WANAWAKE 35,763 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA AWALI WA SARATANI LA MLANGO WA KIZAZI MIKOA SITA INAYOFADHILIWA NA SHIRIKA LA AGPAHI

April 29, 2018

Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon wakati akielezea kuhusu utekelezaji wa shughuli za kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Tanga katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakinamama.

Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji mara baada ya kuelezea utekelezaji wa shughuli za kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Tanga katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakinamama kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon katika mwenye miwani akifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo
Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon kulia akiteta jambo na Dkt Hamisi mara baada ya kumalizika uzinduzi huo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya uzinduzi huo wa tatu kutoka kushoto nyuma mwenye miwani ni Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon

WANAWAKE 35,763 wamefanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi kwenye mikoa sita nchini inayofadhiliwa na shirika la AGPAHI  kwa njia ya Visual Inspection with Acetic (VIA) kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka 2017 hadi Machi mwaka 2018.

Hayo yalibainishwa  na Mratibu wa Shirika la AGPAHI Mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon wakati akielezea kuhusu utekelezaji wa shughuli za kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Tanga katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakinamama ambapo mikoa hiyo sita ni mkoa wa Tanga,Mwanza ,.Mara,Geita ,Shinyanga na Simiyu.
Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwenye kituo cha Afya Ngamini Jijini Tanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya ambapo alisema kati yao wanawake 16561 sawa na asilimia 46.5 wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi

Alisema kati ya wote waliofanyiwa uchunguzi kwa njia ya VIA,2154 sawa na asilimia 6 walikutwa na dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi huku 150 sawa na asilimia 0.4 walikutwa na eneo kubwa kwenye mlango wa kizazi lenye dalili za kansa hiyo .

Aidha alisema pia wengine 534 ambao ni sawa na asilimia 1.4 walishukiwa kuwa na kansa hiyo ambapo huduma za matibabu na rufaa zilitolewa kwa watu hao kwa kuzingatia mwongozo husika.

Alieleza kuwa mojawapo ya kazi ambazo shirika la Agpahi limefanikisha kwa kushirikiana na mkoa, halmashauri katika kufikia ufanisi wa huduma za kinga ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kutoa vifaa tiba kwenye halmashauri zote zenye vituo 54 vinavyotoa huduma hizo.

Mratibu huyo alisema kwa mkoa wa Tanga katika halmashauri ya Jiji mwezi Aprili shirika hilo limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya fedha za kitanzania milioni 50,934,200.00 ambapo baadhi hya vifaa hivyo ni pamoja na Autoclave Steam Sterilizer,Metal Punch Biopsy Machine,Medical Trolley,Kidney Dishes na Privacy Screen.

Alisema pia shirika hilo limeendelea kuwajengea uwezo watumishi wanaotoa huduma za afya kupitia ufadhili mafunzo (Training na Mentorship) ambapo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 wamewapatia mafunzo watumishi 90.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »