SHAKA ASIFU UZALISHAJI WA ZAO LA KARAFUU, ASEMA SERIKALI ILINDE ASILI YA ZAO HILO

August 20, 2017
Zao la Karafuu
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akipanda miti aina ya Mikoko Kwa ajili ya kutunza Mazingira wakati wa ziara yake katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwasili katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya kujionea hali ya upandaji miti aina ya Mikoko unavyoendelea.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumza jambo na Mdhamini wa Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar mara baada ya kutembelea ofisi hizo kujionea hali ya ukusanyaji wa zao la karafuu Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Zao la Karafuu likiwa limehifadhiwa ghalani chini ya Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar
Vijana wakijishughulisha na shughuli za ubabeji mizigo katika ghala la kuhifadhia zao la Karafuu, Wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza maelezo mbalimbali ya Mdhamini wa Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar mara baada ya kutembelea ofisi hizo kujionea hali ya ukusanyaji wa zao la karafuu Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Na Mathias Canal, Pemba

Zanzibar ni maarufu kwa uzalishaji wa karafuu ulimwenguni kwa zaidi ya  karne mbili sasa. Uzalishaji huo ulikuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia tani 35,000 mwaka 1830 na kumiliki soko la karafuu duniani kwa asilimia 90.

Iliongoza katika uzalishaji wa zao hilo kuanzia mwaka 1830 hadi 1940 kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Indonesia.Tathmini iliyofanywa hivi karibuni ya Sensa ya Miti (Woody Biomass Survey 2013) imeonesha kwamba Zanzibar kwa sasa ina idadi ya mikarafuu 4,131,783, ambapo Unguja pekee ina zaidi ya mikarafuu 277,196 na Pemba zaidi ya mikarafuu 3,854,587.

Tathmini ya mwaka 1997 ilionesha idadi ya mikarafuu 790,400 kwa  Unguja na mikarafuu 5,042,700 kwa upande wa Pemba, ikifanya idadi ya mikarafuu yote kuwa ni 5,833,100

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amelitaja zao la karafuu kuwa ni zao muhimu kwa uchumi wa taifa ambalo huongeza kwa kiasi kikubwa kipato kwa wananchi.

Alisema katika kuimarisha zao la karafuu Zanzibar, pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kuna haja ya kupandwa mikarafuu na minazi maskulini, ili wanafunzi waweze kupata uwelewa zaidi wa kutunza na kulienzi zao hilo, kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.

Shaka alisema hayo wakati alipotembelea na kupanda miti aina ya Mikoko Kwa ajili ya kutunza Mazingira ili kuhuisha uoto wa asili na kuepuka mmomonyoko wa ardhi katika eneo la Mwambe lenye asili ya Watumbatu Wilaya ya Mkoani na Mkoa Ni Kusini PEMBA .

Pia aliwasisitiza wananchi kuhusu kupanda miche ya mikarafuu na minazi na kutotupa taka ovyo ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi.

Alisema kuwa serikali inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa inaandaa sheria kali itakayokuwa maalumu kwa kuwachukulia hatua wananchi wanaokata miti ovyo kinyume na utaratibu.

Katika hatua nyingine Shaka alitembelea shirika la Taifa la Biashara Zanzibar kujionea hali ya ununuzi wa zao la karafuu ambapo alimpongeza Mdhamini wa wa shirika hilo Ndg Seif Suleiman Kassim kutokana na kiwango kikubwa cha ukusanyaji wa zao hilo ambapo katika msimu huu hadi kufikia Mwezi Julai 13, 2017 tayari 2203 sawa na Kilogramu 99180.0 zilikuwa zimehifadhiwa kwa ajili ya kupelekwa Unguja.

Alisema uzalishaji wa zao la karafuu, katika Wilaya ya Mkoani unaongoza kwa zaidi ya asilimia 60 ya uzalishaji wa zao hilo kwa zanzibar, na amewataka wananchi kuendelea kutunza mikarafuu, kwani ndio pato la Taifa.

Zanzibar ni visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora duniani. Katika miaka 30 ya nyuma pia ilisifika kwa uzalishaji karafuu nyingi, wastani wa tani 8,605 zilikuwa zikizalishwa kwa mwaka.

Jamii ya wakati huo walikuwa wakizijali, wakizithamini na wakizipenda sana karafuu ukilinganisha na kizazi cha sasa. Walihakikisha karafuu zao wakiuza vituoni tena zinakuwa safi, zimekauka vizuri na zinapata daraja la kwanza.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »