WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AHIMIZA MAHAKAMA KUTENDA HAKI

January 31, 2018
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama kutenda Haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha Haki kutendeka.

Pia ameitaka kutoa fidia ipasayo, kukuza usuluhishi ipasavyo, kukuza usuluhishi baina ya watu husika katika migogoro  na watoe haki bila kujali sababu za hali ya mtu kijamii ama kiuchumi

Waziri Kabudi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Sheria ambayo kilele chake kinatarajiwa kufanyika kesho katika Viwanja vya Mahakama vya Chimala jijini. Kauli mbiu katika siku ya sheria mwaka huu inasema, Matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa wakati na kuzingatia maadili.

Waziri Kabudi pia ameitaka Mahakama ipunguze kuchelewesha kesi bila sababu za msingi na iongeze kasi ya usikilizwaji wa Mashauri kwa 

Ameongeza Wizara inathamini maonesho ya siku ya sheria na maendeleo yanayofanywa na Mahakama katika kuendeleza kuboresha mfumo wa sheria na kwamba Mahakama imekuwa ya kwanza kubadilika katika sekta ya sheria. Hivyo Wizara itahakikisha maboresho ya mahakama yanafanikiwa.

Kabla ya ufungaji wa maonesho hayo, Waziri Kabudi pia amezindua  Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni.

Akizindua jengo hilo la Mahakama lililogarimu zaidi ya Sh.milioni 500  Prof.Kabudi amesema, mkakati wa Mahakama hadi kufikia mwaka jana walikuwa wanahitaji  Mahakama Kuu 19, Mahakama za Hakimu  Mkazi 14, Mahakama za Wilaya 109, Mahakama za Mwanzo 3003 huku wakiwa na uhitaji mkubwa wa ukarabati wa mahakama nyingi nchini. 

Aliipongeza Mahakama kwa ubunifu, umakini na ufanisi waliouonesha kwa kufanya utafiti wa kutumia Moladi na ujenzi bora, imara na wenye gharama nafuu. Prof. Kabudi pia ameipongeza mahakama kwa kujenga majengo hayo katika wilaya mpya, hasa Kigamboni na amewataka kutafuta viwanja zaidi ili jitihada za kuongeza mahakama Kigamboni zifanyike kwa kuwa ipo moja tu.

Pia ameshauri wananchi wa Kigamboni kuhakikisha wanajaribu kutafuta usuluhishi  nje ya Mahakama kwa matatizo yanayowezekana na ikishindikana ndiyo wapeleke mahakamani. 

"Serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya Mahakama kila mwaka ili kuboresha huduma...nitoe rai kwa watumishi na watumiaji mtunze miundombinu, serikali imetumia fedha gharama nyingi muilinde na kuitunza,"amesema. 

Amebainisha mfumo wa Mahakama wa Tehama utapunguza gharama kwa kuwa utasaidia kesi kuendeshwa wakati shahidi akiwa eneo lingine na hata mtu kutumia simu ya kiganjani kupata taarifa za mahakama, kufungua kesi ama kulipa.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omary Othmani Makungu amefurahi nakuahidi kutumia elimu aliyoipata ili kujenga jengo kama hilo kwa gharama nafuu kwani wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika ujenzi wa mahakama Zanzibar.

Katika Wiki hii ya Sheria Mahakama amezindua majengo mapya katika mahakama za Bagamoyo, Kawe, Mkuranga, Kigamboni na Kituo cha Mafunzo Kisutu.
Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Pamalagamba Kabudi akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa Mahakama wakati wa uzinduzi mahakama ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, kulia kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Ferdnandi Wambari na kulia kwake ni Jaji Mkuu  Kuu Zanzibar Omary, Othaman Makungu.
 Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akipanda mti katika jengo jipya la mahakam ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, baada ya kumaliza kuzindua mahakama hiyo mpya.
Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa mahakama nchini Tanzania na Zanzibar

Balozi wa Ujerumani Tanzania ashiriki maadhimisho ya wahanga utawala wa Hitler

January 31, 2018
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter akizungumza na wanafunzi walioshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani. Kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter.

Wanafunzi hao wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Wanafunzi hao wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter pamoja na Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (mbele) pamoja na wanafunzi (nyuma) wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

BALOZI wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter ameshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, yalioshirikisha wanafunzi mbalimbali wa Shule za Sekondari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo aliwataka vijana kujitambua, kupenda kujifunza historia na pia kutokubali kutumika kuchochea vurugu katika maeneo yao.

Maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa mfumo wa 'Nazism' uliolenga kuwateketeza Wayahudi kwa kuamini si binadamu bora yalipoteza uhai wa watu takribani milioni sita wakiwemo watoto. Mfumo ambao pia ulitokomeza watu wenye ulemavu na wafupi kwa kuangamizwa kwa kutumia gesi za sumu na pamoja na moto. 

Aidha alisema baadhi ya maeneo vijana wanaweza kujikuta wanatumika katika matukio yanayochangia vurugu hivyo kuna kila sababu ya wao kupewa elimu ya kujua historia kwa undani ili wasiweze kutumika kwa namna yoyote. 

