WANAOWABEZA MAWAZIRI WA MAGUFULI KUWA HAWAMSHAURI NA WANAMUOGOPA WAMECHEMSHA – MPINA.

November 28, 2016


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (MB) wa Kisesa akivalishwa Scarf na Kijana Mussa Sulumbi baada ya kuwasili katika viwanja vya makao makuu ya Jimbo vilivyopo katika mji mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu.


Pichani, sehemu ya Hadhara iliyokuwepo katika mkutano wa Chama Cha Mapinduzi jimboni Kisesa.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina (MB) wa Kisesa akihutubia wananchi wa Jimbo lake hawapo pichani katika mkutano wa kuelezea mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani ya CCM na utatuzi wa changamoto za jimbo la Kisesa. (Picha, Habari na Evelyn Mkokoi Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais)



Diwani wa Kata ya Lugeka (CHADEMA) Mhe. Zakayo Sarya akiongea mbela ya Hadhara haipo Pichani, akisimama pamoja na madiwani wa Jimbo la Kisesa katika mkutano wa CCM jimboni humo.



Na Evelyn Mkokoi – Mwandoya Meatu
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye Pia ni Mbunge wa jimbo la Kisesa Wilayani Meatu, amesema waowabeza Mawaziri wa Rais Magufuli na kusema kuwa wanamuogopa na kuwa hawawezi kumshauri wamechemsha na wanajidanganya.
Naibu Waziri Mpina (MB) ameyasema hayo leo jimboni Kisesa alipokuwa katika Mkutano na Jimbo wenye lengo la kuelezea mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utatuzi wa Changamoto za Jimbo Hilo.
Mpina alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano wamekuwa wakibezwa kwa kile kinachonadaiwa wanamuogopa Mheshimiwa Rais na hawawezi kumsogelea na kumpa ushauri.
“Naenda kinyume na kauli hiyo kwani hao wanaosema hivyo hawaoni tunachokifanya kuzunguka usiku na mchana kutatua kero za wananchi hii ni katika kutekeleza azma ya chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla ya kuwafikia wanachi na kusikiliza na matatizo yao, juzi nilikuwa Kahama, nikaenda Geita na Singida na leo nipo Hapa Mwandoya ningefika vipi huko bila wananchi kuleta shida zao”. Alisisita Mpina.
“Serikali imeweza kurudisha Hekta nyingi za ardhi zilizokuwa zikimilikiwa na watu binafsi kama Sumaye na zitarudishwa kwa wananchi, leo mnasema vipi Mawaziri wa Magufuli hawamshauri”. Aliuliza Mpina.
Akiendelea kuongea na wana Kisesa Mbunge wa Jimbo Hilo Naibu waziri Mpina, aliongeza kwa kusema kuwa, Pia Ndege aina ya Bombardier Q400 zilizonunuliwa na serikali pamoja na upanuzi wa barabara akitolea mfano wa Barabara ya Mwenge Jijini Dar es Salaam na Barabara ya Airport ya Mwanza, vyote vimefanyika na bado watu wanabeza bila kuona kama Mawaziri wana Mchango na wanamsaidia Mhe. Rais Magufuli.
Akiendelea kusikiliza changamoto za wanakisesa ikiwa ni pamoja na changamoto ya eneo la makaburi na standi ya Mwandoya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu Bw. Mussa Isaac Mpina alilitoea ufafanuzi na kusema kuwa jambo hilo lipo katika mpango wa fedha wa mwaka unaokuja hivyo linasubiri utekelezaji.
Akizitaja baadhi ya changamoto zilizotatuliwa Jimboni Kisesa ikiwa ni pamoja na Barabara, Mitandao ya simu, upatikanaji wa maji safi na salama, na kuwepo kwa Zahanati katika mji mdogo wa Mwandoya, Mhe Mpina alisema kuwa ndani ya muda Mfupi zahanati hiyo itapata vifaa vya kisasa vya Ultra-Sound, X-Ray na Fridge la kuhifadhia Damu kwani Zahanati hiyo imeshakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji na kutoa huduma ya uzazi.
Akiongea kabla ya kuanza kwa Mkutano huo Diwani wa kata ya Lugeka CHADEMA mhe.Zakayo Sarya Maarufu kwa jina la Trump, alisema uchaguzi uliisha wakati alipotangazwa mshindi, kazi inayofuata ni utekelezaji wa masuala ya maendeleo bila kujali itikadi za vyama vyetu.
“ Nawashangaa sana wapinzani wenzangu wa wanaobeza mambo mazuri anayofanya Mhe, Rais mimi Binafsi nampongeza sana kwa jitihada zake za kuleta maendeleo bila kubagua vyama, rangi, dini wala kabila.
Awali akihutubia Mkutano huo Naibu waziri Mpina aliwashuru wana Kisesa kwa kumuamini na kumuweka madarakani tangu 2005 akiwa kijana mdogo na kuhaidi kuwatumikia bila ubaguzi wa aina yoyote kwa manufaa ya taifa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »