BODABODA YATAJWA KIKWAZO CHA BAADHI YA WANAFUNZI KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO YAO

February 11, 2017
USAFIRI wa pikipiki maarufu kama bodaboda wilayani Mkinga mkoani Tanga umetajwa kuwa miongoni mwa vishawishi vikubwa vya kukwamisha juhudi za elimu kwa wanafunzi wa kike kutokufikia malengo yao .

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya shule nyingi kukosa mabweni ambayo
  yanaweza kuwasaidia wanafunzi hao kuepukana na vitendo vya namna hiyo ili waweze kufikia malengo yao ya kupata elimu bora.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu
  wilayani humo, Ajalii Marumwengu wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema hali hiyo inaatokana na shule nyingi kuwepo mbali na sehemu wanazoishi wanafunzi.

Alisema hali hiyo inatokana na mazingira ya umbali wanaotoka wanafunzi
  kuwa mbali na hivyo wengine kulazimika kutembelea umbali wa km 14 mpaka kufika maeneo ya shule.
 “Ukiangalia uhalisia wa mazingira ya shule za kata hasa zilizopo
maeneo ya vijijini ni mbali kwa zipo nyengine ambazo wanafunzi
wanatembea umbali kilomita 7 mpaka 14 hivyo wanapokutana na pikipiki maarufu kama bodaboda na kupewa lifti na baadae wanashawishika kuingia kwenye mahusiano”Alisema.

“Lakini njia sahihi ya kuhakikisha suala hilo linakwisha ni kuwekwa
  mazingira mazuri ya kuanzishwa bweni kwenye shule hizo ili wale wanaokaa mbali waweze kuishi humo ili kuepukana na vishawishi “Alisema.

Aidha alisema pia changamoto nyengine wanao kabiliana nazo ni

kutokuwepo kwa nyumba za walimu na hivyo walimu hao kulazimika kukaa umbali mrefu na maeneo wanayofundishia.
 “Zipo shule nyingi hapa mkinga walimu wanafundisha lakini hawana nyumba za kuishi na hivyo kujikuta wakitembea umbali mrefu kwenda kufundisha hivyo tunaomba hilo nalo liangaliwe kwa jicho la kipekee”Alisema.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »