Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza na
Uongozi wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Jane Goodall, mara baada ya
Mhe. Waziri Makamba kutembelea Ofisi zao Kigoma Mjini. Wa kwanza kulia
ni Bi. Mary Mavanza Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa kuhifadhi mfumo wa
Ikolojia Ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma Bw. Samson Anga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiwa katika boti
Maalumu kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe
Bw. Donatus Bayona (kulia) na Bi.Happy Kiyemi Mkuu wa Idara ya Utalii
wakimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. January Makamba kutembelea Hifadhi ya Gombe
………………………………………………………
Na Lulu Mussa- Kigoma
Shirika lisilo la Kiserikali la
Jane Goodall linalojishughulisha na Mradi wa utafiti wa sokwe na
wanyamapori wengine limepongezwa kwa jitihada zake za kutunza mazingira
na kusaidia jamii kuhifadhi mfumo wa ikolojia ukanda wa Magharibi mwa
Tanzania.
Pongezi hizo zimetolewa leo na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
January Makamba mara baada ya kutembele Ofisi zao Mkoani Kigoma. Waziri
Makamba amesema kuwa Shirikal hilo la Jane Goodall limekuwa mstari wa
mbele katika kubuni miradi ambayo inagusa jamii moja kwa moja.
Akitoa maelezo ya shughuli
zinazotekelezwa na shirika hilo kwasasa, Naibu Mkurugenzi wa Bi. Mary
Mavanza amesema kuwa wanatekeleza miradi mitatu ikiwa ni pamoja na Mradi
wa utafiti wa sokwe na wanyamapori, Mradi wa Mizizi na chipukizi ambao
unatekelezwa nchi nzima katika shule zote na mradi wa uhifadhi
unatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za Mpanda, Nsimbo kwa Mkoa wa
Katavi na Uvinza kwa Mkoa wa Kigoma.
Aidha, Shirika hili pia
limefanikiwa kuhamasisha wanajamii 42 kufanya shughuli za kukuza kipato
ambazo ni rafiki kwa mazingira kupitia ufugaji nyuki na huduma za ki
ikolojia. Pamoja na mafanikio hayo shirikali hili limewasilisha hoja ya
kwa Waziri Makamba kusaidia kukamilika kwa Mchakato wa kupandisha hadhi
ya ardhi jumla kuwa misitu ya Hifadhi ya Wilaya ili kudhibiti idadi
kubwa ya sokwe waliobaki Tanzania ambao kwa sasa hawana ulinzi thabiti.
Taasisi ya Jane Goodall
liliasisiwa miaka 56 iliyopita na mtafifiti Dr. Jane Goodall kwa lengo
la kufanya shughuli za kitafiti, kurejesha uoto wa asili uliopotea na
kuhakikisha wanajamii wanaboresha uchumi wao kwa kutumia maliasili
zinazowazunguka.
Waziri Makamba pia ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa lengo la kufuatilia changamoto za kimazingira Hifadhini hapo.
EmoticonEmoticon