Na Woinde Shizza,Arusha
Kikosi cha Afc Arusha kimejinasibu kuwa kitawafunga
mabigwa wa ligi kuu bara msimu uliomalizika
Timu ya Yanga Afrika,katika
mchezo wao wa kirafiki unaotajarajiwa kupichezwa Jumapili hii May 28 katika kiwanja cha kumbukumbu ya
Sheikh Amri Abeid jijini hapa
Akiongea na Tanga Raha Blog Kocha wa kikosi hichi
kipya cha timu ya AFC Fikiri Elias
alisema kuwa vijana wake wapo tayari kuwapatia burudani wapenzi wa ke wa
soka mkoani hapa huku akiwapa sifa viongozi wa serikali kwa kuwa begakwa bega
katika kuhakikisha soka la mkoa wa Arusha linarudi katika ramani yake
Alisema kuwa japo hii ni mechi yao ya kirafiki baina
yao na timu ya Yanga lakini watatumia mchezo huu pia kuangalia kikosi bora
ambacho kitakaa kambini kwa ajili ya kuandaa timu ya kikosi kitakacho unda AFC
mpya itayoshiriki ligi daraja la kwanza .
,, Pamoja ya kuwa timu ya yanga inawachezaji wazoefu
wengi na pia ndio wametoka tu kutwaa ubigwa mara ya tatu lakini napenda kusema
hivi japo mechi hii ni ya kirafiki lakini nimeaada kikosi kizuri nanauhakika
lazima tutaifunga timu hii ili tuweke historia japo ni mechi ya kirafiki
,,alisema Fikiri
Kwa upande wake kocha msaidizi timu ya
Yanga ambao wameshikilia ubigwa
kwa mara ya tatu mfulukizo ligi kuu bara
Juma Mwambusi alisema kuwa mchezo huu ni muhimu kwao kwani ni moja ya program zao katika kujiandaa kuelekea
katika michuzano inayowakabili ikiwemo
mashindano ya Sport Pesa
Kikosi hichi cha yanga kipo katika ziara ya
kutembeza kombe lake kwa mashabiki wa mikoani ambapo mkoa wa Arusha umekuwa wa
kwanza kuona kombe hilo na wakitoka mkoani hapa wanampango wa kulipeleka mkoani
Dodoma ,ambapo pia wanajangwan hawa wamekuwa ni timu ya tatu kuoka ligi kuu
bara msimu ulioisha kutoa katika aridhi ya jiji la Arusha iliyokuwa na ukame wa
timu za ligi kuu mara baada ya timu za Ruvu shooting na Simba zilizowaikutua hapa katika mtanange wake
ulioisha
Akizungumzia mchezo huo wa kirafiki mmoja wawaandaaji wa mechi hiyo ambayo katibu
wa timu ya AFC Charles Mwaimu alisema
kuwa maandalizi yote yamekamilika timu zote zipo tayari wanaisubiri tu siku ya
mechi ifike.
Aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na pembezoni
kujitokeza kwa wingi kuishabikia timuyao ya AFC ikiwa ni ujio mpya wa timu hii
mara baada ya kupotea kwa muda ,na aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha
kujitokeza kuwapa morali wachezaji wao .
Aidha alisema kuwa pia mbali na mechi hii ya yanga
kucheza na AFC pia wanampango wa timu hii kwenda mkoani manyara kucheza mechi
baada yao na timui ya Merirani.
EmoticonEmoticon