Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAZIRI
wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama
kutenda Haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha
Haki kutendeka.
Pia
ameitaka kutoa fidia ipasayo, kukuza usuluhishi ipasavyo, kukuza
usuluhishi baina ya watu husika katika migogoro na watoe haki bila
kujali sababu za hali ya mtu kijamii ama kiuchumi
Waziri
Kabudi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho
ya Wiki ya Sheria ambayo kilele chake kinatarajiwa kufanyika kesho
katika Viwanja vya Mahakama vya Chimala jijini. Kauli mbiu katika siku
ya sheria mwaka huu inasema, Matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa
wakati na kuzingatia maadili.
Waziri
Kabudi pia ameitaka Mahakama ipunguze kuchelewesha kesi bila sababu za
msingi na iongeze kasi ya usikilizwaji wa Mashauri kwa
Ameongeza
Wizara inathamini maonesho ya siku ya sheria na maendeleo yanayofanywa
na Mahakama katika kuendeleza kuboresha mfumo wa sheria na kwamba
Mahakama imekuwa ya kwanza kubadilika katika sekta ya sheria. Hivyo
Wizara itahakikisha maboresho ya mahakama yanafanikiwa.
Kabla ya ufungaji wa maonesho hayo, Waziri Kabudi pia amezindua Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni.
Akizindua
jengo hilo la Mahakama lililogarimu zaidi ya Sh.milioni 500
Prof.Kabudi amesema, mkakati wa Mahakama hadi kufikia mwaka jana
walikuwa wanahitaji Mahakama Kuu 19, Mahakama za Hakimu Mkazi 14,
Mahakama za Wilaya 109, Mahakama za Mwanzo 3003 huku wakiwa na uhitaji
mkubwa wa ukarabati wa mahakama nyingi nchini.
Aliipongeza
Mahakama kwa ubunifu, umakini na ufanisi waliouonesha kwa kufanya
utafiti wa kutumia Moladi na ujenzi bora, imara na wenye gharama nafuu.
Prof. Kabudi pia ameipongeza mahakama kwa kujenga majengo hayo katika
wilaya mpya, hasa Kigamboni na amewataka kutafuta viwanja zaidi ili
jitihada za kuongeza mahakama Kigamboni zifanyike kwa kuwa ipo moja tu.
Pia
ameshauri wananchi wa Kigamboni kuhakikisha wanajaribu kutafuta
usuluhishi nje ya Mahakama kwa matatizo yanayowezekana na ikishindikana
ndiyo wapeleke mahakamani.
"Serikali
imekuwa ikiongeza bajeti ya Mahakama kila mwaka ili kuboresha
huduma...nitoe rai kwa watumishi na watumiaji mtunze miundombinu,
serikali imetumia fedha gharama nyingi muilinde na kuitunza,"amesema.
Amebainisha
mfumo wa Mahakama wa Tehama utapunguza gharama kwa kuwa utasaidia kesi
kuendeshwa wakati shahidi akiwa eneo lingine na hata mtu kutumia simu ya
kiganjani kupata taarifa za mahakama, kufungua kesi ama kulipa.
Kwa
upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omary Othmani Makungu amefurahi
nakuahidi kutumia elimu aliyoipata ili kujenga jengo kama hilo kwa
gharama nafuu kwani wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika ujenzi wa
mahakama Zanzibar.
Katika
Wiki hii ya Sheria Mahakama amezindua majengo mapya katika mahakama za
Bagamoyo, Kawe, Mkuranga, Kigamboni na Kituo cha Mafunzo Kisutu.
Waziri
wa katiba na Sheria, Profesa Pamalagamba Kabudi akizungumza na wananchi
pamoja na watumishi wa Mahakama wakati wa uzinduzi mahakama ya mwanzo
na Wilaya ya Kigamboni, kulia kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu
Tanzania, Ferdnandi Wambari na kulia kwake ni Jaji Mkuu Kuu Zanzibar
Omary, Othaman Makungu.
Waziri
wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akipanda mti katika
jengo jipya la mahakam ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, baada ya
kumaliza kuzindua mahakama hiyo mpya.
Waziri
wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akiwa katika Picha ya
pamoja na baadhi ya Watumishi wa mahakama nchini Tanzania na Zanzibar