- Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (wa kwanza kulia) akifurahi pamoja na maofisa wa Benki ya NMB mara baada ya uzinduzi rasmi wa hafla ya siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu ilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hazini jijini Dodoma.
- Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu katika mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki.
- Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya walimu mkoa wa Dodoma.
BENKI ya
NMB imezindua rasmi siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo
wa siku ya walimu Mkoa wa Dodoma ulizinduliwa rasmi na Afisa Tawala wa
Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Bw. Jordan Rugimbana.
Hafla
hii adhimu ilifanyika katika ukumbi wa Hazina na kuhudhuliwa na zaidi
ya walimu 200 wa mkoa huo mwishoni mwa wiki. Uzinduzi wa hafla hii ni
miongoni mwa mikakati ya NMB ya kuwafikia walimu nchini kote. Kusudi
kubwa la hafla hiyo ya NMB na Walimu ni kuwaongezea uelewa walimu juu ya
huduma za benki.
Hii
ni kutokana na umuhimu wa kundi hili kubwa katika jamii inayotuzunguka.
NMB wanaimani kwamba mwalimu akielimika jamii nzima itakua imepata
elimu ya huduma za kifedha. Lakini pia kwa kuzingatia ukubwa wa kundi
hili NMB imekua ikitumia fursa hii kupokea mrejesho ya jinsi huduma za
kibenki zinavyopokelewa na wateja wake.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo mjini Dodoma, Meneja mwandamizi wa wateja binafsi
wa NMB, Omari Mtiga alisema NMB inazo huduma mbalimbali ambazo kusudi
lake kubwa ni kumsaidia mteja aweze kujikwamua kiuchumi. Aliongeza kuwa
zipo huduma za mikopo ya aina mbalimbali ambapo walimu wanaweza
kunufaika nayo.
Mikopo
ambayo inatolewa na Benki ya NMB sio kwa ajili ya wafanyabiashara tu
bali ni kwa ajili ya kila mtu mwenye vigezo vya kukopeshwa ambapo walimu
ni miongoni mwa walengwa wa mikopo hii. Msichukue mkopo benki kama
hamna mipango thabiti ya matumizi ya mkopo huo, Ni vyema kuchukua mkopo
benki ukiwa na mipango endelevu," alisema Bw. Omari Mtiga.
"...Tukiwa
kwenye mikakati ya serikali ya Viwanda ni vyema mkatumia vizuri
maonyesho ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza kutembelea mabanda ambayo
mtajifunza namna ya uwekezaji kwenye sekta viwanda ili kujikwamua
kiuchumi kwa kutumia uwepo wa benki ya NMB kwenye jamii yetu bila
kuathiri mwenendo wa jaira zetu. Alisema kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Bi. Rehema Madenge katika hafla hiyo.
- Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya walimu mkoa wa Dodoma.
- Picha za kumbukumbu na Sehemu ya walimu pamoja na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge.
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
EmoticonEmoticon