WATAALAMU
na wanazuoni wamekubaliana haja ya kupitia mpango wa maendeleo endelevu
wa viwanda, SIDP (1996-2020), ili kwenda na wakati kwa kubadili kilimo
na kuiweka nchi katika njia bora ya kufikia uchumi wa viwanda.
Kauli
hiyo imetamkwa kwa namna tofauti na wataalamu hao ambao wamekutana
jijini hapa kuangalia uhusiano uliopo kati ya viwanda, mabadiliko ya
tabia nchi na kilimo; na ni namna gani sera ya viwanda inaweza kupitiwa
upya kuakisi mahusiano haya.
Warsha
hiyo iliyoandaliwa na ESRF na CUTS International imelenga katika
kuelezea umuhimu wa kuangalia mahusiano ya sera ya maendeleo ya viwanda
na mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara.
Wakijadili
mada mbalimbali zilizowasilishwa katika semina hiyo iliyofanyika ESRF,
wataalam hao walitambua umuhimu wa pekee wa kupitia upya sera hiyo ili
iweze kuonesha muunganiko fasaha uliopo kati ya viwanda, kilimo na
biashara; na hatua/mikakati ipi iwepo kukinga adhma hii ya viwanda dhidi
ya athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Wamesema
kwamba kwa kuunganisha sera ya maendeleo endelevu ya viwanda na
uchakataji wa bidhaa za kilimo na kilimo chenyewe kunaleta mwanya wa
kuweka msingi imara katika mchakato wa maendeleo na hasa viwanda. Pia,
kwa kuwa na sera madhubuti, nchi itaweza kuvutia wawekezaji wa ndani na
nje ya nchi kuwekeza katika sekta ya Viwanda, hususani viwanda
vinavyotegemea maligafi za sekta ya kilimo.
- Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Katika
mkutano huo ilikubalika haja ya kuwa na mikakati ya utetezi kwa
kuangalia tafiti zitakazofanywa juu ya kinachojiri katika maendeleo kwa
kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara.
Zaidi ya yote, pia wadau waliona kuna haja kubwa ya kuwa na tafiti
itayoweza kuonesha ni kwa kiasi gani sera ya SIDP (1996-2020) imeweza
kuchangia katika ukuaji wa viwanda Tanzania, na changamato zipi
imekumbana nazo ambazo zinapaswa kutatuliwa na kuanishwa wakati wa
mapitio ya sera hii.
Akiwasilisha
hoja yake ndugu Solomon Baregu, Mtafiti wa ESRF na Meneja wa Mradi wa
PACT EAC 2, amesema kwa kuangalia hali halisi ya sasa ipo haja kwa
wataalamu kutambua changamoto zinazojitokeza katika maendeleo endelevu
ya viwanda na kukiangalia kilimo kama msingi wa uimarishaji wa viwanda.
Aidha
alisema kwamba kwa kuangalia hali ya sasa ipo haja kubwa ya kubadili
kilimo cha Tanzania ili kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha
viwanda kwa kuvipatia mali ghafi ya kutosha na yenye ubora.
Alisema
ni vyema kuelewa uhusiano uliopo katika sera za maendeleo ya viwanda na
kilimo ili kuwa na mpango mahsusi wa utetezi kwa lengo la kuimarisha
viwanda.
Katika
mkutano huo washiriki pia walipitia mambo mbalimbali na hatua
zinazochukuliwa kupitia sera ya mpango wa maendeleo wa viwanda
unaomalizika 2020.
- Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Ushirikishaji Kikanda kutioka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bi. Sekela Mwaisela akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Miongoni
mwa mambo yaliyojitokeza kwenye mazungumzo ya tafiti ni umuhimu wa
kuoanisha sera mbalimbali katika kilimo na viwanda kuzihuisha na kuzipa
mwelekeo wenye maana kama chachu katika kuimarisha uchumi wa viwanda.
Walisema
ipo haja ya kuangalia sera hizo ili ziwe msaada katika kuimarisha
kilimo na kutoa ushindani kwa viwanda vinavyotegemea bidhaa za kilimo
ili kujiimarisha.
Aidha
katika mazungumzo kwenye mkutano huo imeelezwa kuwa ingawa serikali
kupitia wizara zake mbalimbali na Ofisi ya Makamu wa Rais wamechukua
hatua kadhaa kuwa na matokeo bora katika utetezi wa bidhaa za viwanda
zinazotokana na kilimo, kukosekana kwa uangalizi na utekelezaji wa
pamoja kumeleta shida kwa wananchi.
Sera
ya sasa ya maendeleo endelevu ya viwanda (SIDP) imetengenezwa mwaka
1996 na itaisha 2020 lakini bado ipo haja ya kuweka mahusiano katika
utekelezaji wa mpango huo wa maendeleo, kwani kwa mazingira ya sasa
hakuna mahusiano na kuna vikumbo katika sera mbalimbali.
Wamesema
kwamba sera hiyo haitoi mwanya wala mahusiano kati ya viwanda vya
kuchakata mazao ya kilimo, mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama
wa chakula.
- Mtafiti wa ESRF na Meneja wa Mradi wa PACT EAC 2, Solomon Baregu akiwasilisha namna bora ya kufanya utafiti wenye lengo la kuoanisha mpango wa maendeleo endelevu ya viwanda na mabadiliko ya tabia nchi na kilimo wakati wa mkutano huo wa kuzungumzia mradi wa PACT-EAC2 uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Aidha
walisema kwamba mpango wa pili wa maendeleo (2016/17-2020/21) unaonesha
haja ya kuweka Tanzania katika njia ya viwanda kwa kuijengea nchi uwezo
wa kuzalisha katika kilimo na pia katika ufugaji.
Haja
ya kubadilisha Kilimo inatokana na ukweli kuwa ni moja ya sekta
zinazoingiza kipato cha kigeni kwani inachangia asilimia 29.1 ya pato la
taifa, huku ikichangia asilimia 30 ya fedha za kigeni.
Aidha
ndio chanzo pekee cha uhakika cha biashara ikitoa asilimia 65 ya
mahitaji ya viwanda (ghafi) na asilimia 90 ya chakula cha taifa huku
ikiajiri asilimia 66.9 ya nguvu kazi ya Taifa.
Ndugu
Peter Lanya, aliekua Makamu Mwenyekiti wa TCCIA, akitoa ufafanuzi zaidi
alisema kwamba kunatakiwa mabadiliko katika sera hiyo ili kuupa usasa
kwa kuwekeza kwenye mahusiano ya kilimo, mali ghafi kama taifa likitaka
kuendelea kuelekea uchumi wa viwanda.
Naye
ndugu, Joseph Kihaule, Afisa Mkuu wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu
wa Raisi, alisema kwamba kuna haja ya kubadilika katika kilimo ili
kuweza kufanya vyema huku akisema mazungumzo ya kimataifa ya kupata
muafaka, hususani yahusuyo mabadiliko ya tabia nchi, ni muhimu
yakaunganishwa na sera mbalimbali ili kuimarisha kilimo na upatikanaji
wa chakula.
- Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa TCCIA, Peter Lanya akizungumzia SIDP 1996-2020 wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Ushirikishaji Kikanda kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bi. Sekela Mwaisela.
Awali
akifungua semina hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na
uwekezaji (viwanda) Adelhelm Meru alishukuru taasisi za ERSF na CUTS
International kwa kuona umuhimu wa kuwa na mkutano huo wanne wa kitaifa
kuzungumzia mradi wa PACT-EAC.
Katika
hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Viwanda
Ushirikishaji Kikanda, Bi. Sekela Mwaisela alisema kwamba wizara
inatambua haja ya kuweka pamoja viwanda na uchakataji wa mazao ya kilimo
kwa kuwa inasaidia kuweka sawa maendeleo ya viwanda.
Alisema
kwamba kazi iliyofanywa na ESRF inaiweka wizara hiyo katika nafasi bora
zaidi ya kufanya mabadiliko ya muhimu kufikia mwaka 2020.
Alisema
sera hiyo iliyoanza 1996-2020 imepita katika maeneo matatu ambayo
yalilenga kuimarisha uwezo wa viwanda (1996-2000), matumizi ya
teknolojia (2000-2010) na uimarishaji wa viwanda 2010-2020.
Alisema
SIDP imesaidia kuimarisha viwanda na sasa lazima kuwepo na uangalizi
ili kuwepo na mahusiano mazuri kati ya sera zote zinazotegemewa
kuwezesha maendeleo endelevu ya viwanda.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida katika hotuba yake
iliyosomwa na Prof. Fortunata Makene amesema ipo haja kubwa ya kuwepo
kwa mabadiliko katika SIDP kutokana na mahusiano yake na sekta nyingine
hasa yenye uhusiano na kilimo.
Katika
mkutano huo wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji
kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki
(PACT EAC2), Dk Kida alisema kwamba taasisi yake imefurahi kutoa mchango
kwa ajili ya kusaidia kuimarisha viwanda nchini.
Alisema
mkutano huo unaoangalia namna ya kuboresha sera ya viwanda, SIDP
(1996-2020), kabla ya utafiti utakaoanza baadae ni muhimu katika kuona
kwamba kilimo kinaboreshwa sanjari na SIDP kwa kuweka mahusiano ambayo
awali yalikosekana katika sera ya SIDP.
Alisema
kwa taifa la Tanzania ili lisonge mbele ni vyema masuala muhimu katika
SIDP yakaangaliwa ili kutekeleza mipango ya maendeleo ya viwanda kwa
kuhusisha na uchakataji wa mazao ya kilimo.
Aidha
alisema katika utafiti utakaosaidia kuboresha SIDP majukumu ya biashara
ya kimataifa katika maendeleo ya viwanda na tabia nchi haviwezi
kudharaulika.
Alisema
utafiti utakaofanywa utasaidia kuongeza ‘nyama’ zaidi katika mikakati
ya maendeleo kwa kufanya utetezi kwenye mabadiliko ya tabia nchi,
biashara na usalama wa chakula kwa kufanya mabadiliko makubwa katika
uchakataji bidhaa za kilimo kwa kutambua pia makubaliano ya kimataifa
ambayo Tanzania ni mshiriki, hususani UNFCCC na WTO.
EmoticonEmoticon