Mkuu wa
Wilaya ya Kilombero James Ihunyo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba katika
mkutano na wananchi katika Kijiji cha Katarukila akiwa ni muendelezo wa ziara
yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Katurukila na kuwapongeza kwa kuwa Kijiji cha mfano
kwa kuonyesha jitihada za dhati za kuhifadhi mazingira.
Bwana
Candidius Songela akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira January Makamba akingalia ramani inayo onyesha eneo lenye mgogoro
baina ya wanakijiji wa Katarukila na mwekezaji. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya
Kilombero Bw. James Ihunyo.
Na Lulu
Mussa,Kilombero
Wananchi wa Kijiji cha Katurulika, Wilaya
ya Kilombero, Mkoani Morogoro wameahidiwa Mifuko mia moja ya saruji ili
kukamilisha ujenzi wa zahanati katika
tarafa yao inayohudumia wakazi wa vijiji sita.
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kutoa mifuko
hiyo ndani ya wiki moja ikiwa ni pongezi kwa Kijiji hicho kwa kuwa mstari wa
mbele katika kuhifadhi mazingira na msitu wa Magombera.
Awali, Bwana Dandidius Songela alimfamisha Waziri Makamba
changamoto wanazokutana nazo katika Kijiji chao kuwa, ni pamoja na mgogoro
baina ya Kijiji cha Katarukila na mwekezaji anayehodhi sehemu ya eneo la Kijiji
na kusababisha uharibifu wa mazingira. Waziri Makamba aliwasihi wanachi wa
Kijiji cha Katarulika kuwa ni jukumu lao
msingi kulinda msitu huo kwa nguvu zao zote
na kubainisha kuwa Hifadhi endelevu ya mazingira ndio mustakabali wa maisha
yao.
Waziri Makamba ameliagiza Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) kumpa mwekezaji huyo
"Restoration Order" kwa mujibu
wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa
kumtaka arejesha mazingira katika hali yake ya asili, kwakuwa ni eneo tengefu.
kwa upande mwingine Waziri Makamba
amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya
Kilombero Bw. Dennis Londo kuhakikisha wanasheria wa Manispaa wanahudhuria kesi
baina yao na mwekezaji huyo bila kukosa kila inapotajwa na baada ya kuhumu
kutolewa Waziri Makamba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa
(TAKUKURU) kuchunguza kwa kina endapo kulikua na mianya yoyote ya rushwa katika
mchakato wa kumilikisha ardhi ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara.
Waziri Makamba yuko ziarani Kilombero
kuangalia changamoto za mazingira na awali alitembelea Mto Mkondoa Wilayani
Kilosa.



EmoticonEmoticon