Wanafunzi
wa shule za sekondari manispaa ya iringa kunufaika na elimu ya masomo ya
sayansi kutokana na kuandaliwa kambi maalumu kwa ajili ya kuwafindisha kutoka
kwa walimu waliobobea katika masomo hayo kwa wanafunzi wa watakao kuwa tayari
kupata elimu hiyo.
Ofisi
ya mbunge wa viti maalum Ritta Kabati imeandaa mpango wa kuwaongezea elimua
wanafunzi wa shule za sekondari manispaa ya Iringa kwa kuanzisha kambi ya
masomo ya sanyasi itakayo kuwa inafanyika bure kwa wanafunzi wa watakao kuwa
tayari kupata elimu hiyo.
Akizungumza
na Nuru fm Dicksoni Kawovela ambaye ni mratibu wa miradi ya jamii kutoka ofisi
ya mbunge RITTA KABATI amesema kuwa wameamua kuja na mpango huo kwa lengo la
kuinua elimu ya sayansi kwa wanafunzzi wa shule za sekondari hapa manispaa.
Aidha
Kawovela amesema kuwa mafunzo hayo yatakuwa na manufaa kwa walimu na wanafunzi
watakaokuwa wanahudhuria masomo haya ambayo yatakuwa yanatolewa bure.
Kawovela
amewaka wazazi wa wanafunzi kuwaruhusu watoto wao kwenda kwenye makambi hayo
ili waongezewe uwezo katika masomo ya sayansi.
Hata
hiyo Kawovela alisema kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa mama Salma
Kikwete ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania