SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO

January 20, 2017



Na Woinde Shizza,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali haitasita
kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya
Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo.


Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali.

Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa macho

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu
wachache


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi  ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha  Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo



Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori tengefu katika wilaya hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »