Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
MKUU
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wachezaji wa
Gofu wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha heshma ya jeshi
kwa kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora
wanaowakilisha nchi kimataifa.
Aliyasema
hayo Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es Salaam wakati akiagana
na wachezaji Sita wa Gofu wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano
ya wazi ya wanawake nchini Nigeria IBB Ladies Open Championship 2018
yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Jenerali
Mabeyo amesema kama ilivyokuwa katika michezo ya iiadha na ngumi sasa
tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu hii ya Gofu ya Wanawake
kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.
“
Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema na Jeshi kwa ujumla
tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji wa Gofu na hata Michezo mingine
kuhakikisha jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa
chachu kwa wengine,” alisema Jenerali Mabeyo.
Ameongeza
licha ya matumaini yake katika Gofu lakini pia katika Soka licha ya
mchezo huo kutawaliwa na Simba na Yanga lakini sasa walau mwanga
unaonekana baada ya ya Timu ya Jeshi ya Green Worriorrs kuifurusha Timu
ya Simba katika Michuano ya Kombe la Shirirkisho.
“Ushindi
ule ulikuwa Mwanzo mzuri wa kupunguza Ubabe wa Simba na Yanga na
Ushabiki wa Simba na Yanga hata miongoni mwa wachezaji hivyo nanyi kama
mlivyofanya vyema katika mashindano Uganda sasa tunatarajia Ushindi toka
Nigeria,"amesema Jenerali Mabeyo.
Kwa
Upande wa mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo
Mstaafu amewataja wachezaji hao kuwa ni Nahodha Ayne Magombe, Sara Denis
, Sophia Mathius ,Hawa Wanyenche ,Christina Charles na Angel Eaton
huku mkuu wa Msafara akiwa ni Kapten Japhet Masai.
“
Nina matumaini makubwa na Kikosi hiki tunachokituma Nigeria naamini
kitarejesha furaha kwa Klabu ,jeshi na Watanzania kwa ujumla ukizingatia
uwezo Binafsi wa Wachezaji Mazoezi na Historia kutokana na michuano
iliyotangulia” amsema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.
Kwa
Upande wake mwenyekiti wa Chama cha Gofu nchini TGU Joseph tango
amelipongeza jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa jitihada katika
kuendeleza michezo hasa mchezo wa gofu ambao klabu ya Lugalo imekuwa
kielelezo.
Amemuomba
mkuu wa majeshi ya ulinzi na Mlezi wa Klabu ya Lugalo kuendelea
kuisaidia Klabu hiyo ambayo ndio klabu yenye mashindano mengi kwa mwaka
ukilinganisha na Klabu nyingine nchini ikiwemo kusaidia utekelezaji wa
Ujenzi wa Uwanja makao makuu ya nchi Dodoma.
Mashindano
hayo yanayotarajiwa kuanza February 8 na kuchukua siku tatu
yanatarajiwa kushirikisha nchi mbali mbali za Afrika ikiwamo
Kenya,Uganda na Zambia.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Bendera ya taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi l Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni ( Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
Selemani Semunyu).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika Picha ya Pamoja na Wachezaji na Viongozi wa Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Wakuu wa Matawi na Wachezaji wanaotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini
Nigeria hivi karibuni.
Nigeria hivi karibuni.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Afisa habari wa Klabu ya Gofu ya Jeshi ya Lugalo Luteni selemani Semunyu (Kulia) mara baada ya kukabidhi Bendera kwa Nahodha wa Timu ya Wanawake
ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini
Nigeria Hivi karibuni.
ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini
Nigeria Hivi karibuni.