"Upo umuhimu wa vijana kutokubali kushiriki katika masuala ya ukatili, vurugu za aina yoyote ile...alisema vijana wanapaswa kujitambua na kufahamu historia na jukumu lao la kulinda amani kwa faida ya mataifa yao," 

Vijana hao kutoka shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam walipata elimu pia kutoka kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter juu ya historia ya mauaji hayo, ambapo walipata fursa za kujadili na kuuliza maswali tofauti kutoka kwa balozi huyo raia wa Ujerumani.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: DK. KIGWANGALLA AELEZA HATMA YA WAVAMIZI KATIKA HIFADHI YA BONDE LA MTO KILOMBERO

January 31, 2018

YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KINONDONI, MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA NDUGUMBI JUMANNE JANUARI 30, 2018*

YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KINONDONI, MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA NDUGUMBI JUMANNE JANUARI 30, 2018*

January 30, 2018

Image may contain: one or more people, people on stage, crowd and outdoor

Mgombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM Maulid Said Mtulia akinadi sera zake jukwaani na kuomba kura kwa wapiga kura wa Kata ya Ndugumbi.


**********

*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KINONDONI, MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA NDUGUMBI JUMANNE JANUARI 30, 2018*

"Kama Mtulia angekuwa amenunuliwa asingepewa tena dhamana ya kugombea Ubunge " - Mtulia

"Ningekaaje kwenye chama ambacho Mwenyekiti na Katibu hawaelewani, nimejitoa ili niwe na uhuru wa kuwatumikia wana Kinondoni." - Mtulia


"Kile chama hamkusikia kimesimamisha wabunge 8, mlitaka nami nisimamishwe?" - Mtulia

"Mtulia nimejiuzulu ili kuwaokoa Wananchi wa jimbo la Kinondoni" - Mtulia

"Kuhama chama ili kujiunga na chama chenye maendeleo, huo ni usaliti?" - Mtulia

"Mtulia huyu ndio aliotoa hela yake mfukoni kujenga visima vya maji; Mtulia aliyefungua kesi mahakamani kuzuia bomoa bomoa; ndio Mtulia yule aliyeomba maghorofa ya Magomeni Watu waliojitokeza nyumba zao wakae bure" - Mtulia

"Mtulia mimi ni yule yule mkinichagua nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo nikishirikiana na viongozi wenzangu na Rais wangu mpendwa Di. Magufuli " - Mtulia

"Ninaomba tena ridhaa ili nihakikishe nawaletea maendeleo wana Kinondoni kutokana na kugombea kwenye chama chenye ilani ya uchaguzi iliyoshikan dola" - Mtulia

"Naomba dhamana ya kugombea ili nikashirikiane na wenzangu kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020" - Mtulia

"Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na si porojo wala usanii" - Mtulia

"Ukichagua Mtulia umechagua maendeleo; ukimchagua Mtulia umejenga daraja kati ya Wananchi na Serikali" - Mtulia

MBUNGE KABATI ATOA MSAADA WA MIFUKO 25 YA SARUJI KATIKA KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA

January 30, 2018
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji
wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
 Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano (25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa huduma bora ya neon la mungu.

Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.

“Mimi nimejitoa kuchangia shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa aliwaahidi kuwapa mifuko ishirini na tano ya saruji hivyo ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapa mifuko ya saruji yote aliyoiadi hivyo amefanikiwa kutekeleza na kuwaomba wananchi wananchi wengine kuchangia maendeleo ya kanisani.

“Alikuja diwani hapa kwa niaba yangu na kuahidi mifuko hiyo ambayo ni sawa na tani moja hivyo nimeamua kutimiza kuwa lengo langu nikiahidi kitu lazima nitimize malengo yangu ya kuitoa ahadi hiyo” alisema Kabati

Aidha Kabati aliwata wananchi na viongozi mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa jamii na taasisi ambazo hazina uwezo wa kufikia mafanikio yanayotakiwa kwa ajili ya kutatua kero zinazorudisha nyuma maendeleo.

Kabati amesema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kumtegemea mungu ili kuweza kufanikisha malengo wanayotarajia.

Katika hatua nyingine Kabati amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili wakapate elimu ambayo ndiyo itakuwa dira ya maisha yao ya baadae.

Kwa uoande wake mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero alisema kuwa walikuja viongozi wengi na kutoa ahadi nyingi lakini hakuna hata mmoja aliyetimiza ahadi yake zaidi ya mbunge Ritta Kabati.

"Nilialika wageni wengi wakala na kutoa ahadi nyingi kwa mbwembwe nyingi lakini kilichotokea hadi sana viongozi wote hakuna aliyetimiza malengo hayo hivyo nichukue furasa kushukuru" alisema Okero

Mchungaji Okero alimshukuru mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itatusaidia katika ujenzi wa kanisa letu

KATIBU MKUU WA MIFUGO KUKABIDHI RASMI TAARIFA YA CHAPA YA MIFUGO LEO KWA WAZIRI MPINA

January 30, 2018


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na  wafugaji  kuhusu upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta)


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo(mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji  kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.  (Picha na Ngailo Ndatta)
Dereva  wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.  (Picha na Ngailo Ndatta)
Na John Mapepele, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba  timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi  baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.
“Wakuu Wote wa Idara,Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa ” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.
Aidha amezitaka  Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote  katika muda wa nyongeza uliotolewa na Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.
Akizungumza katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga  chapa  mifugo ambayo inatoka nje ya nchi  ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali.
Aidha, Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio raia wa Tanzania  waliyoingia  katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika  vyombo vya sheria.
Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema awali  inakadiliwa kwamba  30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo  toka nje ya nchi.
Ameutaka Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza ushirikiano  na kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana  aliongeza siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji chapa mifugo huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo kikamilifu na  wengine wawili wakipewa onyo kali.
Alida kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi  ya changamoto zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo Halimashauri  ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.
Siku kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma, kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa  Desemba 31 Mwaka jana .
Aidha alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.