Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega kushoto
akizungumza na mfanyabiashara wa samaki aliyejulikana kwa jina la Bw. Ntakokola
Issa katika Mwalo wa Kibirizi Mjini Kigoma kuhusu usafi wa vifaa maalum na gari
la kubebea samaki, gari no T389 AZY linalotumiwa na Mfanyabiashara huyo
lilipokuwa linaonekana katika hali ya
uchafu, Naibu Waziri Ulega alikagua Mwalo wa Kibirizi uliyopo Mjini Kigoma leo
baada ya kumaliza Ziara yake wilayani Uvinza.
Katika Picha ni chaga za kisasaa za kukaushia dagaa katika
mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo
ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga
hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega na Ujumbe
wake wakitoka kukagua gati katika mwalwo wa Muyobozi uliyopo Wilayani uvinza
katika kijiji cha Mwakizega ambapo Naibu Waziri Ulega alifanya ziara leo.
Katika Picha katikati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdalah Ulega akipata maelezo kuhusu Mwalo wa Muyowozi toka kwa Afisa Uvuvi wa
Wilaya ya uvinza Bw. Haroon Chande, wakati wa ziara yake mwalono hapo leo.
Pichani wavuvi wakiteketeza wao wenyewe nyavu haramu
zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa
Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega
alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza leo. (Habari na Picha
na Mwandishi Maalum)
NA; MWANDISHI MAALUM –
UVINZA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega
ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya
kupambana na uvuvi haramu na kutatua kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na
wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi za mifugo.
Ulega ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo
wa Muyobosi uliyopo Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya
zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na
serikali kwa ujumla, kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya
wafugaji.
“Nataka niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari
kuhamia hapa kulisimamia jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka
tayari wafugaji katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa matatizo ya wakulima na wafugaji katika nchi
yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana kabisa, hicho ni kipaumbele chetu
mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika uongozi wetu tutahakikisha kama
siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji basi tutaindoa kabisa, kwa
kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema Ulega.
Ulega alisisitiza
suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za uvuvi na
suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na utamaduni wa
kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Naibu Waziri Ulega
alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa Muyobozi na kuwataka
wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye hadhi ya kimataifa
ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke yake umechangia
kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia vyema mahala hapa
patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi ndo muwe walinzi
wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka” Alisisitiza
Awali, akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha
Mwakizega ambapo mwalo wa Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema
mwalo huo unakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo
huo kuwa na urefu wa mia 20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na
kupakia kabla na baadha ya shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza
urefu wa gati hiyo ili mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za
uvuvi vizuri.
Bw. Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na
changamoto ya kukosa elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa
katika sekta ys uvuvi.