Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya
Masasi, Seleman Mzee, wakati alipokuwa anawasili wilayani humo, Mkoa wa
Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia), kuingia Gereza la Kilimo na
Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasikwa ajili ya ukaguzi wa Gereza
hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa
wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anamfafanulia jambo mara baada
ya kutoka ndani ya Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo
wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa
ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anatoa maelezo kuhusu
Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi. Gereza
hilo lina wafungwa zaidi ya 60 ambao wanafanya shughuli za kilimo na
ufugaji. Kikao hicho kilifanyika ofisi ya Mkuu wa Gereza hilona
kuhudhuriwa na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo
vilivyo chini ya wizara yake pamoja na viongozi wa wilaya hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiiangalia moja ya nyumba za
askari magereza zilizopo jirani na Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani
wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa huo
(RPO), Ismail Mlawa. Kushoto ni Ahmed Bakari, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo.
Masauni alimaliza ziara yake ya mikoa ya kusini kwa kutembelea Gereza
hilo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
EmoticonEmoticon