Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa
Mbaruku amewatakia heri ya sikukuu ya mwaka mpya wakazi wa Jimbo lake na kuwataka wajitume zaidi ili kuweza kupata
mafanikio.
Akitoa salamu hizo kwenye ofisi yake
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo,Mbunge Mussa aliwataka wananchi
hao kutambua kuwa wanashirki kwenye shughuli za kimaendeleo ili kuweza
kujikwamua kiuchumi.
Alisema licha ya kushiriki huo lakini
pia wakulima watambue katika kipindi hiki wanapaswa kutayarisha mashamba yao
ili kuweza kulima kilimo cha kisasa chenye tija.
Aidha pia aliwataka kuhakikisha
wanawajibika kusafisha maeneo yao ili yaweze kuwa na muonekana mzuri ili waweze
kuepukana na magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokana na kuwepo kwa hali hiyo.
“Lakini
pia ni niwatake halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanasafisha maeneo yao
kwa kuondoa takataka “Alisema Mbunge Mussa.
Sanjari na hilo Mbunge huyo pia
aliwataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenye Jimbo lake
kuhakikisha wanaongeza bidhii kwenye masomo ili waweze kufanya vizuri kwenye
mitihani yao
“Niwaambie
wanafunzi wakati wanapokuwa shuleni acheni masuala ya michezo badala yake
hakiksheni mnazingatia elimu kwani ndio mkombozi mkubwa kwenye maisha yenu ya
sasa na baadae “Alisema.
EmoticonEmoticon