VIWANDA MOROGORO VYAPONGEZWA KWA KUNUSURU UHARIBIFU WA MAZINGIRA

September 29, 2017
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Mbele yake ni Bw. George Mratibu wa Kiwanda cha Ngozi Morogoro , cha ACE LATHER TANZANIA LTD, wakiwa katika ukaguzi wa mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka kiwandani hapo ambapo Mpina yupo Mkoani Morogoro katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na kanuni zake, kufuatia maagizo aliyoatoa awali katika ziara ya viwanda hivyo.
 
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji  Safi na Taka Mjini Morogoro,Injinia Halima Mbiru akimuonyesha Naibu Waziri Mpina mpaka wa mabwawa ya maji taka mali ya mamlaka hiyo hayapo pichani Mh Mpina ambaye alifanya ukaguzi wa mabwawa hayo

Naibu Waziri Mpina akikagua mabwawa hayo kama inayoonekana
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina kulia ni Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dkt Kebwe Stephen Kebwe katika kikao kabla ya kuanza ukaguzi viwandani mkoani humo leo (Picha na Evelyn Mkokoi)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina Amekipongeza kiwanda cha nguo cha 21st century na kiwanda cha ngozi cha ACE LEATHER TANZANIA LTD kwa kutekeleza sheria ya mazingira kwa kujenga mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka yanayotoka katika viwanda hivyo.

Akiwa katika Ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa Sheria ya mazingira Mkoani Morogoro leo, Mpina aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC pamoja na Bonde la Wami Ruvu, kuchukua Sampuli za maji hayo  yanayotibiwa katika viwanda hivyo kwa ajili ya vipimo ili kujiridhisha kuwa hayana madhara kwa mazingira na viumbe hai wengine.

Katika ziara hiyo Mpina, Aliagiza NEMC kumuandikia Barua msajili wa hazina ili kujua ukweli wa mmiliki halali wa mabwawa ya majitaka yaliyotelekezwa katika maeneo ya kilimahewa, ili mmiliki halali wa mabwawa hayo kama ni mamlaka ya majitaka iweze kuyahudumia kwa kuyajengea miundombinu ya kisasa  na kuyatibu ili kunususu mazingira, awali ilielezwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kuwa wakati wa msimu wa mvua maji hayo yamekuwa ni kero kwa wakazi hao kwa kutoa harufu kali.

Naibu Waziri Mpina anaendela na ziara yake ya ukaguzi wa mazingira na utekelezaaji wa shieria ya mazingira mkoani Morogoro.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »