Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Simon Msanjila akikabidhi
zawadi kwa Prosper Gasper na Erick Simon kutoka Shule ya Sekondari St.
Jude's jijini Arusha baada ya kuibuka washindi wa jumla wa Mashindano ya
Wanasayansi Chipukizi (YST) yaliyofanyika leo yaliyofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar
es Salaam.
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
SHULE
za Sekondari nchini Tanzania zimetakiwa kuanza kutuma maombi sasa ili
kupata fursa ya kushiriki katika Maonyesho ya 8 ya Sayansi kwa wanafunzi
yanayoandaliwa na Shirika la Young Scientists Tanzania (YST) kila mwaka.
Taarifa
kutoka YST zimeeleza kwamba, maonyesho hayo ni kwa wanafunzi wa kuanzia
kidato za kwanza hadi cha sita kwa shule zote za sekondari – za umma na
binafsi – zilizoko nchini.
“Mwisho
wa kutuma maombi ni Machi 31, 2018 na maonyesho hayo yatafanyika jijini
Dar es Salaam mwezi Agosti,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa
hiyo imeeleza kwamba, kutuma mapema maombi kutasaidia hata zoezi la
mchujo ili kuwapata washiriki wenye mawazo yatakayoleta ushindani pamoja
na ubunifu kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini Tanzania.
Jumla
ya mawazo 100 yanatarajiwa kushindanishwa mwaka huu ambapo washindi
katika vitengo mbalimbali watapatiwa zawadi za fedha pamoja na ufadhili
wa masomo ya chuo kikuu.
MaendeleoVijijini inafahamu
kwamba, wanafunzi Prosper Gasper na Erick Simon wa shule ya Sekondari
ya St. Jude’s kutoka Arusha, ndio walioibuka mabingwa wa jumla wa
sayansi katika Maonyesho ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania 2017 kutokana na wazo lao la “Kutumia Simu za Mkononi kama Mfumo wa Kubaini Ajali za Moto” (The Use of Mobile Network as a Fire Alert System).
Kwa
ushindi huo, mbali ya kutunukiwa medali na tuzo, pia walipata kitita
cha Shs. 1,800,000 pamoja na udhamini wa masomo yao hadi elimu ya juu.
Aidha,
walipata nafasi kwa mara ya kwanza ya kushiriki mashindano ya ubunifu
wa sayansi na teknolojia yaliyofanyika jijini Johannesburg, Afrika
Kusini mwezi Oktoba 2017 na mwaka huu 2018 watashiriki maonyesho ya
kimataifa ya sayansi na teknolojia jijini Dublin, Ireland.
Kumekuwepo
na ongezeko kubwa la ushiriki wa shule za sekondari kutoka shule 4
mwaka 2011 hadi 100, hatua ambayo imetokana na hamasa ya kuendeleza
masomo ya sayansi kwa shule mbalimbali za sekondari nchini.
MaendeleoVijijini inafahamu
kwamba, uwepo wa maonyesho hayo ya sayansi kwa wanafunzi usaidia ufaulu
wa masomo ya sayansi kwa shule nyingi za sekondari nchini, mfano
mmojawapo ukiwa ni Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara.
Katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017,
kwa mara ya kwanza shule hiyo ilipata daraja kwa kwanza (Division One)
kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi, jambo ambalo lilikuwa adimu.
Uchunguzi wa MaendeleoVijijini umebaini
kwamba, kwa miaka takriban 10 mchepuo wa masomo ya sayansi, Kemia,
Baolojia na Jiografia (CBG), haujawahi kutoa hata mwanafunzi mmoja
aliyepata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha sita.
MaendeleoVijijini imegundua
kwamba, miaka yote ufaulu mkubwa wa masomo ya sayansi shuleni hapo
umekuwa daraja la pili (division two) ambao nao haukuwa wa kuridhisha
ikilinganishwa na masomo ya sanaa na uchumi, huku wanaochukua mchepuo wa
sayansi ‘wakiongoza’ kwa kupata daraja la nne pamoja na kupata sufuri.
Kati
ya wanafunzi nane waliopata Daraja la Kwanza mwaka 2017 shuleni hapo,
wawili walikuwa wanachukua mchepuo wa sayansi na kati ya wanafunzi 57
waliopata daraja la pili, 17 wanatoka mchepuo wa sayansi pia.
Wanafunzi wawili waliopata daraja la pili shuleni hapo Diana Sosoka na Nadhra Mresa, ambao walikuwa washindi wa jumla mwaka 2016 katika maonyesho hayo ya sayansi ya YST nao walionyesha kushangazwa na matokeo hayo.
“Kweli
ni maajabu kwa mara ya kwanza kuna Division One kwenye CBG pale shuleni
kwetu, ni mafanikio ambayo yametokana na hamasa ya kuwepo kwa
mashindano haya ya sayansi na sisi tunashukuru kuwa sehemu ya
mafanikio,” anasema Diana.
Diana
na Nadhra ambao walipata ushindi kwa kubuni mashine ya kienyeji ya
kutotoresha mayai, pia walipata udhamini wa masomo ya chuo kikuu kutoka
taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.
Wote
kwa pamoja walikuwa wanachukua mchepuo wa Kemia, Baolojia na Jiographia
(CBG) na kwa bahati nzuri, wote wawili wamepata Division Two ya alama
12.
Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.
|
Uncategories
FURSA NYINGINE YA SCHOLARSHIP YAJA: SHULE ZA SEKONDARI ZATAKIWA KUTUMA MAOMBI SASA KUSHIRIKI MAONYESHO YA SAYANSI YA YST 2018!
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »