Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika

June 17, 2017
Mtoto Ethan Thedore Yona akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kwa njia ya mtandao(App) kijulikanacho kama Ethan Man, hafla hiyo imefanyika leo kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam.

Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo.

Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo.



JUNI 16, 2017: Dar es Salaam, Tanzania. Katika maadhimisho ya Siku yaMtoto wa Afrika mwaka huu  mtoto mwenye umri wa miaka sita  Ethan Theodore Yona  anayesoma darasa la kwanza  amezindua zana(App) yake ya android  ambayo inaonesha shujaa wa hali ya juu akiwa ni muhusika  anayejulikana kama EthanMan. Mhusika  anaegemea upande wake  ni mwenye kipaji kikubwa, ameandika vitabu vya kuvutia,  kubuni michezo ya kijifunza  na kuwapelekea watoto katika  safari za mafunzo.
 Ethan alianza kujishughulisha na mradi huo  alipokuwa na umri wa miaka mitano katika shule ya awali  ikiwa ni matokeo ya mapenzi yake katika  michezo na kujifunza. “Kila mara nilikuwa na nguvu , kufurahia kujifunza  vitu vipya  na kupenda kucheza michezo mbalimbali. Siku moja niliwaambia wazazi wangu  ningependa kuanzisha  mhusika mkuu  jasiri  kwa kuzingatia ubora wangu. Baadaye waliniuliza  ubora huo ni upi  na nikawaambia  mimi ninakipaji kikubwa  na ninaweza kuwa kitu chochote ninachokipenda , naweza kuwa mchezaji soka, nyota wa muziki, mhandisi n.k. Na hivyo ndivyo wazo la mhusika shujaa mkuu  lilivyoanza.”
Ethan  alifanya kazi hiyo na mshauri wa  teknolojia ya elimu katika i-LearnEast Africa, na ambayo inatoa kozi kwa njia ya mtandao  na mafunzo ya mabadiliko  kuunda mhusika huyo  na kuanzisha  kitabu chake cha kwanza cha picha  alichokiita “Nitakapokuwa Mkubwa”. Tulivutiwa sana kufanya kazi na Ethan  katika mradi huu. Inafurahisha kwamba  mtoto mdogo namna hii  kutaka kufanya jambo hili kubwa tulitaka kuwa sehemu  ya huu mradi tangu mwanzo. Ikiwa ni kampuni ya ushauri katika masuala ya elimu tuliona umuhimu wa kujifunza  ambao mradi huu utawapatia watoto. Mchango wa Ethan katika kuandaa kitabu hiki ni wa kushangaza,” alisema Ofisa Mtendaji wa Learn Tech, Deus Ntukamanzina. 
Zana hiyo na michezo  ilianzishwa kwa ushirikiana  na kampuni ya Tujenge Technology  ambayo imejikita katika kuanzisha masuluhisho ya kidijitali  ambayo  yatawezesha  kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii.
 “Tulipoombwa  kuanzisha michezo ya EthanMan  tulifurahi. Kuwa sehemu ya  mradi huu wa kipekee  ndicho kilichotufanya  kuingia katika teknolojia na  kuianzisha. Mchango wetu ilikuwa ni  kuunganisha  mhusika EthanMan na vipaji vyake vingi katika jukwaa ambalo  itakuwa ni rahisi kufikiwa  na kuanzisha  uzoefu mkubwa wa kutumia miongoni mwa watoto. Mchango wa ethan katika kuanzisha michezo ni wa hali ya juu, kwa sababu  kila kitu kimejielekeza katika maisha yake  kama mhusika. Tulikuwa na muda mzuri wa  wa kuunda  kile ambacho tunaamini  kuwa ni bidhaa ya kwanza ya mchezo katika anga ya teknolojia nchini Tanzania.
Zana (App) ya EthnMan  inapatikana kwa kupakua katika hifadhi ya michezo ya android , watoto wataweza kusoma vitabu, kucheza michezo. Na kuwa pamoja na muundaji wa EthanMan, Ethan Theodore Yona.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »