Katika picha kikosi kazi maalum cha oparesheni ya angani ya
ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga inayotokea katika nchi
jirani ya Kenya , mbele ni rubani wa ndege hiyo maalum ya TANAPA Bw. Mark
Athumani akiongoza ujumbe huo kupanda ndege katika uwanja wa kimataifa wa ndege
wa Kilimanjaro (KIA).
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na
kikosi kazi maalum kikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Maria Mashingo
na Rubani wa ndege hiyo maalum ya TANAPA
Bw. Mark Athumani walipokuwa wakijiandaa kwenda kwenye oparesheni maalum ya
angani ya ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika wilaya ya Mwanga wanaotokea
katika Nchi jirani ya Kenya.
Waziri Mpina akimpungia mkono Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo
na Uvivi Dkt Maria Mashingo akiwa na baadhi ya wajumbe wakiingia kupanda ndege maalum kuanza oparesheni ya
ukaguzi wa uvamizi wa mifugo katika Wilaya ya Mwanga wakitokea Kenya.
NA MWANDISHI MAALUM – KILIMANJARO
Serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe katika suala
zima la uvamizi wa mifugo hususan ng’ombe kutoka katika nchi jirani ya Kenya.
Hayo yamebainishwa wilayani Mwanga na Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipozindua rasmi oparesheni maalum ya uvamizi na utambuzi wa mifugo hiyo tokea angani.
Mpina alisema kuwa uvamizi wa mifugo hiyo tokea nchi jirani
ya Kenya unaleta changamoto kubwa ya malisho ya mifugo ya ndani ya nchi
unaopelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji na
husababisha mmomonyoko wa udongo na uharibifu
wa mazingira.
Baada ya kupokea taarifa ya timu ya wataalam iliyoongozwa na
Katibu Mkuu wa Wizara Mifugo na Uvuvi Dkt Maria Mashingo, iliyofanya oparesheni
hiyo maalum kwa kutumia ndege ya shirika la taifa la hifadhi ya
wanyamapori, (TANAPA) taarifa iliyobaini kuwepo kwa makundi makubwa ya ng’ombe
waliokuwa wakihama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuwepo kwa idadi kubwa
ya Maboma, Waziri Mpina alisema ,
“ Haiwezekani ng’ombe wanaingia kwa makundi makubwa hivi
nchini na watendaji wa serikali wapo, lazima kutakuwa na shida katika utendaji,
Oparesheni hii itakuwa ni ya mwisho, kwa ng’ombe watakaoingia tena watendaji
watatolewa sadaka.” Alibainisha Mpina.
“Yawezekana ng’ombe wote 4000 ambao inasemekana walitoroshwa
hapo awali wapo, hivyo Oparesheni ianze rasmi tuwakamate ng’ombe wote,
tuheshimu sana sheria, na nchi jirani tushirikiane katika mambo tuliyokubaliana
kisheria na lolote litakalotokea katika suala hili la uvamizi wa mifugo sheria
itachukua mkondo wake na tusilaumiane” Alisisitiza Mpina.
Awali wataalam waliyokuwepo katika oparesheni hiyo maalum
waliezeza kuwa mifugo mingi iliyoonekana kutokea angani ilikuwa zaidi katika
maeneo ya malisho na maji ya vijiji vya kiti cha Mungu,njiapanda,kirya na
kitongoi cha Mangulai.
Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilya ya Mwanga imeingia kazini
tayari kwa kuanza oparesheni hiyo maalum.
EmoticonEmoticon