Mwanza watakiwa kuchangamkia fursa Maendeleo Bank

October 17, 2017
Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza hii leo Jijini Mwanza, nje ya ukumbi wa mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo nchini TCCIA pamoja na Best Dialogue (Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania).

Binagi Media Group
Wananchi mkoani Mwanza wametakiwa kuchangamkia fursa ya ununuaji wa hisa za Maendeleo Bank ambazo zimeanza kuuzwa tangu Septemba 18 hadi Novemba 03 mwaka huu.

Mkurugenzi wa benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba ametoa rai hiyo hii leo Jijini Mwanza kwenye mafunzo ya mjadala baina ya sekta ya umma na sekta binafsi yaliyoandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA pamoja na pamoja na Best Dialogue (Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania).

Mwangalaba amesema hisa za benki hiyo zinauzwa kwa thamani ya shilingi 600 na kwamba kiwango cha chini ya ununuzi ni hisa 100 zenye thamani ya shilingi 60,000 hivyo wananchi wakiwemo wachangamkie fursa hiyo.

“Tunauza hisa katika soko la hisa na hisa hizi zinauzwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB ambapo tunaunga mkono juhudi za Rais wetu anayesema uchumi wa Tanzania umilikiwe na watanzania wenyewe na njia mojawapo ya kuwajumuisha watanzania wengi ni uuzaji wa hisa sokoni”. Amesisitiza Mwangalaba na kuongeza kwamba hisa hizo pia zinapatikana ofisi za TCCIA.

Naye Mshauri wa Hisa, Richard Manamba amesema ununuzi wa hisa una faida nyingi ikiwemo wanunuzi kupata gawio la faida ambalo benki hulipata na kwamba hisa hizo huongezeka thamani kulingana na nguvu ya soko.

Maendeleo Bank yenye mtaji wa shilingi bilioni 10 sokoni inaendelea kuongeza mtaji wake hadi kufikia shilingi bilioni 17 ambapo inatarajiwa kufungua matawi yake katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza.
Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akielezea umuhimu wa kununua hisa za benki hiyo hii leo Jijini Mwanza ambapo mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yanafanyika.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba wakati akielezea umuhimu wa kununua hisa za benki hiyo.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Elibariki Mmari akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mkurugenzi wa "Maendeleo Bank", Ibrahim Mwangalaba (kulia), wakifutahia mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mkurugenzi wa "Maendeleo Bank", Ibrahim Mwangalaba (kulia), wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Majadiliano yakiendelea
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo (wa tatu) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo (wa tatu) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »