Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akimkabidhi pesa makamu Mwenyekiti wa timu ya lipuli Ayoub nyezi kwa ajili ya timu hiyo inayoshiriki ligi kui Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/2018
Kocha Mkuu wa timu ya lipuli Suleiman matola akitoa shukrani kwa mbunge huyu Ritta Kabati kwa kuichangia timu hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya lipuli wakiwa wanasikiliza kinachojili wakati walipotembelewa na mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati
Na fredy Mgunda, Iringa
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati ameichangia timu ya lipuli jumla ya shilingi lakini saba kwa ajili ya matumizi ya timu ili kuisaidia timu kufanya vizuri kwenye ligi kuu Tanzania bara ambapo inaonekana kuwa ligi hiyo mwaka huu inaonekana kuwa ngumu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pesa hizo Kabati alisema kuwa ameamua kuchangia timu kwa kuwa anapenda michezo hivyo akiona timu ya inateteleka mara nyingi husaidia pale kwenye uwezo wake.
"Mimi ni muumini sana wa michezo hivyo nimekuwa nikijitolea sana kusaidia michezo mbalimbali ndio maana umekuwa mkisikia nikifanya mambo mengi kwenye sekta hii ya michezo,hivi karibuni nilikuwa nianzisha Mashindano ya Ritta Kabati challenge cup ambayo imesaidia kuinua soka la mkoa wa Iringa "alisema
Kabati alisema kuwa ataendelea kuisaidia timu kadili awezavyo kwa kuwa anaipenda timu ya lipuli hivyo hata akienda china ataitafutia timu ya lipuli jezi ambazo zitawasaidia katika ligi kuu na michuano mingine atayokuwa inaendelea hapo baadae.
Selemani Matola ni kocha mkuu wa timu ya lipuli alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wake alioutoa kwa timu Utasababisha kuwapa wachezaji morali wachezaji kuitumikia timu kwa nguvu zao zote.
"Hakuna kitu Kizuri kama viongozi wa serikali na wanasiasa hasa wabunge kuitembelea timu kunawafanya wachezaji kujiona wanathamani na mchango mkuwa kwa timu na ndio mara nyingi timu kufanya vizuri" alisema matola
Kwa upande wake kapteni wa timu ya lipuli Ally Sonso alimshukuru mbunge huyo Ritta Kabati kwa kujitolea kuisaidia timu ya lipuli kunawapa nguvu wachezaji kuona kuwa wanathamini na viongozi na wananchi wa mkoa wa Iringa.
"Ukiangalia hapa wachezaji wananyuso za kutabasamu kwa kuwa amekuja mbunge huyu Kabati kututembelea hivyo tunashukuru sana maana hii laki mbili kwa sisi wachezaji ni chachu kubwa sana"alisema Sonso
Naye makamu Mwenyekiti wa timu ya lipuli Ayoub nyenzi alisema kuwa mbunge Ritta Kabati amekuwa msaada kwa timu hii kwani ameanza toka timu ikiwa kwenye harakati za kupanda ligi kuu Tanzania bara hivyo ni kiongozi muhimu kwa maendeleo ya timu yetu.
"Kwa kweli hadi saizi hakuna viongozi waliotoa kiasi kikubwa cha Pesa kama mbunge huyu Kabati tunashukuru sana kwa mchango wake ambao unatija kubwa sana kwenye timu" alisema Nyenzi
EmoticonEmoticon