Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Mamlaka ya
Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230 kwa
kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo
wa kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani wakati akijibu swali
la Mbunge wa Kigamboni Mhe.Dkt Faustine Engelbert leo Bungeni.
“Mtambo huu umesaidia Mamlaka ya
Mawasiliano nchini kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya
Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea
katika Sekta ya Mawasiliano Duniani kote”,Aliongeza Mhe.Ngonyani
Aidha kati ya pesa izo bilioni
56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni 6,028,081,599
zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya
kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya
hapo kahukuwa na mapato hayo.
Amesema mtambo huu umeiwezesha
TCRA kuwa na uwezo wa kusimamia mawasiliano ya simu za Kimataifa na zile
za mwingiliano,pia mtambo huo umesaidia kudhibiti mawasiliano ya Simu
za ulaghai za kimataifa na kusimamia ubora wa mitandao katika kutoa
huduma bora kwa wananchi,kudhibiti namba tambulishi za vifaa vya
mawasiliano nchini pamoja na usimamiaji wa miamala ya fedha inayopita
katika mitandao ya simu hapa nchini.
“Aidha pamoja na mafanikio hayo
jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na kujiridhisha
juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za mawasiliano na yanayokidhi
mahitaji ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA
zinaendelea”Aliongeza Mhe.Ngonyani.
Aidha Serikali itaendelea
kuwajengea uwezo wataalamu wa TCRA ili waweze kuendana na kasi ya ukuaji
wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususani katika eneo hili la
kuchakata taarifa mbalimbali za huduma za mawasiliano zinazopatikana
kutoka kwa watoa huduma ili kuweza na kujiridhisha juu ya mapato yote.
chanzo:fullshangwe.com
EmoticonEmoticon