WAZIRI MAKAMBA AKAGUA MIRADI INAYOFADHILIWA NA OFISI YAKE

January 01, 2017
kamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Diwani wa Kata ya  Buguruni Mhe.  Adam Fugame (katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni
kamba-2
Sehemu ya Mfereji wa Maji taka unaojengwa eneo la Ilala Bungoni chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).
kamba-3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Wananchi wakazi wa Ilala Bungoni, mara baada ya
kamba-4
kukagua ujenzi wa mrefeji wa maji taka
Bw. Gervas wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Ltd (kulia) akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke – Mtoni kwa Azizi Ali ambapo Kampuni hiyo imepewa kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka.
kamba-5
Mwakilishi wa UNOPS Bw Bernard Omondi akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke – Mtoni kwa Azizi Ali ambapo kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka inaendelea.
kamba-6
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ( wa tatu kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya ziara ya kukagua hatua za ujenzi kwa miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.  Kulia ni Bw. Kanizio Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Msimamizi wa Mradi na Bw. Richard Muyungi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira.
……………..
Na Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amefanyia ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa na Ofisi yake.
Akiwa katika Wilaya ya Ilala, Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa kupitishia maji taka katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi wa eneo hilo.
Waziri Makamba ameugiza uongozi wa Dezo  Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.
“Nataka mradi huu uwe wa mfano kwa ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka mfumo mzuri wa kukusanya maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki” Makamba alisisitiza.
Aidha, Waziri Makamba amewataka wakazi wanaozuka eneo hilo kuacha mara moja utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.
“Kwa kupitia kamati za Mazingira za vitongoji na sheria ndogo ndogo mlizojiwekea hakikisheni kuwa hifadhi ya mazingira inazingatiwa kwa mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.”
Pia, Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Wakandarasi wanaopewa kazi za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na uwezo wa kutosha kwa kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa taka katika makazi ya watu.
“Natoa wito pia kwa vijana wa maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka ili kuwa chanzo cha ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira –  NEMC kutembelea eneo hilo la Ilala Bungoni na kutoa maelekezo kwa Gereji bubu  zinazokiuka hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya shughuli zao pembezoni mwa mfereji unaojengwa.
Ujenzi wa Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Aidha, Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya kazi ya ujenzi huu na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.
Waziri Makamba katika ziara yake hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa Azizi Ali, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la Ujenzi wa Ukuta Barabara ya Obama.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »