Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya
miaka 20 (Tanzanite), Sebastian Nkoma, amekipongeza kikosi chake kwa
kiwango walichokionyesha kwenye mechi dhidi ya Nigeria iliyofanyika
Jumamoisu kwenye Uwanja wa Samuel Ogbemudian mjini hapa.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Nkoma, alisema kuwa kufungwa ni
sehemu ya mchezo, lakini aliweka wazi vijana wake walipambana ila
hawakuwa na bahati ya kupata matokeo waliyoyatarajia.
Kocha Nkoma alisema anaamini watafanya vizuri katika mechi ya
marudiano itakayofanyika jijini Dar es Salaam huku akisema wana nafasi
ndogo ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Mchezo wa marudiano utafanyika Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, uliko Chamazi, Dar es Salaam.
"Kazi haijamalizika, mmefanya kazi kubwa na mmewashangaza wote
walioiangalia mechi hii, waliamini wangepata ushindi mnono zaidi ya huu,
naamini tutafanya vyema katika mechi ya marudiano," alisema kocha huyo
ambaye pia anafundisha timu ya wakubwa ya wanawake ‘Twiga Stars’.
Mkuu wa Msafara, Amina Karuma, alisema kuwa mapambano bado
yanaendelea na anaamini kikosi chake kitashinda katika mechi ya
marudiano itakayochezwa baada ya wiki mbili.
"Msife moyo wanangu, huu ndio mpira na unamatokeo ya aina tatu,
naamini mtawashangaza tena tukia nyumbani," alisema Karuma ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake Tanzania (TWFA) .
Aliongeza kuwa anashikuru wachezaji wote ni wazima na wataendelea na
kambi ili kujiandaa na mchezo wa marudiano huku akiahidi kuwatafutia
mechi ya kirafiki kabla ya kuwakaribisha Nigeria.
EmoticonEmoticon