Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapa fursa
mashabiki wengi kuingia uwanjani kuishangilia timu ya taifa ya wanawake
wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itakayocheza na Falconets ya
Nigeria, Jumapili Oktoba mosi, mwaka huu.
TFF imetoa ofa katika kiingilio.
Kiingilio kitakuwa ni Sh. 500 tu kwa mashabiki watakaoketi eneo la
mzunguko huku kwa wale watakaokaa Jukwaa Kuu (VIP) watalipia Sh. 1,000
tu katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es
Salaam.
“Lengo ni kuvutia mashabiki wengi wakaangalie soka la wanawake.
Wakaingalie timu yetu. Wakaangalie uwezo wa timu yetu, waishangilie kwa
nguvu zote,” amesema Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred.
Kocha wa Tanzanite, Sebastian Nkoma, amesema kwa namna alivyokiandaa
kikosi chake ana imani kitaweza kupindua matokeo ya awali ambayo
Tanzania kwa bahati mbaya ililala mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika
Uwanja wa Samuel Ogbemudian, ulioko Jimbo la Benin nchini Nigeria, wiki
mbili zilizopita.
EmoticonEmoticon