![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgAqsjEofnAS49Px3ZTET4iPbJJnpRkKrBzVwktfb9Nz8eQTtGai66kvGi08mj0KjUeIsGsErDw8rGabx3gxpOXSLnx9FiToN2bwGwQLUIAtgTknmxndm1yQ9Bz_J4ptr_-kX4SnmPia729/s640/1.jpg)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika katika Ukumbi wa White House mjini
Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais wa Zanzibar
Dkt. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bara Philip Mangula
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana akizungumza katika
kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika
katika Ukumbi wa White House mjini Dodoma.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiimba mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi (White House) mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu
Dkt. Salim Ahmed Salim akiwaaga wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi
(CC) mara baada ya kumaliza muda wake.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye amemaliza muda wake Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim. Picha na IKULU