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ameamuru wananchi  wote wanaofanya shughuli mbalimbali za kibinadamu kwenye eneo  hilo kuondoka ifikapo Agosti 30  mwaka huu.

Mhe. Ndaki ameyasema hayo leo (14.04.2022) mara baada ya kufika na kukagua eneo hilo ambapo amewataka wananchi wanaolitumia  kwa shughuli za kilimo kuhakikisha wameondoka mara baada ya mavuno ya mazao yao ambayo kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga huwa ni  kati ya mwezi Aprili hadi Agosti.

“Kwanza ni lazima mfahamu kuwa hili ni eneo la Serikali na mnaishi humo kimakosa na naona tayari mmelima aina mbalimbali za mazao tena bora mngeishia kulima tu, mmeamua kujenga na makazi kabisa, sasa serikali tunataka kulitumia na kwa kuwa hatutaki muone kama mmenyang’anywa mazao yenu ninawapa mpaka mwezi wa 8 muwe mmeshavuna na kuondoa mazao yenu” Amesema Mhe. Ndaki.

Aidha Mhe. Ndaki amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kufanya operesheni ya kuwaondoa  watu wote ambao watakuwa hawajaondoka kwenye eneo hilo baada ya muda uliowekwa ili Serikali kupitia Wizara yake iweze kuanza kulitumia  kwa ajili ya kuzalisha na kunenepeshea ng’ombe na mbuzi wa nyama watakaouzwa kwenye viwanda  vilivyopo hapa nchini.

“Tunataka kuendelea kuongeza mauzo yetu nje ya nchi hivyo mbali na Serikali kulitumia eneo hili kwa ajili ya kuongeza tija kwenye mifugo yetu hivyo tutawakaribisha pia wafanyabiashara binafsi na vikundi vya ushirika kuleta mifugo yao hapa kwa ajili ya kuiongezea thamani na kuiuza kwenye viwanda vyetu ambavyo vipo kama vitano hivi lakini vyote vinafanya kazi chini ya uwezo wake kwa kukosa malighafi” Ameongeza Ndaki.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi na  wananchi wa vijiji vinavyozunguka  eneo hilo,Mwenyekiti wa Kijiji cha Chibe ambacho ni moja ya vijiji vinavyotumia shamba hilo Bw.  Masalu Malale amekiri wao kuvamia  eneo hilo ambapo alibainisha kuwa yeye na wananchi wake wataondoka kwa hiyari ndani ya muda waliopewa kwa sababu uwepo wao hapo ulitokana na eneo hilo kutotumiwa na Serikali  kwa shughuli yoyote ya kiuchumi.

“Kwenye kijiji changu kuna kaya kama 10 ndani eneo hili na baada ya kutambua kuwa tupo kwenye eneo la Serikali tulikubaliana kuwa pindi ikitaka kutumia eneo hili tutaondoka bila tatizo lolote” Alisema Masalu.

Mbali na  kufika kwenye eneo hilo, Mhe. Ndaki alipata fursa ya kutembelea machinjio ya Manispaa ya Shinyanga ambapo baada ya kukagua namna shughuli zinavyofanyika kwenye machinjio hiyo aliuagiza uongozi wa Manispaa hiyo kuwahamasisha wafugaji waliopo Mkoani Shinyanga kwenda kuchinja mifugo yao kwenye machinjio hiyo ili kuiongezea uwezo wake wa kufanya kazi badala ya hivi sasa ambapo  jumla ya mifugo 36 pekee inachinjwa kwa siku badala ya mifugo 500 ambayo ingekidhi uwezo uliosimikwa wa machinjio hiyo.

“Tutashirikiana kutafuta wawekezaji watakaokuwa na uhakika wa kupata ng’ombe na mbuzi wa kutosha na masoko ya mifugo hiyo japo mmeniambia mmeshaanza mazungumzo na mtu mwenye nia ya kuwekeza hapa ila naomba muwe makini sana kwa sababu pale Machinjio ya Dodoma tulipata mwekezaji ambaye ametuletea ugomvi mkubwa sana kiasi cha kuifanya machinjio yetu kutofanya kazi yake kwa ufanisi” Amesema Ndaki.

Mapema kabla ya kuanza ziara yake Mhe. Ndaki alifika kumsalimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ambapo alipokea taarifa ya mkoa huo inayohusu  utekelezaji wa shughuli mbalimbali za sekta za Mifugo na Uvuvi.

MWISHO


MELI ZA MAGARI KUTUA BANDARI YA TANGA KUANZIA MWEZI MEI

April 14, 2022

 



Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya wadau wa Bandari ya Tanga walipotembelea bandarini baada ya kumalizika kwa kikao chao na mamlaka hiyo.


Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud akizungumza wakati wa wadau wa Bandari ya Tanga kilichofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu Nikodemas Mushi


Kaimu Mkurugenzi wa masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu Nikodemas Mushi akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara na kikao cha wadau wa Bandari ya Tanga

AFISA Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC )Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua akizungumza jambo wakati wa kikao cha wadau wa Bandari

Wadau wa kikao hicho wakifuatilia matukio mbalimbali

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

BANDARI ya Tanga inatarajiwa kuanza kupokea Meli za Magari ifikapo Mwezi Mei mwaka huu ambayo yatakuwa yakipelekwa kuhifadhiwa eneo la Mwambani Jijini Tanga .

Hatua hiyo inatajwa kwamba itafungua fursa mpya za kiuchumi kwenye Bandari ambayo kwa sasa inafanyiwa maboresho makubwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake.

Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud wakati wa ziara ya wadau wa Bandari ya Tanga walipotembelea bandarini baada ya kumalizika kwa kikao chao na mamlaka hiyo.

Meneja Mrisha alisema eneo la mwambani lina ukubwa wa hekta 176 sasa kama walivyosema wanatarajia kuhudumia shehena kubwa kutoka 750,000 mpaka kufikia Milioni 3000,000 hivyo mzigo utakuwa ni mwingi.

Alisema kutokana na hilo wamependelea eneo hilo watalitumia kufanya shughuli za nyengine ikiwemo kupakilia mizigo kwenye makontena na kuweka kontena tupu na shughuli zinazoambatana na shughuli za kibandari

Hata hivyo aliwaeleza wadau hao kuhusu maboresho ya Bandari ya Tanga ikiwemo jinsi mradi wa maboresho ulivyo mpaka sasa awamu zote tatu ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni kuongeza kina kutoka mita tatu mpaka mita 13 kwenye mlango bahari,sehemu ya kujeuzia meli na vifaa ambapo iligharimu Bilioni 172.3.

Alisema pia wameona maboresho ya base mbili zenye urefu mita 450 zilizogharimu Bilioni 256.8 na wameona ahadi iliyolewa na mkandarasi ambapo mpaka mwezi Mei watakabidhiwa kipande cha mita 150 na itakapofika octoba wakabidhi mita zote 450.

Hata hivyo alisema kwamba hoja ambazo zimewasilishwa na wadau kwenye kkao hivho wamezichukua na kwenda kuzifanyia kazi na wao wametusikiliza kuwaeleza namna maboresho makubwa yaliyofanyika na kuhaidi kuitumia kwa ajili ya kupitisha shehena zao.

Awali akzingumza mara baada ya ziara ya wadau hao kwenye Bandari hiyo kushuhudia maboresho makubwa yaliyofanyika Kaimu Mkurugenzi wa masoko na Uhusiano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Makao Makuu Nikodemas Mushi alisema mkutano huo ulikuwa na nia ya kukutana na wadau wanaohudumiwa na Bandari ya Tanga ambayo inayohudumia mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo nchi Jirani Rwanda.

Alisema kupitia mkutano huo wanaamini watafungua ukurasa mpaya wa kiboshara na lengo lao ni kuondoa nafasi ya maswali na hoja na changamoto mbalimbali ambazo hazijaweza kutoka upande mmoja kwenda mwengine.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa Masoko na Uhusiano alisema wadau wametoa maoni huku akieleza kwamba Meneja wa Tanga na timu yake wamesikia na wamejipanga tayari kuanza kuzifanyia kazimara moja,.

Alisema na suala ambalo linawahusu makao makuu watalibeba na kulipeleka huku ili yaweze kufanyiwa maamuzi na huo ni mkakati wa kimasoko

Mwisho.

 


WAVUVI WATAKIWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA KUEPUKA VIFO, KUPOTEZA MALI

April 08, 2022

 


Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akiwaonyesha wavuvi wa Mwalo wa Sahare Jijini Tanga namna ya kuvaa vifaa vya kujiokolea wanapokuwa majini wakati alipokwenda akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga na Mwalo wa Sahare Jijini Tanga mkoani Tanga kutoa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira
Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akiwaonyesha wavuvi wa namna ya kuvaa vifaa vya kujiokolea wanapokuwa majini wakati alipokwenda akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga mkoani Tanga  kutoa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira
Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akiwaonyesha wavuvi wa Mwalo wa Sahare Jijini Tanga vifaa vya kujiokolea wanapokuwa baharini ambavyo ni muhimu kuhakikisha wanakuwa navyo kabla ya kuingia majini kufanya shughuli zao wakati wa utoaji wa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira

Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akisisitiza jambo kwa wavuvi wa mwalo wa Sahare Jijini Tanga wakati wa utoaji wa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira
Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akisisitiza jambo wakati akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani MkingaAfisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akizungumza  jambo wakati akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga


AFISA Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la TASAC Kitengo cha Mahusiano na Masoko Amina Miruko akizungumza wakati wa utoaji wa elimu
kwa wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga

Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua kulia akifuatilia kwa umakini maswali kutoka kwa wavuvi,wamiliki wa vyombo



Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la TASAC Martha Kalvin akieleza jambo kwa wavuvi kuhusu umuhimu wa usalama wawapo kwenye shughuli zao

Sehemu ya wavuvi,wamiliki wa vyombo na manahodha wakimsikiliza Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira.

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesisitiza umuhimu wa wavuvi kuzingatia usalama ikiwemo kuwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea wanapokuwa katika shughuli za Uvuvi wawapo majini ili kuwaepusha na vifo,majeruhi na kupoteza mali.

Huku wakisisitiziwa umuhimu wa kuwa na vifaa vya kujiokolea wanapokuwa majini ili viweze kuwasaidia kuepukana na ajali ambazo wanaweza kukumbana nazo.

Wito huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua wakati na akizungumza na wavuvi, wamiliki wa vyombo, manahodha na wananchi wa Vijiji vya Monga Vyeru wilayani Mkinga na Mwalo wa Sahare Jijini Tanga mkoani Tanga walipokwenda kutoa elimu ya umuhimu wa usalama na utunzaji wa mazingira.

Alisema kwamba ni muhimu kwao kuweza kuhakikisha wanazingatia usalama wakati wanapokwenda kufanya shughuli zao kwani hilo litawaepusha na majanga ambayo wanaweza kukutana nayo na kupelekea kupata majeraha au kupoteza maisha na mali.

“Serikali imeona hilo ni jambo la msingi sana na ndio maana tumeona leo tuje hapa Monga Vyeru kuwapa elimu hii ya usalama  na utunzaji wa mazingira hususani mnapokuwa kwenye shughuli zenu hili ni jambo hilo lakini pia kuhakikisha mnakuwa na vifaa vya uokozi”Alisema

“Kwani tunatambua kwamba pia wavuvi wana familia hivyo elimu hii itaweza kuwasaidia kupunguza ajali,kuondoa vifo na kupunguza majeruhi na kuacha familia kuwa tegemezi”Alisema

Afisa Mfawidhi huyo alisema shughuli za usalama sio jambo la mtu mmoja bali ni watu wote hivyo lazima wahakikisha wanazingitia sheria za usalama ikiwemo kuvaa majaketi ya kujiokolea "life jacket" ili yaweze kuwasaidia pindi wanapokumbana na dhoruba baharini waweze kujiokoa.

“Lakini pia kuhakikisha tunakuwa tunazingatia usalama tuwapo majini moto unawaka kutokana na mafuta hauwezi kuuzima na maji ni lazima uhakikisha unatumia mchanga au poda maalumu “Alisema

Hata hivyo alisema ni muhimu na vizuri kwa wenye vyombo vinavyotumika kwa ajili ya shughuli za uvuvi wanakuwa na watu wenye ujuzi na kufanya kazi za majini ikiwemo wajibu wa mmiliki kutii sheria bila shuruti kuhakikisha usalama wake.

Hata hivyo Afisa Mfawidhi huyo aliwataka kuhakikisha kabla hawajaingia majini kuendelea na shughuli zao lazima wawe na cheti kutoka kwenye Shirika hilo ambavyo vinawaruhusu kufanya kazi majini.

“Lakini suala jingine sheria imemuelekeza Afisa Uvuvi asipope leseni ya uvuvi mpaka awe amepata cheti cha Shirika la TASAC cha kuruhusiwa kufanya kazi majini ”Alisema

ULEGA-TUTAENDELEA KULINDA RASILIMALI ZA UVUVI ILI ZIWALINDE WATANZANIA

April 08, 2022

 

.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye (kulia) namna Wizara yake ilivyojipanga kuwainua wavuvi wa Ziwa Tanganyika muda mfupi baada ya kufika ofisini kwa Mkuu wa mkoa huyo leo (08.04.2022).Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo ya DHL, Bw. Paulo Makolosi (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Ulega jinsi kampuni hiyo inavyofanya kazi zake ikiwa ni muda mfupi kabla ya makabidhiano ya Boti ya doria ya uvuvi yaliyofanyika leo (08.04.2022) kwenye Fukwe za Hoteli ya Hiltop mkoani Kigoma.Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo ya DHL, Bw. Paulo Makolosi (kushoto) akimkabidhi Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Ulega boti ya doria ya Uvuvi kwenye hafla iliyofanyika leo (08.04.2022) kwenye Fukwe za Hoteli ya Hiltop mkoani Kigoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah.


 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa Wizara yake itahakikisha inalinda rasilimali za Uvuvi wakati wote ili ziendelee kuwa mkombozi kwa wananchi wanaozunguka vyanzo mbalimbali vya maji ya asili vilivyopo hapa nchini.

Mhe. Ulega ameyasema hayo leo (08.04.2022) wakati wa hafla ya makabidhiano ya boti ya doria ya uvuvi iliyotolewa na Kampuni ya kimataifa usafirishaji wa mizigo ya DHL tukio lililofanyika kwenye ufukwe wa hotel ya Hiltop mkoani Kigoma.

"Kwa sasa tuna kikosi cha wataalam ambacho ni kitengo cha kulinda rasilimali zilizopo katika Ziwa Tanganyika na mtu anaweza asielewe umuhimu wa kazi inayofanyika lakini ni lazima tutekeleze jukumu hili ili kuhakikisha rasilimali hizi zinakinufaisha kizazi kilichopo na kijacho na ninatambua suala hili sio jepesi kwetu kwa sababu kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakinufaika kwa kutumia njia zisizo halali kwenye shughuli zao za Uvuvi" Amesisitiza Ulega.

Mhe. Ulega amesema kuwa Wizara ina mpango wa kukiongezea zaidi uwezo kikosi kazi hicho ili kiweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ambapo alibainisha kuwa wameshawasilisha mawazo ya kukiongezea nguvu kikosi hicho kwa mamlaka za juu ili kiweze kuwa na vitendea kazi vya kisasa na kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao.

"Hawa wanaobeza kazi ya ulinzi wa Rasilimali hizi siku wakiamka na kukuta hakuna samaki watakosa shughuli ya kufanya na watatuuliza wataalam tulikuwa tunafanya shughuli gani hivyo naomba muendelee na shughuli yenu ya ulinzi wa rasilimali hizi ili tuendelee kuunga mkono kampeni ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya Uchumi wa buluu ambao utamnufaisha kila mwananchi na Taifa kwa ujumla" Amesema Ulega.

Mhe. Ulega ameipongeza kampuni hiyo kwa kutoa boti hiyo ya ulinzi wa rasilimali za Uvuvi ambapo mbali na kutekeleza jukumu hilo la msingi amewataka wataalam watakaoisimamia kuhakikisha inatumika kutoa msaada hata kwa wavuvi watakaokumbana na changamoto mbalimbali wakiwa kwenye shughuli zao majini.

Mhe. Ulega ameishukuru kampuni ya DHL kwa msaada wa boti hiyo ambayo inafanya idadi ya jumla ya boti za doria zinazofanya kazi kwa upande wa Ziwa Tanganyika kuwa 10 huku nyingine ya 11 itakayokuwa ukanda wa Kigoma ikitarajiwa kutolewa na Serikali kabla ya Mwezi Mei mwaka huu.

"Sisi pale Wizarani tumekubaliana Dagaa la Kigoma liwe moja ya mazao yetu ya kimkakati na DHL wameiona hiyo fursa ambapo wao wameamua kujikita kwenye kuongeza thamani ya bidhaa hiyo mpaka inafika kwa mlaji huko nje ya nchi na niwaombe wadau wengine wenye nia ya kutumia fursa zilizopo Ziwa Tanganyika na kwingineko waje kwa sababu Serikali yetu inawakaribisha sana wawekezaji wenye nia ya kukuza uchumi wa mwananchi na kuongeza pato la Taifa " Amesema Ulega.

Akibainisha umuhimu wa boti hiyo kwa upande wa shughuli za Uvuvi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amesema kuwa itasaidia kuwezesha uvunaji endelevu wa rasilimali za uvuvi katika Ziwa Tanganyika.

"Kwa mujibu wa taarifa ya takwimu za Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2018 inaonesha kuwa Ziwa Tanganyika linaajiri moja kwa moja wavuvi 26612 ambao hutumia vyombo vya uvuvi 11506 na zaidi ya watu laki 7 hunufaika na shughuli zinazofanyika upande wa Ziwa Tanganyika" Amesema Dkt. Tamatamah.

Mbali na boti hiyo Dkt. Tamatamah amesema kuwa boti nyingine 9 zinazofanya kazi kwa upande wa Ziwa Tanganyika zipo katika vituo vya Kipili, Kasanga, Ikola na moja ikiwa katika kituo cha Buhingu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Paulo Makolosi amesema kuwa wakati wanafika mkoani Kigoma walikuta wasafirishaji wa dagaa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upoteaji wa mizigo yao ikiwa njiani, kupotea kwa ubora wa mazao hayo na kutokuwa na vifungashio bora vya kusafirishia mizigo yao.

"Dagaa walikuwa wakiuzwa kwenye mifuko maarufu kama "shangazi kaja" hivyo tukachukua jukumu la kulialika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambalo lilitoa mafunzo zaidi ya mara sita hapa Kigoma ambapo tuligharamia kila kitu ili kuhakikisha wafanyabiashara wa Kigoma wanabadilika na kufanya shughuli zao kwa kuzingatia viwango stahiki" Amesema Makolosi.

Ameongeza kuwa baada ya kumaliza mafunzo hayo, waliamua kutoa msaada wa vifungashio ambavyo vitasaidia kuzifanya bidhaa hizo zinazosafirishwa kutopoteza ubora wake hata zikikaa kwa muda mrefu.
 
Katika kuhakikisha sekta ya Uvuvi inaendelea kukua, Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza kwenye miundombinu ya masoko na mialo ya kisasa ya kupokelea samaki ukiwemo mwalo wa Kibirizi uliopo Kigoma, soko la Kasanga lililopo Sumbawanga, mwalo wa Ikola uliopo Katavi na soko la Kirando lililopo mkoani Rukwa.

WIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA VYENYE THAMANI YA MILIONI 200

April 05, 2022

 


Wizara ya Afya leo imepokea vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi 203,550,000 kutoka Shirika la USAID kwa kushirikiana na JHPIEGO kupitia mradi wake wa Momentum Challenge Global Leadership (MCGL).

Akiongea wakati wa hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi ametaja vifaa hivyo kuwa ni kompyuta za mezani (Desktops) zipatazo 75 ambazo kupitia Idara yake ya Mafunzo zitasambazwa kwenye vyuo vya kada za Afya vipatavyo sita(6) pamoja na Wizara Makao Makuu.

Prof. Makubi ameishukuru USAID kwa mchango wao mkubwa ambao utakwenda kuboresha mafunzo ya TEHAMA vyuoni na itasaidia kuzalisha wataalamu wa afya wenye ujuzi na umahiri kwenye matumizi hayo nchini.

Ameongeza kuwa vifaa hivyo pia vitachangia kuboresha huduma za mafunzo na amevitaka vyuo vyote vitakavyonufaika na vifaa hivyo kuhakikisha wanatunza na kutumia kwa shughuli zilizokusudiwa.

Hata hivyo Prof. Makubi alitumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa vyuo vya afya nchini kuzingatia weledi na maadili ya utumishi wa umma kwa maendeleo ya Taifa .

“Ni wakati muafaka kwenu ninyi Viongozi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuwa mnazingatia maadili yote ya kitaaluma ili mzalishe wataalamu wenye uwezo katika kusaidia utoaji wa huduma za afya zenye ubora.

Kwa upande wake Mwakilishi wa USAID Dkt. Patrick Swai amesema kuwa USAID itaendelea kuisaidia Wizara ya Afya katika kuboreaha utoaji wa huduma za afya nchini.

Dkt. Swai ameongeza kuwa Tanzania ni nchi mojawapo zilizopewa kipaumbele katika mpango wa kushughulikia vifo vinavyoweza kuzuilika vya wajawazito na watoto.

Naye Mkurugenzi wa Jhpiego nchini Bi.Alice Christensen amesema kuwa Shirika lake litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali na kuahidi kuwa mshirika hai katika kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.

IGP SIRRO AFUNGUA KITUO CHA POLISI CHA KISASA UWANJA WA NDEGE WA DODOMA

IGP SIRRO AFUNGUA KITUO CHA POLISI CHA KISASA UWANJA WA NDEGE WA DODOMA

April 05, 2022

 

 


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka watendaji wa Jeshi hilo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi kwa kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu na wahalifu wanazokutana nazo.

IGP Sirro amesema hayo wakati akifungua kituo cha Polisi cha kisasa kilichopo uwanja wa ndege wa Dodoma mkoani Dodoma ambapo ambao ujenzi wa Kituo hicho cha Polisi na nyumba ya Mkuu wa Kituo cha Polisi umegharimu kiasi cha milioni 115 hadi kukamilika kwake.

Kwenye ufunguzi huo IGP Sirro pia amesema kuwa, ni vyema viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kuwa macho na kuongeza umakini hasa katika kubaini wahalifu, waingizaji wa dawa za kulevya na wamakosa mengine kutokana na uwanja huo kutumiwa na watu mbalimbali kwa shughuli za usafiri wa anga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweli akimuwakilisha Mkuu wa mkoa huo Mhe, Antony Mtaka amesema kuwa, wilaya imeendelea kuhamasisha ufungaji wa kamera za usalama kwa ajili ya kuimarisha udhibiti wa uingizaji wa dawa za kulevya sambamba na uhalifu mwingine.

SEKTA ZA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NCHINI ZIMEKUA – MAJALIWA

SEKTA ZA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NCHINI ZIMEKUA – MAJALIWA

April 05, 2022

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Michezo wa Mwaka 2021 – 2031 baada ya kufungua Kikao Kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma, Aprili 5, 2022. Kushoto ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakala za kitabu cha Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Michezo wa Mwaka 2021 – 2031  baada ya kuuzindua kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma, Aprili 5, 2022. Wa pili kushoto ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, kulia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul na kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa  Kikao Kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua kikao hicho kwenye ukumbi wa  Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma, Aprii 5, 2022.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar jijini Dodoma  kufungua Kikao Kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara , Aprili 5, 2022. Kulia ni Waziri wa  Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

******************************

  • Awahimiza Watanzania kufanya mazoezi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini imekuwa kwa kiasi kikubwa na imeanza kuleta tija kwa maisha ya Watanzania kutokana na miongozo thabiti inayotolewa na Serikali

“Kwenye Sanaa tumeona namna ambavyo nchi hii imeweza kutangazwa vizuri na wasanii wengi kutoka ndani ya nchi, haya yote ni matokeo ya uratibu unaofanywa na Wizara, kwenye michezo tumeona namna ambavyo leo hii Tanzania inavyopata heshima kwa kuwa na timu za michezo mbalimbali zikifanya vizuri ndani na nje ya nchi.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 5, 2022) wakati akifungua kikao kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika katika Ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Amesema Sekta ya  Utamaduni, Sanaa na Michezo imeonesha kuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa vijana wengi na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla huku akitanabaisha kuwa sasa kwenye michezo kuna vijana wa Kitanzania wanaocheza michezo ya kulipwa katika nchi mbalimbali.

“Nitumie fursa hii kuwaasa Watanzania kuwa na moyo wa kuthamini kazi za wasanii wetu, Sanaa inatangaza taifa letu na utamaduni wetu pia unaitangaza nchi yetu.”

Waziri Mkuu amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili kuwawezesha Maafisa Utamaduni na Michezo kutimiza majukumu yao ipasavyo.

“Ni Muhimu sasa TAMISEMI kuhakikisha mnatambua umuhimu wa kitengo cha Michezo, Sanaa na Utamaduni katika Halmashauri kuwa ni moja kati ya vitengo muhimu ndani ya Halmashauri, na pia wapate nafasi ya kutumia taaluma yao kutekeleza majukumu ndani ya Halmashauri ili tuone mafanikio ya sekta hii”.

Aidha Waziri Mkuu ameagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha inaandaa vikao kazi vya maafisa utamaduni mara kwa mara ili kuwawezesha kupata mafunzo, kujua changamoto wanazopitia katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kupata muda wa kufanya tathmini ya maazimio yanayotolewa katika vikao kazi hivyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara hiyo kuhakikisha inaboresha uratibu na usimamizi wa mafunzo ya wataalamu wa michezo Nchini ili kuongeza idadi ya wataalam hao hususan katika mpira wa miguu kwani kumekuwa na kiwango kikubwa cha wakufunzi wa mpira kutoka nje ya nchi huku Tanzania ikikosa wakufunzi wanaofundisha nje ya Tanzania.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka Maafisa Utamaduni Sanaa na Michezo kusimamia na kuratibu vikundi mbalimbali vya mazoezi vilivyo katika maeneo yao. “Ni jukumu lenu kuhakikisha kila Afisa katika eneo lake anahamasisha na kuanzisha vikundi vidogo vidogo vya mazoezi ili kuwe na hamasa ya michezo kwa watu wa rika zote pamoja na kuibua na kukuza vipaji kwa vijana mbalimbali kwa kuratibu shughuli za makundi ya wasanii.”

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Omari Mchengerwa amesema Sekta ya michezo nchini imeendelea kuimarika na imechangia zaidi ya shilingi Bilioni 1.7 katika pato la Taifa na Wizara imeendelea kujipanga ili kuhakikisha mchango wa Sekta hiyo unafikisha shilingi  Bilioni 3 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

“Wizara imeendelea na mikakati ya kufanya maboresho ya miundombinu ya michezo, na hapa ni pamoja na maboresho ya ujenzi wa viwanja vya michezo katika shule 56 ambapo kila Mkoa utakuwa an Shule mbili za michezo, ikienda sambamba na uanzishwaji wa mkakati wa kuibua vipaji wa mtaa kwa mtaa.”

Katika kikao hicho Waziri Mkuu amezindua Mkakati wa Maboresho ya Sekta ya Michezo wa Mwaka 2021/2031 ambao utatoa muongozo wa kusimamia na kuboresha sekta ya michezo Nchini.

MWANANCHI MOMBO ASHINDA PIKIPIKI BONGE LA MPANGO

April 05, 2022

 

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi namba ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi namba ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi kofia ngumu (helmet) ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (katikati) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) akikabidhi kofia ngumu (helmet) ya pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (katikati) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (katikati) akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mshindi wa pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).
Mshindi wa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (kushoto) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga akitoa maneno ya shukran kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (kulia) kwa kupata zawadi hiyo. Ni baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Na ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. (Picha na Yusuph Mussa).
Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Mombo, kabla ya kukabidhi  pikipiki kwa mshindi wa  pikipiki ya miguu mitatu (guta) Justin Magali (hayupo pichani) mkazi wa Kijiji cha Bagamoyo, Kata ya Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga baada ya kushinda pikipiki hiyo kwenye shindano la Bonge la Mpango Awamu ya Pili. Ni katika hafla iliyofanyika Aprili 5, 2022 nje ya Ofisi ya NMB Tawi la Mombo. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mombo Eunice Mabogo. (Picha na Yusuph Mussa).



Na Yusuph Mussa, Korogwe

BENKI ya NMB imeendelea kutoa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu maarufu kama guta, baada ya mwananchi wa Kijiji cha Mazinde, Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Justin Magali (44) kuibuka mshindi.

Akizungumza leo Aprili 5, 2022 kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mombo Tawi la NMB Mombo, Meneja wa  Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper alisema washindi wa fedha taslimu pamoja na pikipiki ya miguu mitatu, ni wateja wote wa benki hiyo ambao wameweka akiba angalau kuanzia sh. 100,000.

"Ndugu Watanzania zawadi tulizoziandaa kwa wateja walioweka akiba  ya walau sh. 100,000 kwenye akaunti zao za NMB, waliingia kwenye orodha ya wanaostahili kushinda. Mpaka sasa tayari kupitia kampeni hii, tumeshatoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi mbalimbali. Pia tumepata washindi 50 wa pikipiki za miguu mitatu ya mizigo.

"Na huyu wa leo ni mshindi aliyejishindia pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya Sky Mark. Zawadi tulizotoa mpaka sasa zina thamani ya sh. milioni 300. Kikubwa leo tunatoa zawadi kwa mshindi wa Kampeni yetu ya Bonge la Mpango Awamu ya Pili ambayo tumeindesha kwa miezi mitatu iliyopita" alisema Prosper.

Prosper alisema Oktoba, 2021, walizindus kampeni maalumu yenye makusudi ya kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watanzania. Kampeni hiyo ilikuja kwa Awamu ya Pili baada ya mafanikio ya Awamu ya Kwanza iliyofanyika mpaka Juni, 2021.

"Kila wiki kulikuwa na washindi 10 wa pesa taslimu, na washindi wawili wa pikipiki za miguu mitatu. Kila mwisho wa mwezi kulikuwa na washindi watatu wa pikipiki za miguu mitatu, na droo kubwa ya mwisho  tumepata washindi 14 wa pikipiki hizi za miguu mitatu za mizigo" alisema Prosper.

Naye mshindi wa pikipiki hiyo, Magali, akizungumza na waandishi wa habari, amewataka Watanzania kuweka akiba Benki ya NMB, kwani pamoja na kupata zawadi ya fedha taslimu ama pikipiki ya miguu mitatu kupitia Kampeni ya Bonge la Mpango, pia fedha zao zinakuwa salama.

MWISHO.