Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini
ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi
Kigwangalla mapema leo ametembelea nyumbani kwa familia ya Akwilina na
kutoa ubani wa pole kwa msiba huo.
"Nimefika
hapa kama Raia mwema tu ambaye nimeguswa na msiba huu na nimetafakari
kwani na mimi kipindi fulani nilipitia chuo hasa kutoka familia zetu
hizi masikini kwa hiyo inapotokea ukio kama ili unaona ni pigo kwa
familia, pigo kwa jamii, pigo kwa wanafunzi wenzake na pigo kwa Taifa
kwa ujumla wake" alieleza Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na vyombo
vya Habari msibani hapo.
Dkt.Kigwanalla
ambaye alifika msibani hapo majira ya saa saba mchana, aliweza kuungana
pamoja na ndugu na jamaa wa wafiwa ambapo pia alipata chakula cha
mchana pamoja na waombolezaji wengine sambamba na kutoa ubani wake kama
mwananchi mwingine.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli ambaye yupo hapo kwa
ajili ya kusimamia shughuli kwa upande wa Serikali, amebainisha kuwa
wataendelea kuratibu baadhi ya mambo yanayoendelea hapo kwani msiba huo
kwa namna moja Serikali imeguswa nao.
Mbali
na Mkuu wa Wilaya hiyo, Wengine waliofika hapo ni pamoja na Mkurugenzi
wa Ubungo, John Kayombo ambapo kwa pamoja na watendaji wengine wa
Kiserikali wameweza kusaidiana na familia ya marehemu katika shughuli
mbalimbali zinazoendelea msibani hapo.
Aidha,
jana viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri Elimu, Mh.
Ndalichako, Naibu Waziri wa Ulinzi Masauni na IGP Siro waliweza
kutembelea kutoa pole katika familia hiyo.
Akwilina
kabla ya kifo chake alikuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16
mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa
wakizuia maandamano ya chama cha siasa cha CHADEMA.
Marehemu Akwilina enzi za uhai wake
Mbunge
wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa familia
ya Akwilina alipotembelea hapo kutoa pole
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akipata taarifa kutoka kwa ndugu Akwilina amabye alikuwa ni mlezi wa binti huyo.
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakipata chakula cha mchana msibani hapo
Viongozi wa Serikali wakipata chakula msibani hapo
Mbunge
wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya ndugu na jamaa
walijitokeza katika msiba huo, Mbezi Luis, Jijini Dar e Salaam
Mbunge
wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati
wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo
Mbunge
wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati
wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo.
--
Andrew Chale
Blogger
Personality | Journalist | Activist | CEO & Online Editor BONGONEWS
| Comedian |Volunteer Red Cross | Sauti za Busara & ZIFF Festivals
2007 to present.
Email: andrewchale@gmail.com
Telephone: +255767076376
Golden Jubilee Towers, Ohio Street, 6th Floor
Po Box Dar es Salaam,Tanzania