Na Benny Kisaka
Abdulkarim Omary Mtiro, almaarufu Cisco Mtiro, umelala Brother tangulia.
Umelala usingizi. Usingizi ambao hautaamka wakati huu. Hautaamka brother kwa kuwa wanaolala usingizi huu wanamngoja aliyewaumba awaamshe.
Kwa neema yake kuu iko siku utaamka Brother. Mara hii ukiamka hutalala tena.
Naam, hutalala. Maana utakuwa umevuka ng'ambo ya pili ya mto. Huko hakuna uchungu na maumivu makali kama uliyoyapitia nyakati zako za mwisho za uhai wako ukiwa hospitali ya Aga Khan. Pumzika kaka yetu.
Leo June 7, saa 7 mchana tunakuzika kwenye makaburi ya Kisutu mahali ambapo miezi michache iliyopita tulimzika rafiki yako wa karibu Afande Chicco. Pumzika kwa amani, mpaka tutakapoonana tena huko juu Ng'ambo ya pili.
Mwanadiplomasia uliyewahi kuwa balozi mdogo Nigeria na pia Balozi Kamili nchini Malaysia.
Tunakuita brother kwa wakazi wa Temeke tukijua umezaliwa peke yako kwa Mzee Omary na Bi Ummi Seif.
Akiwa amezaliwa mtaa Kipata Kariakoo mwaka 1950, baada ya miaka miwili alihamia Temeke hadi anamaliza elimu ya Chuo Kikuu, alihama pale alipoanza kazi wizara ya mambo ya Nje.
Cisco ni jina la utani lililochepua hadi kuliweka rasmi hata kwenye passport yake ikisomeka Abdul Cisco Mtiro amefariki akiwa na miaka 67.
Leo Temeke itanyanyuka eneo ulilokulia na kusoma elimu yako ya msingi shule ya Temeke, na kumaliza elimu hiyo mwaka 1965.
Itakumbukwa 1997 aligombea Ubunge Temeke akishindana na Mrema, viongozi wote wa ngazi za juu wa CCM walikuja kukupigia debe lakini kura hazikutosha.
Umaarufu wako upo Chang'ombe, Ilala, Wailes, Kurasini Masaki, Magomeni, Mbezi Beach, Kariakoo na hata Kinondoni yote.
Ameishi Mikocheni B hadi umauti umemkuta, lakini muda mwingi amekuwa akikutana na marafiki zake viunga vya Kinondoni kwa John Fedha ama nyuma ya ubalozi wa Ufaransa kijiwe cha Octa.
Ni mmoja wa waanzilishi wa bonanza la kila jpili pale Leaders Club, mshabiki mkubwa wa Yanga, rafiki wa kila tabaka na rika na hakuwa mtu wa kujikweza, umaarufu wake ulitawala kwa kuwa mtu mwenye utani mwingi...
Ni mtoto wa mjini hasa, hakuhitaji aimbwe redioni kutokana na sababu zozote.
Nilikuwepo Kisutu kukuzika bro, ulishiriki msiba wa baba yangu Christopher kisaka, ambaye alikuwa mwalimu wako shuleni Temeke, ulitukaribisha nyumbani kwako kupata chakula cha jioni mara kadhaa tulipofika Kuala Lumpur, Malaysia 2011 nikiwa na Juma Pinto, ulinialika arusi ya mwanao Omary, pia nilishiriki.
Mwanadiplomasia, mkuu wa Itifaki mstaafu kwa Mwalimu Nyerere, Mzee Mkapa na awamu ya nne ya Jakaya Kikwete.
Ulikuwa mgeni rasmi miss Temeke 2003. Ulikuwa judge miss Tanzania 2004.
Cisco ana marafiki lukuki kiasi kila mmoja anaweza kumwandika amjuavyo, tena zaidi na vizuri kutipa mimi, ila kwa udogo huu naomba mwenyezi Mungu akupumzishe kwa Amani
EmoticonEmoticon