Na Bashir Nkoromo, Dar
Chama
Cha Cha Mapinduzi (CCM), leo kimeteua viongozi waandamizi watatu kuziba
nafasi zilizokuwa wazi, kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa
majukumu mengine ya serikalini.
Uteuzi
huo, umefuatia Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) katika kikao
chake, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo chini ya
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, na kuridhia mapendekezo ya
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika juzi pia chini ya Dk.
Magufuli.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,
Lumumba jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye amesema, kupitia vikao hivyo, CCM imemteua Rodrick
Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa
wazi na Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Nape
alisema, wapili ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga, kuwa Katibu NEC Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Asha-Rose
Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi na Humphrey Polepole aliyeteuliwa kuwa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Nape
mwenyewe aliyeteuliwa kuwa Waziri.
Amesema,
kupitia kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa, kilichofanyika leo,
mambo kadhaa yaliyopendekezwa na Kamati Kuu, yamejadiliwa na kikao hicho
cha NEC na yote yamepitishwa. Kusoma taarifa ya yooote, yaliyojiri katika kikao hicho cha NEC, sasa/BOFYA HAPA
EmoticonEmoticon