WAMBURA AWATIA SHIME WAKUFUNZI WA WAAMUZI
Makamu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Wambura
amesema, kuna uwezekano mkubwa Bara la Afrika, likatoa idadi kubwa ya
waamuzi katika fainali za michuano mikubwa hususani Kombe la Dunia.
Wambura
alisema hayo Jumatatu Novemba 20, 2017 kwenye Ukumbi wa ILO, Dar es
Salaam wakati aifungua kozi Wakufunzi wa Waamuzi kutoka sehemu
mbalimbali barani Afrika.
Kozi
ya wiki moja ya Wakufunzi wa waamuzi hatua ya tatu ‘Futuro III’
inayofanyika Tanzania kwa nchi 26 kushiriki. Jumla ya Washiriki 58
wanashiriki kozi hiyo kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania.
Kozi
hiyo ina wakufunzi sita wakiwamo Carlos Henriques na Dominic Chiellens
wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), ambao Wambura
aliwataka wakufunzi wanaofundishwa mbinu mbalimbali kufanya kazi kwa
weledi ili kutimiza ndoto hiyo ya Afrika.
“Waamuzi
wa Afrika wana uwezo. Ninyi wakufunzi ni wa kufanya waamuzi wetu kuwa
na uwezo zaidi. Ni Aibu kwa Bara kubwa kama Afrika lenye nchi wanachama
54 wa FIFA kuwa na waamuzi wachache katika fainali za Kombe la Dunia.
“Tuazimie
kuwa na waamuzi wa kutosha katika fainali kubwa kama hizo,” Amesema
Wambura ambaye alipigiwa makofu na washiriki kwa kuwatia shime
wakufunzi.
GRASSROOTS YAFANYIKA KWA MAFANIKIO LINDI
Kozi
ya makocha wa mpango wa Grass Roots unaolenga wachezaji mpira wa miguu
(wasichana na wavulana) wenye umri kati ya miaka 6-12, imefanyika kwa
mafanikio mkoani Lindi.
Kozi
hiyo ilifungwa rasmi Jumapili Novemba 19, 2017 na Mkuu wa Wilaya ya
Lindi Shaibu Ndemanga katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Ilulu mkoani
Lindi.
Akifunga
kozi hiyo iliyoshirikisha walimu 30 wa shule za msingi kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi, Mkuu wa
Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amewakumbusha kuwa elimu waliyoipata
waitumie kama chachu ya kukuza soka la Tanzania,
"Mkoa
wa Lindi umepata bahati kubwa sana kupata elimu hii kwani awali tulijua
ni kwa ajili ya Mkoa wa Dar ila kumbe hata sisi huku Lindi Vijijini
tunatambuliwa na TFF, Nitatoa ushirikiano kwa waalimu wote 30 waliopata
mafunzo ili tuweze kukuza soka letu hasa Wilaya yetu ya Lindi,”
amesema.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi amewapongeza
washiriki wote waliopata kozi hiyo huku akiwahasa kutumia elimu
waliyoipata kufundishia michezo mashuleni.
"Waalimu
sina shaka na nyie, nyie ni bado vijana natambua elimu mliyoipata
itaufanya mkoa wa lindi kupata vijana wengi wakiume na wakike ambao
watapata elimu ya soka kutoka kwenu, ikumbukwe dhumuni la TFF ni kutoa
elimu kwenu ili nyie mkaitumie kwa vijana mashuleni,” amesema.
Madadi
amewataka washiriki kuitumia vizuri nafasi hiyo waliyoipata kwa kwenda
kuwafundisha na kuupenda mpira wa miguu watoto wadogo wenye umri kati ya
miaka 6-12.
Ikumbukwe
kozi hii ya Grass Roots kwa mwaka huu imefanyika mara mbili ambapo
mwezi Septemba na Oktoba zilifanyika Dar kwenye Ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania kwa kushirikisha waalimu wa shule za msingi na
Sekondari kutoka mkoa wa Dar es Saalam.
SIRI YA NINJE KILIMANJARO STARS
Kocha
Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’,
Ammy Conrad Ninje, amesema kwamba ameteua kikosi hicho kwa kuzingatia
mambo makuu matatu.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Ninje alitaja kikosi cha wachezaji 20
kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji mwaka huu wa 2017 ambako
amesema: “Kwanza nataka mchezaji ambaye ana njaa ya mafanikio…
“…Sehemu
pekee ya kupata mafanikio ni pamoja na kucheza timu ya taifa. Pili,
nataka wchezaji wanaofundishika na tatu nataka wachezaji wanaokubali
kufundishika,” amesema Ninje.
Ninje
- Kocha wa Daraja ‘A’ la Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA),
alitaja kikosi hicho Jumamosi Novemba 18, 2017 kwenye Ukumbi wa Hosteli
za TFF, Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kikosi
hicho kinachotarajiwa kuingia kambini Jumapili Novemba 26, mwaka huu
jijini Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC) na Peter
Manyika (Singida United).
Walinzi
ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin
Yondani (Young Africans), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni
(Simba SC) na Mohammed Hussein (Simba SC).
Viungo
wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba
SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC),
Raphael Daud (Young Africans), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal
(Tusker/Kenya) na Ibrahim Ajib (Young Africans).
Washambuliaji
ni Mbaraka Yussuph (Azam FC), Elias Maguri (Dhofar/Mascat, Oman),
Daniel Lyanga (Fanja FC/Mascat) na Yohana Mkomola (Ngorongoro Heroes).
Benchi
la Ufundi linaundwa na yeye Ninje ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence
Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny
Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert
Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
Katika
michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro
Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo
ni timu mwalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika.
Kilimanjaro
Stars ambayo imewahi kutwaa mara tatu taji hilo la Chalenji tangu
kuanzishwa kwake, itaaza kampeni za kurudisha heshima yake dhidi ya
Libya katika kundi hilo la A utaofanyika Desemba 3, mwaka huu.

EmoticonEmoticon