MASHINDANO YA SCOUT KANDA YA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA ARUSHA

December 15, 2016






Skauti wa TZ na wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakipita
mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano ya
skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani Arusha
Skauti Tz na wengine kutoka nchi za afrika mashariki
wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa kambi ya
mashindano inayoendelea mkoani Arusha
Skauti kutoka Kenya na wengine wa nchi za Afrika Mashariki
wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya
mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani
Arusha
.


Na Woinde Shizza,Arusha
Vyama vya scout kanda ya Afrika Mashariki vimekutana mjini hapa kuanza mashindano ya  mascout  yenye lengo la kuwezesha vikosi vya scout kushindana pamoja ili kujipima katika utekelezaji wa programu ya vijana ya stadi za kiscout katika vikosi na jumuiya ya afrika mashariki ambazo
wamekuwa wakijifunza katika maeneo yao.

Akizungumza katika mashindano hayo yalioanza jana meneo ya kisongo jijini hapa,kamishna mkuu wa chama cha skauti tanzania Rashidi Mchata alisema kuwa mashindano hayo yameshirikisha  vijana wa kiscout kutoka nchi tano za
jumuiya ya afrika mashariki.

Mchata alisema kuwa mashindano hayo yatahusisha makundi ya mascout wadogo ,mascout wakubwa na masouti vijana  kutoka kila nchi yatashindana kutengeneza stadi za kiskauti kwa kutumia mbinu zao ambazo wamekuwa
wakifundishwa katika vikosi vyao   kwa ajili ya kuwawezesha kuhudumia jamii na kuwafanya wawe wazalendo.

"Vyama vya mascout kutoka jumuiya ya afrika tumekutana hapa arusha kwa malengo matatu ikiwemo mashindano ,jukwaa la vijana mascout lakini pia
tumekuwa na mkutano mkuu wa makamishna wa skauti kutoka nchi za jumuiya na hii inasaidia kwa pamoja kuhakikisha kuwa vijana wetu wanakuwa wazalendo na
kupitia haya mashindano tutaweza kuwapata washindi ambao wanawakilisha nchi zao walizotokea"alisema Mchata.

Rehema Ramadhani mwanascout kutoka  dar es salaam ambae anawakilisha tanzania katika mashindano hayo alisema kuwa mashindano hayo yanajumuisha mambo yote waliokuwa wanafundishwa kuanzia ngazi ya wilaya na kwamba
yanawapa uzoefu wa stadi zao kutoka kwa mascout wa nchi nyingine za jumuiya ya afrika mashariki.

Alisema kuwa katika vikosi vyao wamekuwa wakifundishwa mambo mbali mbali ikiwemo utunzaji wa mazingira kama ilivyo kauli mbiu ya rais magufuli lakini pia jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu au jamii pale inapopata janga na hivyo wanaamini kuwa wataiwakilisha tanzania kuwa mshindi katika
mashindano

Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la vijana wa  kiscout katika jumuiya ya afrika mashariki Murtadhwa Abdallah alisema kuwa taasisi mbali mbali zinatakiwa kujitokeza na kushirikiana katika kufadhili scout kwani vyama
hivyo vimekuwa vikikabikiwa na changamoto ya fedha hivyo kushindwakujiendesha vyenyewe.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »