Kushoto Dkt. Emmanuel Sweke, Kaimu
Mkurugenzi wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)
Kigoma akimuonyesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega
katikati, kizimba cha kufugia samaki kilichopo katika maji ya ziwa
Tanganyika hakipo pichani, alipotembelea kituo hicho mjini kigoma jana.
Kulia ni Afisa Mifugo wa Mkoa Bw. Noel Byamungu.
Aliyesimama ni Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, akiongea na watumishi wa kituo cha
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, pamoja na
watafiti hawapo pichani, alipotembelea kituo hicho, kulia ni Dkt
Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, na kushoto ni
Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo katika chuo cha mafunzo ya uvuvi FETA
Kigoma, Bw. Simtie Ambakisye, Naibu Waziri Ulega alifanya ziara katika
kituo cha TAFIRI Kigoma pamoja na kutembelea mialo ya Muyobozi na
Kibiri.
Kulia Dkt. Emmanuel Sweke Kaimu
Mkurugenzi wa kituo wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania
(TAFIRI) Kigoma, akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdalah Ulega aliyekaa katikati wakiwa katika boat wakielekea
kuangalia kizimba cha kufugia samaki katika maji ya ziwa Tanganyika,
kushoto ni Afisa Mifugo wa Mkoa wa Kigoma Bw. Noel Byamungu.
……………….
KIGOMA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Abdalah Ulega, amesema kuwa siku za wanaoagiza nyama, maziwa na
samaki kutoka nje ya nchi, zinahesabika kutokana na nchi kuwa na mifigo
ya kutosha kama vile Ngombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku na Punda na hivyo Taifa
kama Tanzania halina sababu yoyote ya kuagiza mazao hayo ya mifugo na
uvuvi kutoka nje ya nchi.
Naibu waziri Ulega aliyasema hayo
alipokuwa katika ziara ya siku tatu Mkoani Kigoma ya kutembelea Mwalo wa
Samaki wa Muyobozi Uliyopo Wilayani Uvinza,Mwalo wa Kibirizi na kituo
cha Taasisi ya Tafiti za Uvuvi Tanzania TAFIRI Kigoma.
“Sioni kwanini tuagize nyama na
maziwa toka nje ya nchi, hatuwezi kuendelea kuangiza nyama, maziwa na
hata mazao ya uvuvi, kwa nini tusiwekeze katika rasilimali zetu za ndani
katika mifugo na samaki na kuongeza pato la taifa? “Aliuliza Ulega.
Ulega aliongeza kwa kusema kuwa
Wizara yake haitawavumilia waafanyabiashara wanaoagiza nyama, maziwa na
mazao ya samaki toka nje ya nchi kwani sekya ya mifugo na uvuvi ni
sekta ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija katika taifa.
Tarkibani “tani elfu 20 za samaki
zinaingizwa kutoka nje ya nchi kila mwaka, samaki ambao wanafugwa katika
maeneo mengine duniani, lakini sisi hapa nchini tunao katika mazingira
ya asili.” Alisema
Na hapa Mhe. Ulega aliitaka TAFIRI
kuhakikisha wanawafikia wafugaji wa samaki kwa kufanya tafiti zao ili
kujua changamoto wanazokutana nazo na kujua namna ya kuzitatua, akitolea
mfano wa chakula sahihi kinachotakiwa kupewa masamki wanaofugwa na
kuangalia miundombinu ya kufugia.
Akizungumzia suala la zana za
uvuvi katika ziwa Tanganyika alipokuwa akiongea na watafiti na watumishi
wa TAFIRI, Ulega alisema “TAFIRI mfanye tafiti ya aina ya nyavu
zinazotumiwa kwa kiasi kikubwa na wavuvi ili kuona kama zinafaa
kuendelea kutumika, maana kumekuwa na malalamiko toka kwa wavuvi
yanayopelekea kushuka kwa kiwango cha upatikanaji wa samaki na dagaa
katika ziwa hili kutokana na matumizi ya nyavu hizo.” Alisema
Sambamba na hilo Ulega alisema
Wizara yake ina mpango wa kuimarisha eneo la tafiti kwa kuongeza
rasilimali fedha kwa kukarabati miundombinu na kuongeza rasilimali watu.
“Kila Mwaka TAFIRI itakuwa
inafanya tafiti kuhusu mambo ambayo Wizara itakuwa imeyaelekeza ili
kuondokana na suala la watafiti hawa kufanya kazi za watu wengine.”
Alisema
Akizungumzia swala la mafanikio ya
soko la nyama la nje ya nchi, Ulega alisema, “Hatuwezi kusafirisha
nyama nje ya nchi kama mkakati wetu wa chanjo ya mifugo hauko sawa,
lazima tuwe na mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo, soko la
kimataifa linaangalia sana swala hili, Sisi kama Wizara tunaenda kusema
kuwa kwa yoyote anayetaka kufuga swala la chanjo ni lazima.” Alisisiza
Ulega.
Ulega aliendelea kusema kuwa ni
lazima wizara kutengeneza mikakati ambayo itamfanya mfugaji asitaabike
wazo wambalo amesema kama litaridhiwa litafanyiwa kazi.
“kuna watu wanaona mifugo ni balaa, mifugo siyo balaa mifugo na neema.” Alisisitiza.
Aidha Ulega alisisitiza suala la
uwekezaji kwa ufugaji wa samaki kama njia ya kusaidia kupunguza kiwango
kikubwa cha uvuvi haramu wa samaki katika maeneo mbalimbali nchini, huku
akipongeza jitihada za taasisi ya utafiti wa samaki TAFIRI kushirikiana
na wananchi na kuonesha mfano wa namna ya ufugaji bora wa samaki
unaowaonesha wafugaji wa samaki kuitumia ili kufikia malengo
waliyokusudia.
Naibu Waziri Ulega pia alisema
Serikali imepanga kuongeza makusanyo katika sekta ya mifugo kutoka
bilioni kumi na sita hadi bilioni hamsini baada ya kuifanya mifugo ya
ndani kuwa bora na kuwa ya kiushindani katika soko la kimataifa, hivyo
suala la chanjo litakuwa la lazima.