Foundation
for civil society ambao ni asasi huru imetangaza kutumia utaratibu wa JUMANNE YA KUTOA (GIVINGTUESDAY) utaratibu
ambao unatumika duniani kote kwa ajili ya kuhamasisha watu na jamii kuwa na
moyo wa kujitolea kwa ajili ya wahitaji ambapo asasi hiyo imetangaza
kuadhimisha siku hiyo hapa nchini kwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanaosoma
katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko
ikiwa ni mara ya kwanza kwa Asasi hiyo kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Akizungumza
na mtandao huu katika mahojiano maalum leo Martha Olotu ambaye ni
Busness,Development and Partinaship Manager wa Asasi hiyo amesema kuwa FCS
inalenga kutumia Utaratibu wa Jumanne ya Kutoa kwa namna ya kuhamasisha Moyo wa
kujitolewa kwa wenye Uhitaji,ikiwa ni Jitihada za ulimwengu ambazo zilizinduliwa
Rasmi Tangu mwaka 2012 na shirika la New York’s 92nd streat Y kwa
ushirikiano na UN Foundation,Lengo likiwa ni kuweka siku maalum kwa ajili
kuheshimu na kuadhimisha ukarimu katika
kutoa,ambapo kwa sasa siku hii imekuwa ikiadhimishwa na nchi nyingi Duniani
ikihusisha makampuni Binafsi,watu binafsi,familia na asasi za kiraia.
Akizungumzia
maadhimisho hayo ambayo yatafanyika Tarehe 29 mwezi wa November Karin Rupia
Ambaye Ni Resource Mobilization Executive Kutoka katika asasi hiyo amesema kuwa
shirika hilo litakabidhi michango iliyotolewa, na kujiunga kufurahi na watoto
kwenye shughuli kama kupima afya za watoto hao,kuchora na watoto,kucheza na
watoto kusafisha watoto pamoja na kuwasomea watoto hao wa shule ya msingi Uhuru
mchanganyiko.
Kwa
maelezo zaidi Juu ya siku hiyo unaweza kutizama HABARI24 TV kwenye Youtube account yetu hapo.
EmoticonEmoticon